Sherehe ya Mwaka Mpya ni ya Kikristo, Waislamu tumeivamia tu bila kujua

Wewe usiwe na itikadi za siasa kali na kishabiki, kwani huyo papa akifanya jambo zuri tusimsifie kwakuwa yeye sio Muisilamu??!, Papa akisema uzinzi ni haramu nikatae kwakuwa yeye sio mtu wa dini yangu??, halikadhalika papa akigundua jambo lenye faida kwa binadamu kama hiyo kalenda tumbeze kwakuwa yeye sio muisilamu??, Sisi Waisilamu hatupo hivyo labda nyinyi msiokuwa na mafundisho ya hulka njema na uadilifu ndio mnaweza kupinga jambo jema kwakuwa tu jambo hilo kafanya au kalianzisha mtu msiyempenda au kutoka dini nyingine (mfumo kristo).

Mtume wetu mtukufu alipata kusema; Jambo lolote jema mkiliona ni mali (Hazina) iliyopotea ya muislamu, hiyo kalenda inayo manufaa kwetu sasa Kwanini tuibeze kwakuwa aliyeianzisha ni papa??, tena kiongozi mkuu wa kidinii duniani !!, acha akili za kitoto.
Acha kuandika magazeti, JIBU NILICHOKUULIZA.

Nimekuuliza, Unamshukuru Alah kwa Mwaka uliopita huu wa Kanisa ulioanzishwa na Papa wa Kanisa Katoliki?

JIBU HILO SWALI KAMA NILIVYOKUULIZA.
 
Hawakutumia ndiyo maana siyo msingi msingi ni kusherehekea.
Sasa kama hawakutumia kwa nini wewe unatumia?

Msingi wa hoja yako ni kwamba huwezi kusherehekea kwa sababu mitume na manabii hawakusherehekea.... Yaani wewe hufanyi kitu kama mitume hawakufanya.

Sasa swali langu ni hili... Kama mitume hawakuutumia huu mwaka wa Kikristo, kwa nini wewe Unautumia?
 
Sasa kama hawakutumia kwa nini wewe unatumia?

Msingi wa hoja yako ni kwamba huwezi kusherehekea kwa sababu mitume na manabii hawakusherehekea.... Yaani wewe hufanyi kitu kama mitume hawakufanya.

Sasa swali langu ni hili... Kama mitume hawakuutumia huu mwaka wa Kikristo, kwa nini wewe Unautumia?
Kwanza kipindi Cha mitume na manabii hapakuwa na Ukristo hili kwanza weka akilini.

Pili, nikeshakueleza vizuri huko juu nashangaa unarudia swali ambalo nimeshakujibu. Hili tatizo lako Sasa, sa vizuri nilichokiandika.
 
Ukitoka hili hayo mengine yote ni dharura.
Kupanda Gari kunakuwaje dharura? Acha kuchekesha watu.

1. Waislam wanamiliki mabus ya biashara.
Kwa nini hakuna mabus ya wanaume na ya wanawake?

2. Waislam wenye magari private, kwa nini huwa wanajichanganya jinsia zote huko kwenye hayo magari yao?
 
Kupanda Gari kunakuwaje dharura? Acha kuchekesha watu.

1. Waislam wanamiliki mabus ya biashara.
Kwa nini hakuna mabus ya wanaume na ya wanawake?

2. Waislam wenye magari private, kwa nini huwa wanajichanganya jinsia zote huko kwenye hayo magari yao?
Unajua maana ya dharura ? Serikali.inatoa muongozo gani kuhusu usafiri wa imma ? Sasa usiwe mjinga kiasi usihoji mambo kwa ujinga Bali uliza ujibiwe.
 
Hii kalenda tunayotumia,Gregorian Calendar ilikuja baada ya Julian Calendar, zote zina uhusiano na Issa ndio maana utakuta maneno kama AD au BC yote yanamrefer Nabii Issa.

