Sheikh Mkuu Zuberi jenga shule kubwa badala ya misikiti mikubwa

Sasa shule 30 tanzania nzima ndio kitu cha kujisifu!!
Unajua idadi ya shule ambazo taasisi/madhehebu ya kikristo yanazo individually?

Dhehebu moja tu la Walokole TAG lina shule nyingi kuliko Bakwata ambayo ndiyo muwakilishi wa waislam tz nzima.

Hapo sijataja madhehebu makubwa kama RC,KKKT na Anglican.

Acha kujilinganisha na usiofanana nao. Bakwata inashindwa na dhehebu dogo tu la kikristo kwa idadi ya shule. Nyie watu amkeni,
Mkuu BAKWATA imejaa wapigaji.
Kuna msikiti ghorofa moja,ulianza kujengwa mimi nipo primary mpaka leo haujawahi isha, kuna matajiri,wafanyabiashara, wadhamini/ wahisani nk.
Viongozi wa bakwata wamepoteza imani kwa waumini,hivyo mambo yanajiendea hovyo.Bakwata ingekuwa taasisi moja matata kwa sababubu ina rasilimali watu wengi sana karibu 1/4 ya watazania,
Inashindwa nini kuendelea !!
 
Mbona watu hao tunao mkuu? Wako maprofessor waliohifadhi quran pia
 
Idadi ya wiaslamu wako kwenye vyuo vikuu, ofisi za umma na sehemu zote za utumishi ni ndogo sana kulinganisha na watu wa dini nyingine.

Bila shaka pamoja na mambo mengine ya kihistoria, imani, ukabila, ukanda na kiuchumi lakini idadi ndogo ya watoto wa kiislamu kwenye vyuo vikuu ukilinganisha na watoto wa dini nyingine inaweza kuwa sababu ya msingi ya shida hii

Badala ya kuwaza kujengewa misikiti mingi na mikubwa weka jitihada zako kwenye kujenga shule na vyuo vingi ambako watoto wengi wa kiislam watapata ilmu dunia pia. Elimu hii ndiyo inayotoa wahandisi, madaktari, wauguzi, walimu, marais, mawaziri, wakurugenzi na watumishi wengine.

Fanya sensa ya watumishi kwenye kila wizara, ofisi, shule Na vyuo vya umma Na binafsi ujionee hali ilivyo. Pitapita huko uone idadi ya walimu wa vyuo vikuu huko.

Mazoezi ya kuhifadhi Qur'an yaende sambamba na mazoezi ya kuhifadhi hisabati Na fizikia kwenye madrasa zao.

Kama viongozi wa ofisi mbalimbali wengi ni wa dini fulani bila shaka watumishi wanaotegemea maoni yao kwenye kuajiliwa na kuteuliwa kwenye nafasi mbalimbali bila shaka watakuwa kama wa dini za wanaowateua. Like dissolve like.
Kujenga msikiti na madrasa zitazosomesha Qur'aan na Sunnah ni bora mara elfu kuliko kujenga shule.
 
Utawapata wapi mkuu? Yaani mtu awe na PHD au masters halafu pia awe kasoma na elimu ya kitabu itakayo mpa sifa ya kua sheikh??? Haiwezekani, tusitengeneze sheria ambazo practically haziwezekani mkuu
Watu hawa wapo wengi. Sema elimu ya dini huwa inachukua muda mrefu sana kujifunza kuliko elimu hii ya mazingira.
 
Utawapata wapi mkuu? Yaani mtu awe na PHD au masters halafu pia awe kasoma na elimu ya kitabu itakayo mpa sifa ya kua sheikh??? Haiwezekani, tusitengeneze sheria ambazo practically haziwezekani mkuu
Kwa hio hao waislamu wenye phd wote hawajasoma dini unaweza kunihakikishia hilo?
Mi mwenyewe ninadigrii na nimesoma dini, tena sijakulia ujiji, au Tanga, au Bagamoyo, vipi wale waliokulia huko ambapo ni lazima usome dini au waliosoma islamic school.
Shule za kislamu hazifundishi somo la dini ?
Mkuu unaongea kama darasa la 7 hivi, nakushangaa ujue. Umesoma wapi mkuu ?
 
Unatumika. Hayo mawazo yako ni ya kishetani. Msikiti ni jambo la kheri na kupata thawabu kusaidia waja wa Mnyaazi Mungu wewe unakuja kupinga?shule zipo ngapi hapa nchini? Wewe ni Kafir. Na unatumika na shetani. Shule hizi ndo zinapunguza idadi ya waumini misikitini. Unaumia na nini kuona msikiti mkubwa ukijengwa?mbona yapo makanisa makubwa?

