Sheikh Ponda akamatwa Dar!

Sabato masalia

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
228
134
Yule 'Mwanaharakati' maarufu wa dini ya kiislamu Sheikh Ponda Issa Ponda amekamatwa na polisi usiku huu akiwa katika msikiti wa Temeke Tungi

UPDATES:
Ni taarifa za kweli na aliwindwa kwa siku tatu ili akamatwe katika mazingira salama yasiyoweza kuibua mtafaruku na huu ni mwanzo, huenda hatua kubwa zaidi zitachukuliwa kwa Redio Imaan.
- Ponda alikamatwa mida ya saa 5 usiku muda ambao unahisiwa kuwa sawa na ambao mwenzake Sheikh Farid wa Uamsho (Zanzibar) anadaiwa kupotea; unaweza kufuatilia - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wa-uamsho-atekwa-nyara-visiwani-zanzibar.html
- Wafuasi wa Ponda wameanza purukushani, unaweza kusoma - https://www.jamiiforums.com/habari-...si-wa-sheikh-ponda-waanzisha-purukushani.html

KAULI YA KAMANDA KOVA:
Kamanda Kova akiongelea sakata la kukamatwa kwa bwana Ponda na maandano ya waislamu waliokuwa wanajaribu kushinikiza bwana Ponda aachiwe huru bila masharti; amesema kuanzia leo watu wote lazima wafuate sheria huku akisisitiza kuhusu jambo hilo amesema 'mambo ya kutofuata sheria, mambo ya kudhani kuna wengine wako juu ya sheria yamepitwa na wakati kuanzia leo'

Amesema bwana Ponda atapewa dhamana na ndugu zake baada ya kufuata utaratibu wa sheria, amesisitiza kwamba kamwe jeshi la polisi halitamuachia eti kwa sababu ya mashinikizo kutoka kwa baadhi ya watu (nafikiri alikua anakumbuka mara ya mwisho walivomuachia bila masharti baada ya kupata shinikizo kutoka kwa waislamu)

Source: Radio One breaking news!

Taarifa ya Wakili wa Sheikh Ponda Issa Ponda, Wakili Juma Nassoro

Asalaam Alaykum!

Saa 4 asubuhi nilifika Central Police kusimamia mahojiano yake na Polisi kwa mujibu wa haki za mtuhumiwa nilionana na msaidizi wa ZCO daada ya utambulisho na kumfahamisha haki zake wakati wa mahojiano alihojiwa. Ukiacha namna alivyokamatwa mpaka naondoka polisi saa 10 kasoro alikuwa ktk hali nzuri na polisi akiwa kituoni hawakumfanyia lolote lililokinyume na haki za mtu aliyechini ya ulinzi.

Sheikh anatuhumiwa na mambo yafuatayo:-

1. Kuhamasisha maandamano kwenda Wizara ya Mambo ya Ndani. Wakati wa mahojiano walitaka kujua yafuatayo:-
i. Kwanini waliandamana
ii. Nani aliandaa mabango
iii. Kwanini walisema kuwa baada ya maandamano yale wataenda kumng'oa Mufti na Ndalichako
iv. Nani aliandaa maandamano

Sheikh alikiri kuhamasisha maandamano na pia alikubali ujumbe uliuokuwa katika mabango ulikuwa umebeba hisia za waislamu. Isipokuwa yeye hajui nani aliyaandika hayo mabango. Kuhusu Mufti na Ndalichako alisema wanastahili kuondolewa kwasababu ya kuongoza kwa dhulma dhidi ya waislamu. Pia alisema maandamano yaliandaliwa na Taasisi na Jumuiya za Kiislamu na yeye ni katibu wake.

2. Kuvamia kiwanja cha chang'ombe

Hapa alijibu kuwa huo ni mgogoro wa ardhi na waislamu wapo pale kwasababu ni kiwanja cha waislamu. Na kama kuna mtu anadai amevamiwa eneo lake huo ni mgogoro wa ardhi aende kushitaki mahakama ya ardhi na waislamu wapo tayari kufika mahakamani kujibu. Pia alikiri kuwa amehusika ktk ujenzi wa msikiti unaojengwa ktk eneo hilo.

3. Kuhamasisha maandamano kidongo chekundu

4. Vurugu Mbagala.

Haya mawili ya mwisho hakuhojiwa kwasababu mafaili yanayohusu malalamiko hayo yalikuwa hayajafika central lakini vilevile muda ulikuwa umeenda sana. Kwani mpaka tunamaliza mahojiano ilikuwa ni saa kumi kasoro hivi toka saa nne asubuhi.


