Je, PhD hewa zipewe kipaumbele kwenye nafasi za uongozi na siasa?

musabuze

Member
May 25, 2018
30
25
vasily-koloda-8CqDvPuo_kI-unsplash.jpg

Miaka ya hivi karibuni Tanzania imekuwa na ongezeko la watumishi wengi wa umma ambao wanaongeza elimu ili kujiweka katika nafasi nzuri za kuwa viongozi katika ngazi mbalimbali za serikali. Asilimia kubwa wakiwa ni watumishi wanaowania Masters na asilimia iliyobaki ni PhD.

Hii imepelekea mfumo wa elimu vyuoni kuingia dosari kwa wanafunzi wanaotarajia kufundishwa na walimu wenye historia nzuri kimasomo(Educational Background) na Uzoefu na weledi katika kazi.

Tafiti zinaonesha kutokana na ongezeko la watu tunaoamini kuwa wameelimika kutumia nafasi zao kimkakati ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kupata vyeo katika ofisi za umma imepelekea vyuo vikuu kujaa walimu wanaowaza madaraka na kupoteza umakini kwenye majukumu yao ya kufundisha na kusimamia malezi ya kitaaluma kwa wanafunzi.

Inasikitisha kuona Mwalimu mwenye ambaye hajasoma Form 4 na Form 6 ana Phd ila hana uwezo wa kufundisha ilihali wapo walimu wenye Masters au Degree wenye uwezo mkubwa wa kufundisha.

Serikalin ikiendelea kuruhusu wasomi wajinga wawafundishe vijana tutaendelea kulaumu vijana hawajitumi

Vyuo vikuu ni mahali pa kujifunza mambo mengi ila kwa sasa ni sehemu ya baadhi ya watumishi wa umma au waalimu kujishikiza wakingoja vyeo vya juu katika serikali

Je Phd zikipewa kipaumbele kwenye ngazi za uongozi katika taasisi za kiserikali nani atawafundisha vijana vyuoni?
 
Back
Top Bottom