Na wala wewe si msemaji wa waislamu acha kuingilia mambo yasiyokuhusu. Umenichefua sana. Kwa nini usi deal na mambo yako pekee?
 
Siku nyingine usikubali ujinga ukuendeshe hovyo namna hivyo ,na hakuna mabikira 72 walio ahidiwa
Thibitisha hili kama hakuja ahadi hiyo.

Huwa unatumia nini kupima mambo ? Kama unatumia akili pekee unakosea sababu akili ina ukomo kama yalivyo macho yana ukomo wa kuona.
 
Watu hawa wapo wengi. Sema elimu ya dini huwa inachukua muda mrefu sana kujifunza kuliko elimu hii ya mazingira.
Elimu ya dini inaendeshwa kizamani ndio maana inachukua muda mrefu.
Hakuna mtaala, ukimaliza juzuu hii unahamia ngingine.
Unakariri tu!!
Elimu ya kiislamu ya sekondari ndio kidogo imepangwa kwa sababu inasimamiwa na wizara ya elimu na mitihani hutolewa na wizara ila madrasa kila ustadhi anajiamulia yeye.
Akiondoka akaja mwingine anaaza na yake.
Maustadhi hawana vyeti vya kuwatambulisha. Mwingine ni kanjanja anataka mishahara tu.
Elimu yetu ya dini inatakiwa tukae tuiundie dira.
 
Una elimu yoyote ya dini hata zile halaaq za misikitini ? Maana naona unaandika ujinga na uongo,mpaka nimeamua tuanze mwanzo kabisa.

Elimu ya dini ni tofauti na elimu ya secular,kila unacho soma katika dini lazima ukifanyie kazi,ndiyo maana kuna taratibu walimu katika vituo vya usomeshaji dini unao enda ngazi kwa kazi. Achilia mbali hizi madrasa,ambazo zipo zina mitaala kuna hizi marakizi na darasa duara katika misikiti.

Ni ujinga kuilinganisha elimu ya dini na secular,labda uwe huzijui elimu hizi mbili,elimu ya secular ina mitaala ila mitaala hovyo kwayo inakuwekea mambo mengi ya uongo na yasiyo fanya kazi katika uhalisia.

Kosa kubwa kuikosea adabu elimu ya dini. Lingine chukua hili,siku zote mitaala huwa haikidhi haja,labda uwe mgeni katika masuala ya kielimu. Leo hii katika hiyo "sucular" unayo ipigia chapuo,shahada ya miaka minne unaweza kuisoma katika miaka miwili au mitatu,lakini wameshikilia ukiritimba na uoga unawafanya wawe vichwa mchunga.

Elimu si vyeti bali elimu ni kile ulicho nacho,unaonekana wewe si mdau wa elimu. Leo kupitia vyeti zimetokea ghishi ambazo hazihesabiki kwa wingi wake. Wangapi hawakusoma kwenye mavyuo yanayo toa vyeti katika elimu ya secular lakini mpaka kesho nadharia zao mnasomeshwa ?

Wenye kujua thamani ya elimu na maana ya elimu,tembelea vyuo vya dini hasa kile cha "Madina University" wamepita walimu pale hawana vyeti ila walikuwa wanajua vitu,wakapewa nafasi na kusomesha hao wanao pewa mavyeti ya stashahada,shahada,uzamili na uzamivu.

Wangapi wana vyeti ila hawana kitu katika kile walichosomea ? Sasa elimu haiko hivyo.
 
Mskiti ndio uliosimamisha uislamu. Siku waislamu wakiimarisha misikiti badala ya kutumika kwa ibada ya swala pekee, na kurudi katika asili yake basi uislamu utasimama tena. Mtoa mada hata hujui kazi za msikiti kama walivyo waislamu wengi.
 
Jadili utolewaji wa elimu kwa jamii yote na si waislamu tu. Wamasai na waislamu wepi wamenyimwa elimu zaidi?
Tanzania elimu yetu kwa ujimla ipo nyuma, si wakiristu si waislamu si wapagani.
Mimi kama mtaalamu wa elumu nashauri ujadili elimu bora kwa kila mtanzania, suala la vikundi vikundi halina mantiki. Shule za serikali zipo kwa ajili ya kila mtu.
Bakwata walirithishwa na warabu kujenga msikiti na si shule.
Bakwata inaendeshwa na mashehe, unategemea watajenga shule ?
Bakwata wameshindwa kuzisimamia shule zilizopo , je wataweza kujenga zingine ?
Mind set ya waislamu inatakiwa ibadirike, waige warabu wa Dubai, wamefanya mapinduzi ya kifikra na kuachana na fikra za jadi ya kiislamu.
Waige wa Iran wametoka kwenye dhana ya kusubili akhera na kuijenga mifumo ya dunia ya kisasa.
Ukienda msikitini ni mawaidha ya hadithi za mtume tu, hakuna kujadili changamoto za kielimu,sayansi na teknolojia, hii ni kwa sababu uelewa wa mashekh ni hadith za mtume tu, habali za Globalization haziwahusu,uwekezaji hauwahusu.
Kila ijumaa unazikiliza hadithi ile ile mpaka unazeeka.Unatalajia jipya mkuu,.
samahani kama nimekukwaza ila uwongo kwangu mwiko.
Haujanikwaza mkuu nafurah Sana napoona mtu anasimamakwa ajil ya watu wake wapate elimu bila kijar dini au itikidi