Sasa sisi Waislam imekuwaje hatulijui hili au kufuata mkumbo? au ndio dunia inaongozwa na mfumo Kristo?
Before Christ Ni inamuhusu vp nabii issa sijui Ni Nani kwanza huyo issa
 
Daladala ni dharura?
Nyie jamaa ni comedy sana.

Migahawani huwa mnakaa jinsia tofauti?
Sokoni mnakaa jinsia tofauti?
Vyuoni/shuleni huwa mnakaa jinsia tofauti?
Kwenye ndege huwa mnakaa jinsia tofauti?
Wanaoenda Zanzibar huwa wanakaa jinsia tofauti?
Uwanja wa taifa huwa mnakaa jinsia tofauti?



Hebu punguza ujuaji kidogo.
Bora betting kuliko uislam
 
Unajua maana ya dharura ? Serikali.inatoa muongozo gani kuhusu usafiri wa imma ? Sasa usiwe mjinga kiasi usihoji mambo kwa ujinga Bali uliza ujibiwe.
1. Kwa hiyo Serikali imetoa mwongozo kuwa Wanawake na Wanaume wachanganyike kwenye usafiri wa umma? Huo muongozo uko wapi?

2. Serikali inakataza mtu kwenye gari lake binafsi kutenganisha jinsia kati ya Me na Ke?
Serikali imetoa muongozo kuhusu hili?

Haya maswali yangu yajibiwe vizuri.
 
Watu ambao wamefilisika akili za maisha ndio huja na hizi hoja ili wapate uhalali katika jamii wanayoishi waonekane nao wana malengo au shughuli fulani.

Sasa nikikuuliza hapo unachokitafuta ni nini unaweza kunambia?!

So hiyo kalenda inakuzuia nini kufanya maisha yako au inakubugudhi nini hadi ushindwe kuishi kama wanadamu wengine?!

Ni dhahiri kichwa chako kimejazwa na hofu ya maisha na pengine kuna mambo hayakuendei sawa sasa unajaribu kutafuta sehemu ya kutolea hasira zako za maisha.

Sikiliza Dogo (nakuita dogo kwa makusudi iwe una umri mdogo au upo na miaka 50 wewe bado unaonekana haujakua kiakili kuongea vitu kama hivi), kwenye haya maisha usipokuwa na mfumo na mipangilio mizuri ya kuishi utabakia kuwa kama mwendawazimu.

Tuliza kichwa chako, tafakari njia zako, elewa vema mafunzo ya imani yako, tafuta pesa kwa uhalali, heshimu watu wengine ikiwamo imani kama vile wao ambavyo wanakuheshimu kisha uishi kwa utulivu sio ukorofi.

Achana na huo ujinga ujinga wa kalenda. Ingekuwa ni tatizo basi maisha yasingeenda kama vile unavyoyaona leo hii.
Hapa umemaliza mkuu.

Sent from my Infinix X624B using JamiiForums mobile app
 
Acha kuandika magazeti, JIBU NILICHOKUULIZA.

Nimekuuliza, Unamshukuru Alah kwa Mwaka uliopita huu wa Kanisa ulioanzishwa na Papa wa Kanisa Katoliki?

JIBU HILO SWALI KAMA NILIVYOKUULIZA.


Wewe upo sawa kichwani??-- Unadhani mimi ni mshirikina kama wewe??---soma vizuri hapa; NAMSHUKURU ALLAH KWA "NEEMA" ALIZONIJALIA KATIKA MWAKA ULIOPITA HUO HUO WA KALENDA YA GREGORIAN, mimi huwa si mshukuru Allah kwa ajili ya kuingia mwaka mpya wa Gregorian nk bali namshukuru Allah kwa neema zake na baraka alizonijalia katika mwaka uliopita huo wa Gregorian na hilo sio dhambi katika dini yetu.

Usipoelewa hapo utakuwa na lako jambo.

Mfano leo akija papa na akatoa pesa ya kujengea msikiti tuache kuchukua kwakuwa yeye sio Muisilamu?? au kama tukichukua na kujenga msikiti tuache kumshukuru??!,

Acha fikra za kifanatism katika dini.
 
Back
Top Bottom