Shule: Wapi nimpeleke mwanangu?

Shule: Wapi nimpeleke mwanangu?

nimesoma humu watu wengi wanasema watoto wa darasa la kwanza wanafanyiwa interview, mtoto wa darasa la kwanza hafai kufanyiwa interview this is wrong. kinachotakiwa kufanyika ni kithibitisho tu kama anaweza kuanza darasa la kwanza kutoka kwa walimu wake wa vidudu. nadhani hiyo interview inatumika kama ukiuliza kwa nini mwanangu hajapata nafasi utaambiwa kafeli iterview.
embu fikiria unaambiwa mwanao kafeli interview darasa la kwanza na wengine wamefaulu, eti hana hakili za kujiunga na shule hii???
wazazi wa JF kwa kuwaona watoto wao wana akili kabla hata hawajaanza real shule kiboko..

kuna mtu amesema mwanawe anajua kusoma kabla hajaanza la kwanza...
jamani a e i o u abcd et al sio kujua kusoma.....

ni vigumu sana kujua kama mwanafunzi atakuwaje au anaakili kiasi gani kwa ajili wengine wanachelewa kuonyesha dalili zao.....
mwalimu wa shule ya msingi kazi yake ni kumnoa mtoto na kuhakikisha ananawiri kielimu. madhumuni makubwa ya shule ya msingi ni kuhakikisha mwanafunzi anaweza kuyajua mambo mawili muhimu lugha na hisabati kwa ajili haya ndio mambo ambayo atakumbana nayo katika maisha yake yote. kwa mlio nje mtaelewa jinsi nchi za wenzetu hata form 6 bado wanataka uwe umefanya vizuri kwenye english na hisabati(uk).

kuhusiana na shule bwana max kuna mambo mengi ya kuzingatia wakati unamchagulia shule mwanao.....
1. ufundishaji kama watu wengi humu ndani walivyoongelea
2. mazingira ya shule ilipo ni muhimu sana
3. vitu vilivyopo shuleni je shule ina viwanja vya michezo hichi ni kitu muhimu sana kwa mtoto na watu wengi wanaki overlook. mtoto anapocheza ni vizuri kwa afya yake obesity ni hatari, anaweza akawa na talent nyingine ambayo sio masomo, pia mtoto anakuwa na furaha na hichi ni kitu muhimu ambacho kinamfanya mtoto apende kwenda shule. embu fikiria wewe ukicheza na mtoto wako anapata furaha kiasi gani.
4. tabia za wanafunzi mimi nilipata bahati ya kusoma shule hizi za private (nairobi) nikiwa secondary watoto wengi ambao wazazi wao wanazo huwa wanakuwa na kiburi cha kuzarau kusoma na kudhani kwamba hela kwao zitakuwepo milele. kama mkuu YE hapo juu anvyosema ni wizi wa pesa tu.

5. na kama ulivyosema ni bweni - uangalie menu ya shule ikoje ili kuepusha kuingia gharama za kununua vitu vya kula kula.
6. inabidi na wewe uwe unafatilia progress yake hichi ni kitu muhimu sana

Semilong,

Na mimi nimechoka akili kusikia wazazi wa JF wanashabikia kitoto cha vidudu kufanyiwa "interview" ya kujiunga na darasa la kwanza. Kama unavyosema, wengine wanachelewa kuonyesha uwezo wao. Albert Einstein hakuwa genius darasani. Alifanya dead end jobs kabla ya kutulia na kuja na Nadharia Maalum ya Uwiano. Eti unamfanyia mtoto wa vidudu "interview." "Interview" ya kutathmini kama anajua kusoma na kuandika?

Kuna kitu umesisitiza, Semilong, kuhusu kufuatilia maendeleo ya mtoto. Nilitaka nikwambie tu, usije ukamfundisha mwanao maneno "hichi kitu," "hana hakili," "embu fikiria."

Hiki, akili, hebu.
 
...
If it was me i would have recomended Muhimbili primary school mbona nishule nzuri tuu

Hapo Muhimbili Primary School wanaanzia na elementary school? Na je kwa upande wa secondary, ukiacha IST, ni shule gani nyingine zinatumia mtaala wa nje ya Tanzania ambazo zipo Dar?

...
...wanafundisha kutoka na na mtaala huo huo wa nje ila sema wao kwa kiswahili.

Je Muhimbili nao wanatumia IB curriculum isipokuwa wao wanafundisha kiswahili?