Lengo langu lilikuwa wazid kuongeza shule ili watu wote wapate fursa hi adhmu ya elimu wasiishie shule 30 ambazo mdau hapo juu anaona wamefanikiwa
 
Una elimu yoyote ya dini hata zile halaaq za misikitini ? Maana naona unaandika ujinga na uongo,mpaka nimeamua tuanze mwanzo kabisa.

Elimu ya dini ni tofauti na elimu ya secular,kila unacho soma katika dini lazima ukifanyie kazi,ndiyo maana kuna taratibu walimu katika vituo vya usomeshaji dini unao enda ngazi kwa kazi. Achilia mbali hizi madrasa,ambazo zipo zina mitaala kuna hizi marakizi na darasa duara katika misikiti.

Ni ujinga kuilinganisha elimu ya dini na secular,labda uwe huzijui elimu hizi mbili,elimu ya secular ina mitaala ila mitaala hovyo kwayo inakuwekea mambo mengi ya uongo na yasiyo fanya kazi katika uhalisia.

Kosa kubwa kuikosea adabu elimu ya dini. Lingine chukua hili,siku zote mitaala huwa haikidhi haja,labda uwe mgeni katika masuala ya kielimu. Leo hii katika hiyo "sucular" unayo ipigia chapuo,shahada ya miaka minne unaweza kuisoma katika miaka miwili au mitatu,lakini wameshikilia ukiritimba na uoga unawafanya wawe vichwa mchunga.

Elimu si vyeti bali elimu ni kile ulicho nacho,unaonekana wewe si mdau wa elimu. Leo kupitia vyeti zimetokea ghishi ambazo hazihesabiki kwa wingi wake. Wangapi hawakusoma kwenye mavyuo yanayo toa vyeti katika elimu ya secular lakini mpaka kesho nadharia zao mnasomeshwa ?

Wenye kujua thamani ya elimu na maana ya elimu,tembelea vyuo vya dini hasa kile cha "Madina University" wamepita walimu pale hawana vyeti ila walikuwa wanajua vitu,wakapewa nafasi na kusomesha hao wanao pewa mavyeti ya stashahada,shahada,uzamili na uzamivu.

Wangapi wana vyeti ila hawana kitu katika kile walichosomea ? Sasa elimu haiko hivyo.
Hakuna mdau wa elimu yoyote anaejua maana ya elimi akabeza vyeti.Dunia nzima elimu ni vyeti kasoro madrasa.
Yani unamzoa mtu afundishe hujui level yake ya elimu ,kisa kapitia madrasa, ni kupitwa na wakati.
madrasa zinatakiwa ziundiwe mtaala, ukubali ukatae.
kusoma soma tu bila direction, kukariri, juzuu, kutafsiri quran kila madrasa inafundisha kivyake.
Mambo yanayofundishwaa madrasa hayatafanyiwi kazi yoyote zaidi ya mawaidha na kusali, yena ukiwa mdau msikitini
Sura mbili tatu zinatosha sana kusali.
Ukisoma juzuu 30 unazitumia wapi?
Watu kama nyie ndio mnaifanya BAKWATA isiaminike kwa chochote.
Warabu walitudanganya sana bado kuna watu wanadumisha fikra za kiarabu. Mataifa ya kiarabu ni mataifa yaliofeli vibaya sana katika karne ya 21 kisa kupingana na fikra mpya.
Hivi sio ujinga kuendelea kujenga misikiti huku misikiti iliopo haijai watu kisa umekaririshwa.
Naona unatoa mifano isio endana kabisa na hoja. Kusoma mawazo ya wasio enda shule wala si hoja ya kutokwenda shule au kutokuwa na vyeti.
unaweza kukubali kufanyiwa operation na daktari aliejifunza huko mitaani au unazungumza tu kujifurahisha?
Madrasa zibadili mfumo, vinginevyo kelele za kutengwa hazitakuja kuisha.
Unamfundisha mtu qurani na suna humpi ujuzi wowote katika karne ya 21, unaamini kudra wakati wenzio wanautafuta ujuzi, wakijitegemea wewe unaanza kulalama.
Mfumo wa elimu ya kiislamu umefeli vibaya sana, watu tuna ndugu wamekariri hizo elimu na hawana mbele wala nyuma.
Madrasa zinawapotezea watu mda hakuna zaidi. Ipi siku waislamu wengi watagundua kuwa walipotezewa mda tu.
 
