Jmushi1, nimeandika haya baada ya kuwasoma wachangiaji walokuwa wakitukana matusi mazito na kutangaza vita. Sikuanzisha mimi hoja au mada hii. Kosa langu ni kuuliza Sheikh Ponda amefanya kosa gani? watu wanataka niamini kwamba anahusika na mauaji ya Mbagala jambo ambalo halikuwepo hapa kijiweni isipokuwa maswala ya Redio Iman.
Nachojua mimi hii ni redio ya mtu ambaye kaisajili kwa kutumia jumuiya wa Waislaam huko Mrogoro. Hawa huenda na kurecord watu mbali mbali nchini ikiwa ni pamoja na huy Sheikh Ponda ktk propaganda zao za Kidini ambazo wananchi wameikemea serikali kwa muda mrefu lakini hadi leo ina operate..
Ponda sii mwanahisa wala mmiliki wa hiyo redio isipokuwa hawa jamaa hurekodi speach zake ambazo kusema kweli binafsi yangu sijazisikia isipokuwa moja inayohusu kuipinga serikali ktk swala la sensa, maswala ya MoU na hata NECTA ambayo kwa madai yake inatakiwa seirkali iyafanyie uchunguzi..I would..Kama mnayo hotuba yoyote ya Ponda inayoukashifu Ukristu ningeomba sana mniwekee ili nami nimjue huyu Sheikh ni mtu wa aina gani lakini anapotetea maslahi ya waislaam sioni tatizo ndio kazi yake aloapa kuifanya kama navyowasikia Mbowe, Dr.Slaa kuwatetea wananchi na Chadema, Wenyeviti wa Union iwe madaktari, walimu, watumishi wa serikali au Jumuiya ya Wanawake na watoto nchini wakilalamikia serikali. Hawa wote kama hukubaliani nao utawaona wanasababisha vurugu nchini..
Nitasema tena Wadanganyika mnapenda sana kuuchonga na kutangaza vita lakini hamuwezi vita na wala sii jambo la kuombea. Diplomacy inawezekana na tusiwe na jazba tuzungumze vitu kwa kituo tupate kujua kitu gani kinafanyika. Narudia tena kuuliza Ponda amefanya kosa gani? nambie halafu tutaendelea na mjadala..
Unaposema watanganyika hatuwezi vita una maana gani?Hawaviwezi vita dhidi ya nani?Waislam?Ni waislam ndo wenye kuweza vita?Naomba uwe specific hapo.
Kuhusu Ponda,hata wewe unamtetea bila kujuwa kwamba ni mashtaka gani atakayofunguliwa na kuona ushahidi utakaotolewa dhidi yake ndipo ujuwe kama kaonewa ama vipi.
Haya maneno ya wana JF humu haina maana kwamba wanafahamu ushahidi utakaotolewa na waendesha mashtaka,haya ni mambo ya hisia tu,hisia ambazo hata zimesababishwa na ukweli kwamba kuna chuki za kidini zinazosambazwa na vyombo hivyo vya habari,na ndiyo maana chuki inazidi kuenea.
Kama wewe ni muumini wa kusema kuna mfumo kristo,hilo tayari ni kupandikiza chuki.Kumbuka wakati wa sensa,chadema walizuiwa kufanya mkutano na hata ikasababisha kuuwawa kwa Mwangosi,lakini serikali ilifumbia macho waliowakataza waumini wao wasihesabiwe.
Sasa jiulize hapo kuhusu double standard.Nani mwenye kukwamisha zoezi la sensa hapo?mwenye kufanya mkutano ama mwenye kusema wakatae kuhesabiwa?
Narudia tena mkuu pia kwamba msichanganye dini na siasa,kwasababu unatolea mifano ya wanasiasa na kulinganisha na hayo ya Ponda kwa kudai ni haki za waislam,sasa ina maana hao kina Slaa na Mbowe wanapigania haki za "chadema wakristo"?si unaona ulivyokuwa twisted kwenye hiyo hoja?
Kama ni hivyo,basi si waislam muanzishe chama cha kiislam cha kisiasa kama bado hakipo?Kwasababu kamwe usidhani kuwa chama cha kisiasa kikijiingiza kwenye kuitetea imani moja ya dini basi kutakuwepo na usalama nchini mwetu.
Pia kwa kumalizia,sidhani hata kama hatua ya kumkamata Ponda inalengo la kutenda haki yoyote,kwasababu chini ya serikali hii,hilo ni msamiati.Serikali ingekuwa na nia ya kudhibiti uhuni huu,ingefanya hivyo toka kitambo sana.
Badala yake nadhani serikali ndiyo yenye nia mbaya kwenye hili.Subiri tuone mashtaka watakayomfungulia ndo utakuja kuniambia.Hakuna hata siku moja rais huyu tuliyenaye ameonyesha kuupinga udini.Na hili la kukamatwa pengine ni shinikizo flani,siwezi kujuwa limetoka wapi,lakini nina uhakika siyo hatua ambayo inaonyesha honesty ya rais kwenye kushughulikia hizi issue.
Na nilishawahi kuanzisha thread yenye kuelezea udini wa JK,lakini imefungwa kimyakimya,tena wakati watu wakiwa hawaichangii tena.Ukweli ni kwamba udini umeoteshwa,kupaliliwa na kukuzwa na serikali ya JK chini ya amiri jeshi mkuu mwenyewe!Hauhitaji kuwa akili ya astronaut kuona hilo.
Pengine kuna ushahidi ambao ni overwhelming,na ameshindwa kuifumbia issue hii macho.Kama unasema hujawahi kusikiliza hotuba za Ponda,basi usi conclude kwamba hajawahi kuziponda imani za wengine.