Asante.
 
Anyway mimi nashindwa hata kushangaa hapa, watu mmeombwa ushauri /information zitakazo msaidia Max kuamua wapi ampeleke mtoto wake, sasa mjadala wa kama interview kwa watoto ni sahihi au si sahihi unakujaje hapa? kama tunataka kujadili hili ianzishwe thread nyingine, ila hapa tumpe ushauri /information itakayomsaidia Max kwanza.

Mkuu max,

Zingatia ushauri wa ndugu Maane, naungana naye 100% labda tu wadau wengine wakuletee shule nyingine za namna hiyo zilizopo mikoani pia ili upate a wider choice! Nyingine hapa zitakuwa ni bla bla tu ndugu yangu!
 
Je kuna shule nyingine yeyote unayoijua yenye kufundisha kwa kutumia mtaala wa nje, na shule hiyo iko Dar, na inayochukua watoto kuanzia elementary school? Kwa ajili ya watoto walioanza masomo nje ya nchi na wanaotegemea kuendelea na masomo nje ya nchi hapo baadae.

Mama,
Unaweza kujaribu Dar es Independent School.Ni same standard na IST( International School of Tanganyika) ila wao fees iko kidogo chini ukilinganisha na IST.Inaanzia from KG to High School - Form VI.
Many expatriates wanapeleka watoto wao pale na ni shule nzuri.
 
Mama,
... Dar es Independent School.... wao fees iko kidogo chini ukilinganisha na IST. Inaanzia from KG to High School - Form VI.
....

Nashukuru sana kwa maelezo muafaka kabisa. Asante kwa Mwanzilishi wa thread hii, na pia Maane na wengine waliotoa mitazamo yao.
 
Mama unaweza kujaribu shule kama Laurette.

Vile vile kuna shule ambazo ziko accredited na Council of International Schools
-Aga Khan Mzizima Secondary School(IB and IGCSE/GCE)
-Haven of Peace Academy(UK) CIS Members Directory
 
Max mpeleke MANZESE PRIMARY SCHOOL aende kuchangamka then sekondari kama ni binti mpeleke MARIAN GIRLS
 
Mie natafuta shule nzuri ya kawaida ya sekondari kwa ajili ya mwanangu wa kiume ambaye kamaliza form four na nahitaji kumpatia shule nzuri kwa ajili ya masomo ya A level.
Hizo international schools siziwezi, lakini kama kuna shule zingine nzuri zinazotumia mtaala wa hapa hapa kwetu danganyika naomba nifahamishwe. Naungana na Max, nahitaji sana!
 
Shule yenye rekodi nzuri muda mrefu (boarding na day) kwa Mwanza ipo inaitwa Nyakahoja Primary (shule iko chini ya masista). Fees should be very reasonable, bei zake sio za International level. Ila wengi waliopitia hapo wanafanya vizuri sehemu mbali mbali nchini na nje ya nchi.
Pia kuna Isamilo International School (Mwanza). Na kama walivyosema wengine St. Constantine (Arusha - International wannabees), ISM (Moshi na Arusha Branch) na IST. Inategemea na mfuko wako.
ISM na IST wanafanya IGCSE mpaka form 4. halafu 5 and 6 ni IB (fees bonyezeni kwenye website). Kama una mfuko, bania bania halafu jipinde umweke mtoto wako asome IB. Hapo utakuwa umemonita tabia ya mtoto wako mpaka umzogeze afanye IB. By the time unamweka IB unajua ur money is worth investing. Kama zinacharge, IB is the key to any university in the word! Marekani tena unaweza hata ukaruka modules au hata 1st year of University.

Nimepitia njia hizo, na ni kweli, kama mtoto wako hajatulia akili (hata kama ni bright), ataishia kuvuta bangi, ulevi, kubwia na kutoka kavu, na utalia investment yako. Hii haihusiani na shule, ni tabia ya mtoto tu kupapatika na freedom entrusted on them. Tabia ya kusema sijui shule inawaharibu au haiwadiscipline ni uongo. Inabidi watu tufike umri fulani tukubali responsibitilities zetu kama individuals, wazazi na familia etc. Kama mtoto anapapatika na bangi atavuta tu, nothing to do with the school.

