Shule: Wapi nimpeleke mwanangu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shule: Wapi nimpeleke mwanangu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Maxence Melo, Apr 21, 2009.

 1. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #1
  Apr 21, 2009
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Wakuu,

  Najua kuna shule nyingi kwa hapa Tanzania. Kwa kuangalia matokeo tu naweza kuchanganya madawa.

  Ninachotaka kujua, ni shule gani ina

  • walimu walio committed,
  • mandhari nzuri ya kufundishia na kusomea
  • bweni (si kutwa)
  • Inaweza kuwa ya jinsia moja ama tofauti
  • Maadili mazuri kwa walimu wake na wanafunzi ambapo nitampeleka mdogo wangu akasomea kwa amani na kuwa na busara
  • performance yake inaridhisha katika mitihani iwe ni kwa kufuata mtaala wa Tanzania ama nje
  • gharama zinazoendana na ufundishaji na malezi (na ni kiasi gani?)
  Kifupi nahitaji kujua shule ambayo mdogo wangu (kwangu ni kama mwanangu tu) akisomea hapo (kuanzia msingi na kuendelea) nitajisikia kufarijika kuwa kalelewa katika maadili mazuri na amepata kujua mengi badala ya kukariri kwa ajili ya mitihani.

  Suala la gharama za masomo si tatizo japo ni muhimu kujua ili kulinganisha na ubora wa elimu inayotolewa.

  Nitashukuru kwa mapendekezo.
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Ndani ya Tanzania hii??
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Why not use NECT Results of 2008 to get the best 10 Schools in perfomance??

  Then choose One: Over kigezo cha mkoa, Masista n.k
   
 4. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwani shule zote za msingi Tanzania zinafanya mitihani ya Baraza la Mitihani?

  Shule inayotafutwa hapa, kama alivyoandika mwenyewe, ni hata zile zenye mitaala ya kigeni.
   
 5. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Maxence, there you are. Hakuna headache kwa sasa kama kupata shule bora ya msingi then Secondary. Mtoto anakuwa nursery school, ok ila tu anapo turn 5 unaanza kuwaza shule ya kumpeleka ndo ngoma inaanza. Kuna shule ambazo wazazi huwa wanasema ni nzuri kwa primary (academy) na baadhi ni kama:

  1. St. Joseph Millenium Schools iko chini ya Jimbo la Dar es Salaam (pale Forodhani) ila kasheshe ni kuipata maana ni lazima uhakikishe mtoto wako ni extra bright ili aweze ku compete interview. Pale Sr. ambaye ni Headteacher ni strict sana, waalimu wote ni diploma na degree tu. Ada ni 1.5 million per year (3 terms including transport) excluding uniforms na vitu vingine vidogovidogo. Mtoto wa ndugu yangu anasoma hapa. Ni hatari, yupo std four lakini wa form one hampati kwa masomo ya nature kama science. Pia naamini kwa masomo mengine wapo juu sana. Ni boys na gilrs. Wanafaulu wote darasani kila mwaka isipokuwa tu mwaka wa kwanza walipoanza 2003 kwa sababu walianzia darasa la nne kwa kuokoteza wanafunzi toka shule zingine wakawakarabati na akafeli mmoja tu. Ila kama nilivyosema, mtoto wako huyo ni lazima kichwani ziwe zinachemka, pale ni pagumu kupata maana pia wana stream moja tu. Pengine mwaka ujao wanaweza kuwa na streams mbili kwa darasa la 1 kwani sasa serikali imesharudisha majengo kwa jimbo 100% tangu mwaka huu na waalimu wa forodhani wameshahamishiwa shule nyingine. Form four ya mwisho ni ya mwaka jana, hakuna mwanafunzi wa secondary tena. Pengo ana mpango wa kuifanya boarding (primary) ila ni mpaka waweke infrastructure na ukarabati wa majengo yaliyokuwa ya secondary maana yamechoka mbaya kabisa.

  2.Tusiime Nursery and Primary Tabata

  3. St. Teresa iko Ukonga

  4. Christ the King iko Tabata

  Zote ni kwa upande wa DSM. Sina details kwa 2-4.
   
 6. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Maane,

  Mie mtoto wangu Muislam je watampokea ktk hizi shule?
   
 7. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Tuangalie pia kama hizo performance unazosema ni genuine!!!! Je ni zile za kiukweli au ni zile za kupewa majibu??? Kwa kigezo cha shule za masista nakubaliana na wewe. Kwanza shule za kanisa ni nzuri sana maana zinafundisha na maadili pia. Kwa kweli kama ingewezekana kizazi cha leo ni lazima tungewasomesha primary na O-level shule za misheni. At least huko hata kama kuna utovu wa nidhamu lakini si kama shule za kawaida. Pia watoto wanaofaulu huko hata kama hawaongozi but wanakuwa na elimu bora ya kiukweli na wakienda sekondari huwa wanaogoza maana kufaulu kwa kulikuwa kwa ukweli.
   
 8. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mtoto anataka kuingia darasa la kwanza unamu interview nini sasa?