DHAMANA.
Baada ya mahojiano niliomba apatiwe dhamana na kesho afike polisi kwa mahojiano zaidi. Polisi waliokuwa wanamhoji walikataa kwa hoja kuwa suala hilo liko kwa viongozi wakuu wa jeshi la polisi. Waliomba nikamwone ZCO Bw. Msangi, yeye alisema hawezi kulitolea maamuzi akanitaka nimwone Kamanda Kova. Nilienda kuonana na Kamanda Kova naye aliniambia kuwa hawawezi kutoa dhamana mpaka amalize mahojiano yaliyobaki. Na vile vile alisema wanasubiri wapate ushauri toka ofisi ya DPP. Lakini zaidi akasema kwa kuwa issue ya Mbagala kuna watu wameshitakiwa kwa armed robbery kosa ambalo halina dhamana si vizuri kumpa dhamana sasa kwani huenda katika upelelezi wao wanaweza kumuunganisha na washitakiwa wa armed robbery Mbagala. Kwa ufupi hiyo ndio hali iliyokuwepo.


NAOMBA WAISLAMU WAAMBIWE WAWE NA SUBIRA WAKATI HUU WAIFANYE LOLOTE LITAKALOWAPA NAFASI MAADUI WA UISLAMU MANENO YA KUSEMA


Maasalamu!
Juma Nassoro - Wakili
 
Sasa isiwe akamatwe kwa sababu wameamua kumtoa kafara; Ponda hajaanza leo kusema anayoyasema. Kama muda wote (miaka yote) wameweza kumvumilia imekuwaje leo waamke na kusema wanamkamata?

Kama kosa ni yale ya Mbagala au anayoyasema ukweli ni kuwa itakuwa ni kumuonea! Kosa ni la serikali inayotawala. Ukiacha mlango wazi kwenye zizi kila sikuw watu wanakuambia chui ataingia na kula mbuzi nawe ukapuuzia siku chui akiingia na kula utalaumu zizi kwanini halikufungwa?
 
Ni taarifa za kweli na aliwindwa kwa siku tatu ili akamatwe katika mazingira salama yasiyoweza kuibua mtafaruku na huu ni mwanzo, huenda hatua kubwa zaidi zitachukuliwa kwa Redio Imani.

Nini kiliizuia serikali kuchukua hatua kubwa kwa radio Imani siku za nyuma? Bado naamni serikali adilifu ingekwisha shughulikia tatizo na chuki za kidini muda mrefu nyuma.
 
Yote 9 hii habari iwe ni kweli na kama ni kweli wasitufanye watoto wadogo kwa kumwachia bila vigezo vya kueleweka! Anastahili kujibu tuhuma nyingi sana na awajibishwe! Tumechoka na maneno na vitendo vyake vilivyojaa chorus!
 
Mzee Mwanakijiji

Labda ya mbagala ndio yame waamsha huu sio utani tena, na ni watu gani anaowaamsha kwa fikra zake ambazo hazifai.

Let it be true na anyongwe
 
Last edited by a moderator:
Sasa isiwe akamatwe kwa sababu wameamua kumtoa kafara; Ponda hajaanza leo kusema anayoyasema. Kama muda wote (miaka yote) wameweza kumvumilia imekuwaje leo waamke na kusema wanamkamata?

Kama kosa ni yale ya Mbagala au anayoyasema ukweli ni kuwa itakuwa ni kumuonea! Kosa ni la serikali inayotawala. Ukiacha mlango wazi kwenye zizi kila sikuw watu wanakuambia chui ataingia na kula mbuzi nawe ukapuuzia siku chui akiingia na kula utalaumu zizi kwanini halikufungwa?
Hapo sijakupata mwanakijiji. Kwa hiyo kama kwa muda mrefu ulikuwa unaacha mlango wa zizi wazi kwa kuamini kwamba chui hataingia, lakini ikatokea siku moja akaingia hutachukua hatua? Kinachoonekana ni kwamba serikali ilikuwa inampuuza kwa muda mrefu. Sasa imeanza kuona matunda ya kauli za huyu mhuni, na imechukua hatua.

Kama ni kwa mfano wako basi, serikali inachukua hatu za kufunga zizi ili huyu chui asirudi tena. Ninaungana na wale wanaosema polisi wasiishia kwa Ponda tu, bali waende mbali zaidi kwa kuifuta kabisa Radio Iman na gazeti la Al-nuur. Hivi ni virusi vibaya sana kwa mstakabali wa amani yetu. Sioni kibaya kwa serikali kuchukua hatua hiyo.
 
ni kweli wamemkamata maana ni janga kwa taifa letu akati yeye sio mtz...mbona sheikh mkuu hana reasons kama zake...a behave bwana, hatutaki kuwa kama somalia na vita
 
Back
Top Bottom