Shirika la Ndege la Tanzania anzisheni safari za Madagascar na Shelisheli moja kwa moja; naona fursa ya utalii kubwa

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Mashirika ya ndege yanayopeleka ndege kwenye visiwa maarifu Afrika ni machache sana. Nimejaribu leo kutafuta ndege ya Kwenye Madagascar au shelisheli kuwatembelea baadhi ya wafanya biashara wanaokula raha huko nimekosea hadi niende Dubai au Ethiopia au Kenya.

Ikabidi nisome fursa zilizopo kwenye hivi visiwa; nilichogundua mnyororo wa utalii kati ya Arusha, Zanzibar na hivi visiwa ni mkubwa kuliko hata kupeleka ndege India.

Niwaombe wenye shirika letu waanzishe ndege ya moja kwa moja kutoka Tanzania kwenda Madagascar na Sheli sheli waone kama kipindi cha utalii ndege zitakosa siti.

Hivi visiwa vina uchumi mkubwa wa utalii. Tanzania tuna utalii mkubwa; tuwafanye watalii waunganishe likizo zao kati ya Tanzania na utalii wa visiwa hivi tuone faida yake, nimeiona kama hizi ni fursa muhimu sana kwa mtu mwenye akili ya biashara.

Nikifakiwa kuingia huko ntaweka hapa more opportunities hasa za biashara watanzania wachangamkie.
 
Utalii wa shelisheli ni ufukwe tu ambao na sisi tunao sioni uwezekano wa mtalii kwenda shelisheli halafu aje Tanzania ni bora awe Tanzania/Zanzibar afurahie utalii wa fukwe na wanyama kwa pamoja- sehemu moja itakayomletea nafuu.

Shelisheli na Madagasca ni competitor wetu na hatuwezi kuji complement labda kwa uchumi wa mazao ya kilimo, ufugaji tunaweza kuuza hususani kwa route ya mizigo.
 
Haudhani mtalii akimaliza huko anaweza kuja huku kutembelea mbuga za wanyama, au akaanza huku kisha akaenda huko. Mata nyingi watalii hutembelea nchi zaidi ya moja kwa safari moja.
 
Back
Top Bottom