Natakiwa kuwa na nini endapo nahitaji kusafiri kwa ndege kwa safari za ndani ya Tanzania?

Kinumbo

JF-Expert Member
Dec 8, 2019
2,742
4,931
Moja kwa moja kwenye dhumuni la uzi wangu, wakuu nauliza kuhusu utaratibu wa kusafiri kwa usafiri wa ndege kwa safari za ndani ya Tanzania sio kutoka nje ya nchi.

Mimi binafsi sijawahi kutumia usafiri huo sasa niliona mwishoni mwa mwezi huu niende mapumziko huko kijijini kwetu nikaenjoy na kina bibi na babu. Na nikaona kwa awamu hii nitumie usafiri wa ndege.

Naomba mnipe muongozo napaswa kuwa na nini hasa, au ni kama usafiri wa basi tu? Yaani naenda kwa wakala nakata tiketi kisha nasubiri siku ya safari naenda kupanda ndege kisha tunaondoka, sijui chochote wakuu naomba mnieleweshe.

Labda kuna documents unapaswa kuwa nazo, maana kwa safari za nje nasikia uwe na pasipoti sijui visa sasa kwa safari za humu humu Tanzania utaratibu ukoje? Yaani kutoka mkoa fulani kwenda mkoa fulani utaratibu ni upi tafadhali.

Niko hapa nasubiri muongozo, asanteni.
===
Vitu vya kuzingatia wakati wa safari za ndani za ndege soma Natakiwa kuwa na nini endapo nahitaji kusafiri kwa ndege kwa safari za ndani ya Tanzania?
 
Moja kwa moja kwenye dhumuni la uzi wangu, wakuu nauliza kuhusu utaratibu wa kusafiri kwa usafiri wa ndege kwa safari za ndani ya Tanzania sio kutoka nje ya nchi.

Mimi binafsi sijawahi kutumia usafiri huo sasa niliona mwishoni mwa mwezi huu niende mapumziko huko kijijini kwetu nikaenjoy na kina bibi na babu. Na nikaona kwa awamu hii nitumie usafiri wa ndege.

Naomba mnipe muongozo napaswa kuwa na nini hasa, au ni kama usafiri wa basi tu? Yaani naenda kwa wakala nakata tiketi kisha nasubiri siku ya safari naenda kupanda ndege kisha tunaondoka, sijui chochote wakuu naomba mnieleweshe.

Labda kuna documents unapaswa kuwa nazo, maana kwa safari za nje nasikia uwe na pasipoti sijui visa sasa kwa safari za humu humu Tanzania utaratibu ukoje? Yaani kutoka mkoa fulani kwenda mkoa fulani utaratibu ni upi tafadhali.

Niko hapa nasubiri muongozo, asanteni.
Uwe na ticket ya ndege ya huko unakokwenda na kitambulisho chako. Uwahi airport at least saa 1 na nusu kabla ya ndege kuondoka.
 
Mkuu fanya hivi.
1. Kata ticket yako
2. Jiandae kwa safari. Usibebe vitu vilipuzi kama viberiti, perfume, vimiminika.
3. Wanaokwambia uwahi masaa 2 au 3 ni waongo, hiyo ni safari za nje. Safari za ndani minimu time pale ni dk 40 kabla ya safari kuanza. Jitahidi angalua dk 60 uwe pale. Yaani kama ndege inaondoka saa 8 fika saa 7.
4. Usibebe begi kubwa sana. Mzigo wa kilo 20 kushuka chini unabeba bure ukizidi utalipia kila kilo iliyoongezeka....bei tazama huko kwenye ticket yako.
5. Kibegi kidogo cha kuweka kwenye carriers unaweza kuwa nacho pia. Hiki hulipii pia.
6. Beba kitambulisho chochote kile chenye picha yako. Hata cha kazini kwako kinatosha.
7. Kama hupendi usumbufu usivae viatu wala suruali yenye mkanda. Vaa sandals na pensi/track au simple nyepesi nyepesi.
8. Sali Mungu akujaalie safari njema.
9. Kuwa makini kwenye waiting room pale. Ishike flight namba yako. Ukisikia "Flight namba ZX215 Air Tanzania (or whichever unasafiri nayo) kutoka Dar kwenda Bukoba saa 8:00 mchana abiria elekea kwenye ndege" Uende huku umeshika ticket yako mkononi.
9. Ya kwenye ndege utaambiwa huko huko ndani.
Asante.
 
Chief umemaliza kila kitu na uzi ufungwe tu.
 
Shukrani sana ubarikiwe

Perfect!!!
 
Moja kwa moja kwenye dhumuni la uzi wangu, wakuu nauliza kuhusu utaratibu wa kusafiri kwa usafiri wa ndege kwa safari za ndani ya Tanzania sio kutoka nje ya nchi.

Mimi binafsi sijawahi kutumia usafiri huo sasa niliona mwishoni mwa mwezi huu niende mapumziko huko kijijini kwetu nikaenjoy na kina bibi na babu. Na nikaona kwa awamu hii nitumie usafiri wa ndege.

Naomba mnipe muongozo napaswa kuwa na nini hasa, au ni kama usafiri wa basi tu? Yaani naenda kwa wakala nakata tiketi kisha nasubiri siku ya safari naenda kupanda ndege kisha tunaondoka, sijui chochote wakuu naomba mnieleweshe.

Labda kuna documents unapaswa kuwa nazo, maana kwa safari za nje nasikia uwe na pasipoti sijui visa sasa kwa safari za humu humu Tanzania utaratibu ukoje? Yaani kutoka mkoa fulani kwenda mkoa fulani utaratibu ni upi tafadhali.

Niko hapa nasubiri muongozo, asanteni.
Hongera kwa hatua hiyo. Ni maendeleo.

Majibu yameshatolewa comment namba 2, 8 na 9.

Fanya kama walivyokuelekeza.

Umeshakata tiketi? Unaweza ukapata kaunafuu endapo utakata tiketi mapema. Bei hubadilika kadiri muda unavyosonga mbele.
 
Muhimu ni hela ya kununua tiketi, shati safi na suruali nzima nzima, viatu nadhifu, ukiwa na kakoti ka kutupia juu ni swaga nzuri.

Tiketi unaweza kata online au kwa ajenti tu. Siku ya safari nenda zako Airport ukifika uliza terminal 2 kisha nyooka lile lango la kuingilia abiria pale opposite na yale maduka duka. Jamaa watakagua tiketi yako ila wataomba kitambulisho ili walinganishe majina na ya kwenye tiketi. Wakiridhika unazama ndani mzee

Ukifika ndani baada ya kupita kwenye maskana yale nyooka kwenye dirisha la ukaguzi wa tiketi, angalia juu ya dirisha kuhakikisha ni shirika hilo ulilokatia tiketi, hao warembo wakikupokea hapo dirishani watakuelekeza kila kitu. Wakikagua tiketi wanakupa bodingi pass. Wakishakupa hii mzee the rest is history........ushakula mwewe jua
 
Back
Top Bottom