Mkoba wa Mama
JF-Expert Member
- May 5, 2021
- 280
- 173
Anayefanya vizuri lazima apongezwe na atambuliwe, haiwezekani mtoto amefanya vizuri mpaka kufikia kuwa Tanzania One lakini hatambuliwi na kupewa heshima yake, vilevile kwa shule zinazofanya vizuri zaidi.
Kama kuna kasoro na mapungufu, mamlaka husika ziyafanyie kazi na sio kuondoa utaratibu wa kutambua juhudi na kazi nzuri wanazofanya watu. Ni jambo la kushangaza sana kuona mamlaka inashindwa kushughulikia changamoto walizodai zinasababishwa na utaratibu huo na badala yake wakauonda, kwa hiyo tutasitisha mambo mangapi kwa kushindwa kutumia akili na uwezo wetu kutatua changamoto zinazojitokeza? Maana yake kuna siku wizara ya elimu itaacha kuandaa mtihani wa taifa kwa sababu kuna wizi na udanganyifu? Jibu ni hapana.
Ikiwa tu wafanyakazi huwa wanapewa tuzo na kutambuliwa kwa kazi nzuri walizofanya (wakati ni wajibu wao kufanya kazi nzuri na wanalipwa kwa ajili ya kazi hizo) kwa nini tusiwatambue na kuwapongeza hadharani na kuwapa heshima yao watoto wanaofanya vizuri katika masomo yao pamoja na shule bora?
Huu ni udhaifu mkubwa sana, kama kuna changamoto, Prof. Mkenda aangalie namna ya kuzitatua na sio kuondoa utaratibu huu mzuri uliokuwepo.
Wizara inaweza kuweka utaratibu wa kuwatambua wanafunzi bora kulingana na tahasusi (kwa kidato cha sita) mfano, wanafunzi bora kwa wanafunzi wanaochukua masomo ya sayansi, biashara, sanaa n.k, Kwa upande wa shule wazigawe katika madaraja na idadi ya wanafunzi, mfano, shule za daraja la kwanza (zile za vipaji maalum), daraja la kati na daraja la chini (kwa shule mpya au shule za pembezoni ambazo bado kimiundombinu na kitaaluma hazijajua sana) au utaratibu wowote ambao utafaa. Lakini hoja ya kusema utaratibu wa kutangaza wanafunzi na shule bora unapelekea wizi wa mitihani na kugeuka kama sehemu ya biashara kwa shule binafsi ni ufinyu wa kufikiri na ukwepaji wa wajibu kwa mamlaka husika.