Share nasi matukio yako ya ukuaji

Ilikuwa mkesha wa mwaka mpya nipo na kaka yangu mtoto wa baba mkubwa wangu, mama akaenda kanisani usiku akasema fungenu mlango msitoke nje basi tukatukia ndani.

Kufika mishale ya saa 3 hivi zikapita ngoma balaa enzi hizo mikesha ina vibe ni ngoma za madumu na nyimbo si tukashwishika kaifwata. Tukazunguka na ngoma hadi saa 6 usiku kaka yangu akakutana na washikaji wake akaniacha na ngoma matokeo yake ngoma ikaisha watu wananza kurudi makwao najikuta nipo mtaa wa mbali kishenzi na home halafu kufika nyumbani lazima nipite msitu mkubwa wenye makaburi na ilisemekana kuna majini.

Nilileta kisa hiki mkesha wa mwaka mpya mwaka jana

 
Mkuu na wewe ulikaa seed farm pale igowole kwa mwalimu kauta aloooo wewe ni chuma kama mimi. Pia nimepita pale.

Kauta hoyee .. alinikimbiza na mlinzi nilitoroka kwenda kuiba mapindigesi [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Shangaziii [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚Aunt nilikuwa na matukio Kuna moja baba alinipigia na banio la moto ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
1. Kumtukana mwalimu Mbando kumbe alikuwa nyuma yangu sikumuona. Nikiwa shule ya Msingi kulikuwa na Mwalimu mmoja mkali na anachapa sana alikuwa anaitwa :Mbando". Sasa siku moja nikiwa na wenzake nikawa namtukana kuwa Mwalimu "Mbando ni Mpumbavu" sana kumbe alikuwa anakuja na yupo nyuma yangu. Wenzangu wala hawakunishtua. Hahaaaaaa, nilipigwa sana siku hiyo na nikaambiwa nije na wazazi shuleni.

2. Nimeanza Msingi 1991. Kulikuwa na Mwalimu mmoja anaitwa Mwalimu "Shilla" alikuwa mkali sana. Akanipiga kibao kwani nilikuwa napiga Kelele. Hahaaaaa nikatoka nje na kuokota mawe na kuanza kupiga juu ya bati la shule kwa hasira. Hapo ndipo niliacha shule rasmi. Mwaka 1992 nikaenda tena shule. Nikamkuta yule yule Mwalimu Shilla ndio mwalimu wa Darasa la kwanza. Akanifukuza nikaanza kumlilia na kuomba msamaha. Akajua sasa nimekuwa akaniruhusu kuanza rasmi darasa la kwanza.

3. Simu 1 na wenzangu tumetafuta yale matunda ya minyonyo. Tukachukua zile mbegu zake na kuzikaanga kwani tulisikia yanatoa mafuta ukiyakaanga. Tukawa tunayale yale mambengu pamoja na mafuta yake yaliyokuwa yaanza kutoka kwa kuyakaanfa kwenye moto. Sitasahau jinsi tulivyotapika siku ile.
 
Naona Leejay49 amelike pilau...๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ Itakuwa anapenda pilau huyu lee
 
Du hii balaa aisee!
1. Je, alizeti ilikuwa ya kula hadi ukawanyima wenzako? Kuna mahali fulani niliona watoto walikuwa wanakaanga alizeti. Mlikuwa mnakaanga mnakula?

2. Pole kwa kukatishwa mgegedo. Ina maana mama alipoondoka hukupata tena genye za kuendelea kugegeda? Hahahaha!

Back to story sharing................
Kipindi nikiwa shule ya msingi, tulikuwa na ujinga wa kujificha juu ya miti. Tuliamini kwamba mtu ukipanda juu ya mti aliye chini hakuoni. Utoto bhana!

Sasa siku moja mimi na mwenzangu tukajificha juu ya mti ili kukwepa kuonekana kwa walimu. Kumbe mti tuliojificha upo mbali na mahali alipokuwa mwalimu mkuu akiwapa adhabu wanafunzi wenzetu (huku tumevaa mashati meupe). Eeh bwane ehh, kumbe mtu akiwa mbali na miti anakuona vizuri tu aisee!