  Hiyo kwangu inanionyesha hao walimu unao waita strict wenye degree na diploma nao ni ovyo. Kwa hiyo, mtoto katoka vidudu unampa mtihani wa kuingia darasa la kwanza kuona kama alifuzu vizuri vidudu? Vidudu kuna mitihani siku hizi? Na kama hakwenda vidudu jee, huyo mtoto ni mjinga definately hafai hapo St. Joseph Millenium Schools, au?

  Hao St. Joseph Millenium Schools wanataka mteremko wa kufundisha vitoto ambavyo wanaona vitawarahisishia kazi. Sio ualimu huo.
   
 9. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #9
  Apr 21, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Watampokea bila kipingamizi. Kwa upande wa Millenium wanakueleza kabisa kuwa shule yao ni ya kanisa, hivyo watoto wanafundishwa somo la dini kwa wote na kwa mantiki ya Kikatoliki. Hakuna cha Lutheran, mara mlokole, Anglikan. Wote ni kupiga ishara ya msalaba tu. Waislam pale ni kibao na wazazi wako comfortable na Elimu. Ndugu yangu siku hizi kwa upande wa Elimu angalia substance na maadili kwa mtoto. Akirudi nyumbani mfundishe ya kwako ila kwa umakini sana ili asije akaleta masuala ya dini shuleni. Wa ndugu yangu si Mkatoliki na anasali kikatoliki hata akibariki chakula, na tunafurahia na kumpa moyo tu. Tunachotaka ni ile elimu na maadili. Na ana tabia njema siwezi kuelezea.
   
 10. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Kwa taarifa yako shule zote nzuri siku hizi za primary (private) mtoto haingii bila interview. Hata kwa za serikali siku hizi hakuna interview lakini ni lazima mtoto awe anafahamu kusoma na kuandika. Tena nikupe tahadhari kabisa hakikisha mtoto wako unamfundisha nursery course yote na akitoka hapo anajua kuandika, kusoma and speaking right english kama unataka afanye vizuri. Hayo ya kusubiri waalimu wakufunzie yamepitwa na wakati. Hakuna mtoto wangu aliyeanza shule bila kujua kusoma na kuandika at 5 years. At 3 years watoto wangu huwa wanaweza counting and aphabets kiasi and speaking english kiasi. Akiwa 4 years anasoma na kuandika and speaking fluently, and I am in Tanzania.
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Max umeowa juzi tu mtoto anataka shule mara hii?
   
 12. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #12
  Apr 21, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Jamani Masanilo. Kasema ni wa ndugu yake ila ni kama mtoto wake. Lakini hata hivyo kwani kale kamajaribio ka form six an form four kwani si ni katoto?? Tehe tehe mkuu Max. Ukitaka kujua kama kuna watoto wa majaribio basi wewe jaribu kuolewa na watani zangu Wangoni, yaani ukubali tu kupokea watoto wa majaribio si chini ya wanne!!! Yaani jamaa mabao yao ni mazito lazima keeper afungwe!!
   
 13. M

  Mama JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2009
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Kwa upande wa shule zenye mitaala ya nje ya Tanzania, International school of Tanganyika ni mojawapo.

  Mwenye kujua zaidi kuhusu hii shule anaweza kusaidia.
   
 14. Sasha Fierce

  Sasha Fierce JF-Expert Member

  #14
  Apr 21, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 362
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  Its good and expensive,inategemea na mfuko wako.
   
 15. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #15
  Apr 21, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Unamaanisha mtoto hufanyiwa interview wajue kama anajua kusoma na kuandika na kadhalika? Neno "interview" maana yake nini?

  Manake tusisema watoto wajue hili na lile na "fluently" na "kiasi" na kadhalika. Tuanze na wazazi kwanza.

  "Interview" maana yake nini?
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Apr 21, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  I couldn't agree with you more...
   
 17. M

  Mama JF-Expert Member

  #17
  Apr 21, 2009
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Je kuna shule nyingine yeyote unayoijua yenye kufundisha kwa kutumia mtaala wa nje, na shule hiyo iko Dar, na inayochukua watoto kuanzia elementary school? Kwa ajili ya watoto walioanza masomo nje ya nchi na wanaotegemea kuendelea na masomo nje ya nchi hapo baadae.
   
 18. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #18
  Apr 21, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Google plse..!
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Apr 21, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
 20. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #20
  Apr 21, 2009
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  To me what I believe hakuna mtoto mjinga hata siku moja. What we are after ni material gani unampa mtoto. Sasa kama hizo st zinazotaka watoto bright ni makosa. Tutambue kuwa ni haki ya kila mtoto kupata elimu bora. Je hao ambao tunawaita sio bright tunawatenga? Tuchukulie mfano, kwenye familia ya kila mtu anayesoma forum hii ni wote wana akili sawa? Mimi kaka yangu ana masters in science lakini mwambie akamate computer ajaribu kusearch mambo, ni sawa na mwanangu wa darasa la saba. Mimi nafikiri kwa level ya kuingia darasa la kwanza watoto waachwe waende, then tuwajenge kimasomo.
  Nikirudi kwenye mada shule ambazo zinafundisha vizuri kwa mtizamo wangu ni shule za makanisa. So ni vizuri ukaweka wazi kuwa ni shule za mikoa gani unatafuta ili kila aliye katika mkoa huo ambaye ni mwanaJF aweze kukupa data accordingly.
   
Loading...