Benefit ya IB, unakuwa multi-cultured. Unajifunza kuwa critical thinker. The freedom you are given to express yourself stays with you. Nothing phases you!! IB inakufanya uwe complete, una mix masomo yote more or less from arts to sciences, wewe unachagua masomo 3 ufanye katika higher level, na matatu katika subsid level, plus compulsory Theory of Knowledge and creatice action service (CAS - helps you be socially responsible to the society around you). Kama strength yako ni Sciences, unaweza chukua Physics, Chemistry, Biology/Maths at higher level, halafu unachukua economics, language etc at subsid level. Kama arts ni strength yako, unachukua arts at higher level, halafu sciences at subsidiary level. This is what makes IB hot katika university nyingi/anywhere in the world, maana you are a well rounded person (yaani hujafocus kwenye kusoma tu PCM au PCB etc ambayo kwakweli ina narrow ujuzi wako).

Lakini kama mfuko hautoshi, haiwezi zuia mtu yeyote kufika anakotaka. Pia unaweza usispend pesa kubwa mtoto wako akaparamia tu mabangi!! Life is about risks.

I highly recommend Nyakahoja, sijapita, ila naijua sana. Ni ya kikristo, ila waislamu kibao wamepita hapo. Nina marafiki wa kiislamu wamepita hapo, and they are the most objective Islamic people I know. Kwa waislamu, mimi na encourage upeleke mtoto wako katika shule hizi, na kama ndugu aliyeweka mfano hapo juu...wewe kama mzazi jua responsibility yako nyumbani kumfundisha dini yako, lakini jua anapata kisomo kizuri sana.
 
Pia kuna Isamilo International School (Mwanza). Na kama walivyosema wengine St. Constantine (Arusha - International wannabees), ISM (Moshi na Arusha Branch) na IST. Inategemea na mfuko wako.
ISM na IST wanafanya IGCSE mpaka form 4. halafu 5 and 6 ni IB (fees bonyezeni kwenye website). Kama una mfuko, bania bania halafu jipinde umweke mtoto wako asome IB. Hapo utakuwa umemonita tabia ya mtoto wako mpaka umzogeze afanye IB. By the time unamweka IB unajua ur money is worth investing. Kama zinacharge, IB is the key to any university in the word! Marekani tena unaweza hata ukaruka modules au hata 1st year of University.

Nimepitia njia hizo, na ni kweli, kama mtoto wako hajatulia akili (hata kama ni bright), ataishia kuvuta bangi, ulevi, kubwia na kutoka kavu, na utalia investment yako. Hii haihusiani na shule, ni tabia ya mtoto tu kupapatika na freedom entrusted on them. Tabia ya kusema sijui shule inawaharibu au haiwadiscipline ni uongo. Inabidi watu tufike umri fulani tukubali responsibitilities zetu kama individuals, wazazi na familia etc. Kama mtoto anapapatika na bangi atavuta tu, nothing to do with the school.

Benefit ya IB, unakuwa multi-cultured. Unajifunza kuwa critical thinker. The freedom you are given to express yourself stays with you. Nothing phases you!! IB inakufanya uwe complete, una mix masomo yote more or less from arts to sciences, wewe unachagua masomo 3 ufanye katika higher level, na matatu katika subsid level, plus compulsory Theory of Knowledge and creatice action service (CAS - helps you be socially responsible to the society around you). Kama strength yako ni Sciences, unaweza chukua Physics, Chemistry, Biology/Maths at higher level, halafu unachukua economics, language etc at subsid level. Kama arts ni strength yako, unachukua arts at higher level, halafu sciences at subsidiary level. This is what makes IB hot katika university nyingi/anywhere in the world, maana you are a well rounded person (yaani hujafocus kwenye kusoma tu PCM au PCB etc ambayo kwakweli ina narrow ujuzi wako).

....

Asante kwa maelezo haya.
 
Yeah its damn expensive. My son wanted to join Moshi International school for Diploma 1 (that is what we call form 5) its UDS 16800 per year for borders. So if you are looking for that kind make sure ya pocket is ,,,, u know!
No EPA money please!

It is now usd-20,000+ for borders hii ni 2009/2010
 
Maane,

Mie mtoto wangu Muislam je watampokea ktk hizi shule?
Watampokea tu, dini sio kigezo cha kumregister mwanafunzi, wala usihofu kwamba ataondolewa relini. They are teaching academics subject and not religion subjects and mybe so moral stuff here and there!
 
"Interview" maana yake nini?