Sasa shule 30 tanzania nzima ndio kitu cha kujisifu!!
Unajua idadi ya shule ambazo taasisi/madhehebu ya kikristo yanazo individually?

Dhehebu moja tu la Walokole TAG lina shule nyingi kuliko Bakwata ambayo ndiyo muwakilishi wa waislam tz nzima.

Hapo sijataja madhehebu makubwa kama RC,KKKT na Anglican.

Acha kujilinganisha na usiofanana nao. Bakwata inashindwa na dhehebu dogo tu la kikristo kwa idadi ya shule. Nyie watu amkeni,
Kumbuka BAKWATA ni Baraza kuu la Waislamu Tanzania,zipo Taasisi nyingi za kiislamu,zina shule, vyuo.Na Taasisi hizo ziko Tanzania nzima.Zipo zinazomiliki zaidi ya shule tatu,na zaidi ndani ya mkoa mmoja.
Uislamu uko tofauti na ukristo,kuwa ukristo umegawanyika,na kutofautiana mambo mengi katika ibada,lakini katika uislamu nyingi ya taasisi katika ibada ziko sawa.,ndio ikawa wengi wasio kuwa waislamu,wanashindwa kutofautisha baina ya BAKWATA na Taasisi za kiislam,na kujuwa kuwa BAKWATA ni kiongozi katika uislamu,Tanzania,katika uislamu ziko tasisi nyingi,lakini hazitofautiani katika ibada,ndio ukaona katika kuomba dua,za kitaifa,anakuja Sheikh mmoja tu,kuwakilisha Taasisi zote za kiislamu,Swala zinasaliwa bila utofauti,siku ya ijumaa,waislamu wote wanaswali ijumaa,hakuna wanaoswali jumamosi au jumapili kama wakristo walivogawanyika,waislamu wote wanakwenda Hija mji mmoja wa Maka,kwenye Qur'an wote wanafuata Qur'an hiyo hiyo,hawana utofauti,kama katika ukristo kila dhehebu lina Biblia yake.
Kwa hiyo jua,ziko Taasisi nyingi za kiislamu Zina shule zao pia,mbali na BAKWATWA.
Kuna Taasisi kama Istiqama,ina shule zake Tanzania nzima,kuna Islamic Foundation,Wana shule zao ,kuna African Muslim Agency(direct aid),Wana shule zao,kuna Maawah Islamia,kuna Answar muslim,Wana shule zao,kuna Jumuia ya kuhifadhisha Qur'an,Wana shule zao,kuna Ilala Islamic,wana shule zao,Nk ni Taasisi nyingi,hapo hatujagusa madhehebu mengine,kama Shia,Bohora,Aghakhan,Suni Jamaat nk
 
Sio waisilamu tu, Hata wakiristo.
Wako busy kujenga makanisa, vishule vya watoto wao vipo hovyo.
Waislamu na wakiristo wote waamke akili, waache tabia ya mkoloni ya kuwadumaza akili misikitini na makanisani.
Watu wote tuboreshe shule zinazotuzunguka, kwa kweli ni kama magofu, hizo saint ni chache tu na wala sio tegemeo ka jamii kubwa bali wachache tu.
Wachungaji ba mashehe hawzhawahi kuitisha harembee ta shple zinaziwazunguka bal kuongeza majengo.
Tanzania haina uhaba wa misikiti na makanisa ila shule, hospitali na vifaa vyake.
Sio kweli. Wakristo wana shule nyingi sana. Hakuna dhehebu kubwa halina shule za awali, secondary na chuo kikuu. Tena za kutosha
 
Sio kweli. Wakristo wana shule nyingi sana. Hakuna dhehebu kubwa halina shule za awali, secondary na chuo kikuu. Tena za kutosha
Taasisi za kiislamu,ziko nyingi,na karibia zote zinamiliki shule,na vyuo tofauti na BAKWATWA shule na vyuo vinavyomilikiwa na BAKWATA,mnashinda kutofautisha kwa vile katika uislamu tofauti na ukristo,madhehebu makubwa Tanzania Suni,ambao ni sawa na BAKWATA katika ibada,ila BAKWATA,ni BARAZA KUU.
 
Back
Top Bottom