ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,017
- 7,220
Max,
Samahani kwamba sitaweza kujibu swali lako la msingi katika kukusaidia kupata shule, ilaninaomba nichangie kidogo kwenye huu mjadala.
Ni vyema jamii ya kitanzania, hasahasa jamii ya wasomi, ikawa inafanya maamuzi yake objectively. Kweli watoto wetu wanachohitaji ni hizi shule za kulipa dola 10,000 kwa mwaka? Ninaposema tuwe objective namaanisha tuwe result oriented. Je watoto waliosoma kwenye hizi shule wamefanya nini kinachotuvutia na sisi kutaka kuwapeleka watoto wetu huko? je, wale waliosoma kwenye hizo shule wana mchango gani kwenye jamii yetu ya sasa kutokana na kile walichojifunza kwa gharama kubwa kuliko medical degree? Nitatoa mfano hapa, Mzumbe Secondary na Ilboru imetoa wataalam ambao wamejaa kwenye mahospitali yetu, wanafundisha kwenye vyuo vyetu, watafiti etc. Hawa waliosoma IST na ISM wako wapi? Harvard University imetoa viongozi katika nyanja mbalimbali za kisansi, kisiasi nk. IST na ISM zilikuwepo kabla hata ya kuanzishwa kwa utaratibu wa shule za watoto wenye viapji maalum, inakuwaje waliosoma kwenye hizi shule za watoto wenye viapji maalum tunawaona kwenye jamii lakini waliosoma IST na ISM hatuwaoni? Hii inanirudisha kwenye soma la falsafa ya udaktari, what is the meaning of good?- hili siyo swali rahisi, lakini kila mtu anaweza kujipatia jibu litakalomfaa.
Nadhani shule nzuri kwa mtoto ni ile ambayo kwanza ni salama kwake, pili ambayo itampa ujuzi utakaomuwezesha kuyamudu maisha yake na kuwa na nafasi na uwezo wa kushiriki katika kuendeleza jamii. Je, katika maeneo unayoishi hakuna shule yenye kumwezesha kijana wako kuyapata haya? Kama ipo hakuna haja ya kusita kumwandikishe mtoto huko.
Pia nitaandika kidogo kuhusu wazazi wanaowatafutia watoto wao shule za A-level. Mtoto aliyemaliza form four anategemewa kufahamu zaidi kuhusu shule za A-level kuliko wazazi wake(of course kama wazazi sio walimu). Kuna swala la combination, mtoto anatarajiwa kufahamu zaidi combination anayoipeda na kuimudu kuliko mzazi. Kwa Tanzania wanafunzi humaliza form four na umri wa kama miaka 17 hivi. Ni vyema wazazi wakawa na moyo wa kuwaamini watoto na kuwaacha wasimamie mambo wanayoweza kuyamudu.Nadhani swala kutafuta shule ya A-level mwanafunzi aliyemaliza form four anaiweza, wazazi/walezi wampe guidence na kumuwezesha financially. Hii ni katika kumjenga mtoto kujitegemea.