Kwa kiswahili maana yake ni usaili/kusaili.

Kimsingi wanataka kumhoji mtoto na kung'amua vitu (vipaji, uelewa nk) vilivyojificha ambavyo huwezi kuvijua kwa mtu kuandika au kuangalia rekodi nyingine. Kimantiki, sioni ubaya katika hili kwa sababu kwanza analinganishwa na watoo wa rika lake na sio watu wazima na pili inawapa walimu fursa ya kumfahamu mwanafunzi wanayetaka kum-enroll.

Nadhani kuna philosophical problem (si Tanzania pekee) kwa taasisi za elimu kuchagua wanafunzi wanaoonekana wana uwezo kiakili ili kujiunga na taasisi hizo.

Kama lengo la shule ni kuondoa ujinga, nilitegemea wale wanaoonekana wajinga zaidi ndio wapewe nafasi ya mwanzo ya kujifunza! Sioni mantiki ya shule kujisifu kufaulisha wanafunzi kama ilichagua wale wenye uwezo tu. Uwezo wa mwalimu/taasisi ya elimu unapaswa kupimwa kwa umahili wao wa kufaulisha wanafunzi ambao awali hawakuwa na uwezo (i.e. walikuwa wajinga)!
 
Mpeleke Alhassan Mwinyi Primary School, iko MIkocheni ni nzuri mwanangu anasoma pale darasa la nne.

Nenda kaone uchague
 
Maxence, there you are. Hakuna headache kwa sasa kama kupata shule bora ya msingi then Secondary. Mtoto anakuwa nursery school, ok ila tu anapo turn 5 unaanza kuwaza shule ya kumpeleka ndo ngoma inaanza. Kuna shule ambazo wazazi huwa wanasema ni nzuri kwa primary (academy) na baadhi ni kama:

1. St. Joseph Millenium Schools iko chini ya Jimbo la Dar es Salaam (pale Forodhani) ila kasheshe ni kuipata maana ni lazima uhakikishe mtoto wako ni extra bright ili aweze ku compete interview. Pale Sr. ambaye ni Headteacher ni strict sana, waalimu wote ni diploma na degree tu. Ada ni 1.5 million per year (3 terms including transport) excluding uniforms na vitu vingine vidogovidogo. Mtoto wa ndugu yangu anasoma hapa. Ni hatari, yupo std four lakini wa form one hampati kwa masomo ya nature kama science. Pia naamini kwa masomo mengine wapo juu sana. Ni boys na gilrs. Wanafaulu wote darasani kila mwaka isipokuwa tu mwaka wa kwanza walipoanza 2003 kwa sababu walianzia darasa la nne kwa kuokoteza wanafunzi toka shule zingine wakawakarabati na akafeli mmoja tu. Ila kama nilivyosema, mtoto wako huyo ni lazima kichwani ziwe zinachemka, pale ni pagumu kupata maana pia wana stream moja tu. Pengine mwaka ujao wanaweza kuwa na streams mbili kwa darasa la 1 kwani sasa serikali imesharudisha majengo kwa jimbo 100% tangu mwaka huu na waalimu wa forodhani wameshahamishiwa shule nyingine. Form four ya mwisho ni ya mwaka jana, hakuna mwanafunzi wa secondary tena. Pengo ana mpango wa kuifanya boarding (primary) ila ni mpaka waweke infrastructure na ukarabati wa majengo yaliyokuwa ya secondary maana yamechoka mbaya kabisa.

2.Tusiime Nursery and Primary Tabata

3. St. Teresa iko Ukonga

4. Christ the King iko Tabata

Zote ni kwa upande wa DSM. Sina details kwa 2-4.

Mtoto wangu wa kiume alisoma St Teresa akiwa Primary, ni nzuri na alikuwa anafanya vizuri. Tatizo hawakuwa na Boarding ikawa inakuwa ngumu kuendelea kumuacha pale.

Mwaka au miezi 18 iliyopita waibadilishiwa Headmistress, sasa sijasikia iwapo ujio wa Head mpya umeboresha au umeshusha kiwango. Ni muhimu kufuatilia.
 
Kwa kiswahili maana yake ni usaili/kusaili.

Kimsingi wanataka kumhoji mtoto na kung'amua vitu (vipaji, uelewa nk) vilivyojificha ambavyo huwezi kuvijua kwa mtu kuandika au kuangalia rekodi nyingine. Kimantiki, sioni ubaya katika hili kwa sababu kwanza analinganishwa na watoo wa rika lake na sio watu wazima na pili inawapa walimu fursa ya kumfahamu mwanafunzi wanayetaka kum-enroll.