Basi mwalimu alipotuona akamtuma mwanafunzi mmoja mkubwa atufuate. Ile kushtuka huyu hapa! Tukashuka harakaharaka tukataka kukimbia lakini tukajua hata tukimbie hatuwezi kufua dafu. Sanasana tutakuwa tunajiongezea idadi ya makosa. Na huyo mwalimu aliyemtuma kutushusha hana masikhara aisee. Tukaone isiwe taabu tukajisalimisha tukakamatwa mateka akatupeleka kwa mwalimu.

Siku hiyo tulikula fimbo kidogo nijikojolee. Tangu siku hiyo tukaona tena kupanda kwenye miti hakutusaidii. Tukawa wanafunzi watiifu hadi tulipohitimu shule.

Utoto raha sana aisee!
 
Hahahaha! Pole sana mkuu. utoto raha sana. Ungesem ukweli wangekuua, bora ulipobakia kuwa jeuri. Hahahaha!
 
Mimi binafsi nilichelewa sana kuanza kujihusisha na mambo ya ngono katika ukuaji wangu, lakini nilipokuwa chalii flani hivi nilijaribiu kujihusisha na tabia hiyo mbaya na kwa bahati nzuri sikufanikiwa.

Mara zote nlipojaribu nilijikuta katika mikono ya wazazi na wana jamii wenye nia niema.

Katika majaribio yangu yote mawili niikamatwa, na hii ilinipa fedhea sana katika umri ndogo maana sasa ikaonekana kwamba mimi ni mtoto mshenzi na sipaswa kuaminiwa japo nilikuwa mpole sana.

Tulihama ule mtaa, na skuwahi tena kujihusisha na tabia hiyo chafu mpaka nilipokuwa na umri sahihi.

Jamii ilinichukulia kama mzaririshaji wa kingono na mbakaji, lakini cha ajabu washkaji zangu walikuwa wanafanikisha ๐Ÿ˜…
 
Wakati nikiwa chalii, kwa mtoto wa kiume kuwa na m.avuzi ilikuwa dili sana, ila Mimi na mdogo wangu hatukuwa nayo.

Sasa kwenye kupiga story kitaa, wadau wakawa wanasema ukikojoa kwenye jiko asubuhi utaamka na msitu wa kufa mtu. Usiku baada ya kula, tukavizia wengine wameenda kulala, Mimi na dogo tukaenda kukojolea jiko.

Asubuhi palivyokucha kabla hata hatujapata muda wa kujikagua m.avuzi kama yameota au la, tuliamshwa na Mshua. Ile ndio ilikuwa mara ya kwanza kuiona bad side ya Mshua.

Ofcourse alinipatia somo pia, kwamba m.avuzi yanaambatana na maumivu. Tokea yameota rasmi, shida haziishi, majukumu yanazidi n.k
 
Dah hatari sana .
Mpende sana mama lakini nahisi sasa umebadilika maana hamkawii nyie watu wa hivi tukikutana bar mnatutegeshea tunaenda maliwato mnakojolea kwenye vinywaji vyetu [emoji848]

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Darasa la nne lilikua na uhaba wa dawati, tukaitwa mbele wote, mwalimu akaanza kupanga moja moja mpaka dawati lijae, bahati mbaya mimi nikawa wa mwisho nikaambiwa nitafute dawati lolote nikae, hapo kila dawati lina wanafunzi wa tano, kila ninapoenda nakataliwa , niliumia sana ila kwa vile nilikua mnyonge tokea chekechea sikujali sana, mwalimu alilazimisha nikae kwenye dawati la wanafunzi wembamba hivyo rukwa sita ila mimi nilikua nakaa upande.

Wiki ile ikaisha nikapata wazo , mpaka darasa la nne liishe nitateseka sana , jumapili kanisa letu lilikua karibu na shule, ibada yetu watoto ilikua ibada ya pili , niliwahi asubuhi sana nikaenda shuleni, nikaenda kuchukua dawati darasa la kwanza nikaleta darasa la nne nikaliweka nyuma kabisa.

Jumatatu ikafika japo nina wasi wasi lakini niko nafurahia kukaa dawati nzima peke yangu!
Sikuulizwa ila mpaka natoka darasa la nne nilikua nakaa kwa ku enjoy sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