[
Mkuu huwezi kunukuu mchango wa MBUNGE akiwa bungeni na mchango wa kiongozi mwenyekiti akiwa ktk mihadhara ya hkuhutubia. Watu hawa hawa unewabadilisha sehemu zao ungesikia yakizungumzwa haya haya na mtu tofauti. Zitto akichagia bajeti ya niashati na madini hawezi kuzungumzia Education, education education wala Mbowe akiwa pale hawezi kuzungumzia Ufisadi wa wizara ya nishati na madini..Kila maneno yana mahala pake!Ni muda sasa unapita tangu tetesi na wakati mwingine si tetesi bali mazungumzo ya baadhi ya viongozi wa Chadema kuhusu Zitto kuonyesha kuwa ni mtu asiyehitajika kwa sasa ndani ya Chama.
Mwenendo wake ambao hata mimi siukubali umezidisha ari ya wengi wa wanachama na wapenzi wa Chadema washindwe kuhimili subra na uvumilivu kiasi cha kutumia kila fursa wanazozipata za kumjadili Zitto (mara nyingi huwa mitandaoni) kuonyesha wasivyomkubali kiongozi huyu.
Juzi, wakati Mhe. Freeman Mbowe alipokuwa akizungumza wakati wa kuchangia kampeni za vuguvugu la mabadiliko alitoa kauli ambayo kwangu mimi na wengie wenye akili tuliamini kuwa inakwenda kinyume na matwaka, mapenzi, mahitaji na fikra za Zitto mwenyewe. Ingawa sitaweza kusema neno kwa neno, angalau nirudie matamshi ya Mwenyekiti katika muktadha wa maudhui yale yale aliyotaka tuelewe. Mwenyekiti alisema hivi ..."Priority number 1 ni Education, Number 2 ni Education na number 3 ni Education.... akaendelea akasema, tunataka wabunge wa Chadema mwaka 2015 wafike 150. N a fucus yetu kwa sasa katika hilo SIO KUJUA nani atakuwa mbunge, na pia kwa sasa hatuhangaiki na kujua NANI ATAKUWA RAIS...."
Kwa matamshi hayo ya mwenyekiti, ukilinganisha na yale ambayo Zitto mwenyewe amekuwa akiyahubiri siku za karibuni pamoja na wapiga propaganda wake wa gazeti la Mwananchi ni dhahiri kwamba utaona Zitto anazungumza vitu ambavyo kwa sasa SIO focus ya chama. Na kama hivyo ndivyo sishangai kuona viongozi wengi wa Chama wakikwazika na matamshi ya Z
itto. Lakini sio kwambaq Zitto hajui kuwa viongozi wenzake hawafurahishwi na kauli zake. Kwa nini anaendeleza mivutano hiyo isiyo na maana, yeye mwenyewe anajua.
Nimepata bahati ya kuwa karibu na baadhi ya viongozi wa juu wa Chadema wakiwamo wabunge. Wengi hawamwoni Zitto kama ni kiongozi wanayemtaka. Na baadhi yao wapatapo nafasi husema wazi kuwa Zitto ni mharibifu wa Chama kwa sasa.
Kauli rasmi ya Chama kuhusu matamshi ya Zitto na namna Zitto anavyokiharibu chama kwa kuunda mtandao wa makundi hasa kundi lake litakalotetea na kupigania dhamira yake ya kutamani kuwa Rais kabla muda rasmi wa Chama kutangaza azma zenye mwelekeo huo ingali kutolewa.
Wakati Chama kikihofia au kikimwogopa Zitto, magazeti nayo hayako nyuma kuongeza petroli kwenye moto. Mojawapo ni hili hapa la HOJA.
Viongozi wa Chadema, jitokezeni hadharani. Mkubali au Mpinge harakati za Zitto na kama Zitto yuko pamoja nanyi tunajua atashiriki na yeye kutoa ufafanuzi wa maoni yake kwa kauli ya chama kuhusu Urais.
Mnapokaa kimya, hoja za UDINI na UKANDA zinazochochewa na CCM pamoja na baadhi ya vyombo vya habari zitashamiri na mwisho wa siku chama kitashindwa kujipatia wanachama zaidi kwa kuaminishwa kuwa Zitto anachukiwa kwa sababu ya dini au ukanda anaotokea.
Na Zitto mwenyewe pia ninamshauri ajitokeze hadharani kudhihirisha yupo na wenzake ama yuko peke yake ndani ya Chama.