Nadhani kuna philosophical problem (si Tanzania pekee) kwa taasisi za elimu kuchagua wanafunzi wanaoonekana wana uwezo kiakili ili kujiunga na taasisi hizo.

Kama lengo la shule ni kuondoa ujinga, nilitegemea wale wanaoonekana wajinga zaidi ndio wapewe nafasi ya mwanzo ya kujifunza! Sioni mantiki ya shule kujisifu kufaulisha wanafunzi kama ilichagua wale wenye uwezo tu. Uwezo wa mwalimu/taasisi ya elimu unapaswa kupimwa kwa umahili wao wa kufaulisha wanafunzi ambao awali hawakuwa na uwezo (i.e. walikuwa wajinga)!

Walimu kumfanyia usaili sio tu kwamba wanapima uwezo wa mtoto. Mtoto wa miaka 5 akifanyiwa usaili ni kipimo kizuri kujua nyumba anayotoka ni ya namna gani. Walimu wanajua hali halisi kuwa hata kama utamfundisha vizuri namna gani, nyumbani nako lazima kuwe kumetulia katika kukuza ipaji. Tatizo ni kuwa wazazi wengi wa kitanzania tunapenda mno kukaa baa..!!
 
Kwa upande wa shule zenye mitaala ya nje ya Tanzania, International school of Tanganyika ni mojawapo.

Mwenye kujua zaidi kuhusu hii shule anaweza kusaidia.

Mimi nilifukuzwa hii shule nilipokua grade 1 for a very minor one-off offence. Nadhani I was 5 years old. Kwakweli hiyo dismissal ilikua unfair. When I look back, nadhani it had something to do with my race. Natahadharisha tu kama mtoto wako sio mzungu.
 
Unajua wengine hapa tulisoma shule za sikinde za watoto wa wakulima, lakini haidhuru tunaweza kuwa na mawili matatu.

Kuhusu hizo shule za academy kwa kweli sina idea..maana sikuwahi hata kudream kwenda huko. Kama Maane alivyosema nadhani kwa kweli sasa hivi kwa watu wa kawaida ambao uwezo ni mdogo, tegemeo kubwa ni SHULE ZA MAKANISA. Shule za mission ni nzuri sana. LAKINI inabidi ufuate masharti yao. Kama wewe ni dhehebu lingine inabidi uwe tayari mtoto wako kupewa maadili ya kikatoliki au kilutheri.

Personally nimesoma mission and I can tell you for sure. Iam who Iam today kwa sababu ya yale maisha na songombingo za mapadre NA Mabruda. Kusali kila asubuhi...kuimba nk..It was all good. So Max..sijui uwezo wako..kama uko safi unaweza kufuata ushauri wa wakubwa humu kuhusu hizi International Schools. Ila kama ndo uwezo mdogo..think shule za makanisa.

Ila kitu kimoja ambacho nimeona humu: Kwa kweli TANZANIA kadri siku zinavyokwenda thamani ya elimu inayotolewa na serikali inazidi kushuka. Maana hakuna hata mmoja aliyeshauri jamaa aende shule za serikali. Jamani wananchi we need to do something..otherwise watoto wetu watakosa elimu bora na watakuwa wapagazi wa hawa wanaoenda IST na kwingineko. I can tell, mtu wa Kigoma huo uwezo wa IST hana..sasa jamani something must be done to help this poor guy..na yeye aje kucompete na wengine.

Ushauri wangu: mpeleke mtoto shule ambayo utajua kabisa atapata maadili na elimu at the same time. Either of the two will be good for him/her
 
All in all, elimu inaanzia nyumbani.

Kama nyumbani kuna mazingira mazuri ya kumwezesha mwanafunzi kujisomea na kuelimika, mtoto atafanya vizuri shuleni. Kama mtoto analelewa na watu wanaopenda maarifa, hata shuleni atafanya vizuri.

Mazingira ya nyumbani yakikaa kielimu, mtoto atafanya vizuri hata akipelekwa kwenye shule ya kata. Lakini watoto wanaotokea nyumba za hovyo, hata apelekwe International school gani atachemsha tu.

Shule inaanzia nyumbani.
 
Back
Top Bottom