Depal
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 51,716
- 208,985
Hahaaa mkuu Certified Hater matukio yako yale uwa ni vichekesho sana, ndo vile tu umetoroka… ukirejea utajibu.
Ilibidi ukae na walimu uwaeleze, tena uwazuge kuwa umeona wala sio ndoto[emoji1787][emoji1787]Nikiwa primary school nilikuwa mpole na mkimya sana hali iliyopelekea kupendwa sana na baadhi ya walimu, ilifikia hatua nikawa miongoni mwa wanafunzi wanaoachwa kuadhibiwa hata likiadhibiwa darasa zima( wengine wanaachwa kwa sababu mbalimbali kama za kiafya). Darasa la 5 akahamia mwl mmoja wakike ana mwanae wakwanza wakiume mwenye jina kama langu, alikuwa mkali sana ila hakuwai kunipiga kabisa alikuwa ananipenda kwa sababu n mtulivu na nna jina kama la mwanae.
Nikawa siadhibiwi kazi yangu ni kuleta fimbo nzuri kwa ajili ya kuadhibu wengine na kwa akili za kitoto na nilivyokuwa mtiifu kufuata maelekezo nilikuwa naleta fimbo nzuri kweli kweli. Nilikuwa na chimbo langu mtoni kwenye mti mmoja ulikuwa umenyooka haswa na fimbo zake hazivunjiki haraka.
Hii ikanijengea chuki kwa baadhi ya wanafunzi wenzangu na ukizingatia mimi huwa siadhibiwi.
Usiku mmoja nimelala nikaota nimefuata fimbo kama kawaida, kabla sijafika kwenye ule mti nikaona mzuka/mzimu unatisha umevalia mavazi meupe juu mpaka chini, nikasita kuendelea nikaanza kurudi nyuma, ghafla ukaanza kunifuata na kunifukuza ile nageuka ili nikimbie vizuri nikashtuka usingizini.
Alooh kuanzia ile siku nilikoma kwenda kufuata fimbo kwenye ule mti, nikawa nachukia ile kazi kadri siku zilivyosogea nikawa napeleka vifimbo vya hovyo na mwshowe nikaambiwa naona kazi imekushinda, akapewa mtu mwingine. Ile ndoto kuna namna ilikuwa na ujumbe maana ilinitisha kweli kweli.
😂 huyo mwl alikuwa mkali sana nisingeweza kumwambia ila nilijiongeza kitoto nikabuni mbinu mbadala.Ilibidi ukae na walimu uwaeleze, tena uwazuge kuwa umeona wala sio ndoto[emoji1787][emoji1787]
Namba 3 nilikuepo!1. Mwalimu alikuwa anakaa kwenye koti na kukihamisha na kudondoka chini pwaa. Darasa zima lika Cheka. Ila Mungu c athumani adhabu alipewa mwingine . Maana nisogeza kiti na kusogea mbele.
Ilipogundulika ni mimi. Nikaambiwa nije na mzazi. Nilishambuliwa na ofisi nzima ya walimu. Na kurudi nyumba kama season nyingine ya adhabu.
2. Tupo na Wana Huwa tunatabia yankuchokoza mbwa wa geti Kali, tunachungulia kwenye upenyo tunabweka wuuu,wuuu, mbwa anabweka hatari, siku hazigandi tunaona Raha wenzangu wakawa wanapanda kwenye geti na kumfanya mbwa afyatuke kwenye mnyororo wake akaukata. Aloooo, bwana Yesu saidia nilikimbia kimya kimya niliposimama nikaamza kulia.
Jamaa yetu alipigwa bite za kutosha akalazwa na kuchomwa sindao za mbwa kichaaa.
Wengine ikawa adhabu mkienda kumwona fimbo 12.
3. Mechi za ndondo kapu kati ya mtaa na mtaa, Kuna watoto wa mabibo jeshin wakaja kucheza kwetu , tukafungwa tukaleta uhuni kuwa tupo mtaani kwetu tukachomoa goli ilikuwa matawi ya mnazi lilikuwa upande wetu tukarusha kwenye nyumba mojawapo ikaingia ndani, ugomv8 ugomvi jamaa yetu mmoja mjukuu wa Mary chipungahelo akagungulia mbwa wake wahuni wakakimbia woote, tukajua tumemaliza
Saa mbili usiku wakaja tena na brothers zao wengine walikiwa sijui MP wale waliangusha kichapo, kwa watu wengine sisi kwenye ugomvi tukampiga dogo mmoja baba yake.mjeshi nahisi aliumia vibaya jichoni. Mpaka sasa nichongo. Ulikuwa mzozo mkubwa sana. Lakini kesi sijui iliishaje .
4. Kuiba /kupora kofia ya police, akiwa anacheza kamali. Aisee cjawahi kuona police anakuwa mpole kiasi kile l, hii kesi yake tulipona kwa sababu aloyekuwa kwenye kesi alikuwa mjukuu wa Mkubwa.
5. Kesi zilivyokuwa nyingi nikapelekwa kijijini kama adhabu. Shule moja inaitwa igowole ipo mufindi. Mkataba wa kwenda Kule nikifanya ujinga wowote, mzazi hayupo na hakuna wa kunitetea, Kule nikakutana na watoto wanatoka morogoro wamepinda balaa, tunakumbuka shule ilikuwa na miradi tofauti, walimu wetu ndo walikiwa wanafaidi direct na ile.miraid, gafla wanafunzi wakagoma na maandano na mgomo mimi nikawa moja ya VIONGOZi wagomaji kwa stand 1. Migomo ya zamani ni kupasua vioo vya madarasani shuleni, nyumba za walimu, kubomoa ghala za misosi na pamoja na kuchoma mifugo na kuharibu mazao.. mishale ya saa 6 kwenda saa 7 fujo zimekolea kumbe FFU WALIKUJA KIMYA KIMYA C GIZANI. GAFLA UNASHANGAA MTU KAVAA KIOO KAMA ANAENDA KUVUA KAMBALE mabomu wa machozi mawili tumedakwa kama kuku wote. Wengine tukalal porini kwenye magogo baridi inatupiga... Aisee nimechoka kuandika
Ila Mungu alikuwa anasikikiza sana Sala za Mama, maana Kuna siku alikuwa anasali sitting room anasema Mungu huyu mtoto nakukabidhi wewe, ikiwezekana kama sio mpango wako asiwe wangu mpeleke Sehemu sahihi kama Yusuph. Alooooo
Ila na wewe mchokozi aise! Kama hivi visa unavifikiliaje?
1. 200.....hapo nipo F5, boarding, nkatoloka. Maisha ya kuaa ndani huku ulikuwa dei,hayakuwa sawa. Kukawa na mshikaji nilisoma nae, kumbe kwao kuna rubisi,kali af tamu balaa. Nikanywa weeee,kumbe moshi unapanda mi sielewi. Njia ya kwenda kwao,kuepuka kukutana na mtu,ni sehemu ya kufugia ng'ombe wa maziwa,pamezinguushiwa senyenge.
Kukawa na maembe sasa. Ile narudi mida ya saa moja,mi naenda tu,nikasema niwapelekee washikaji hata maembe. Nkacuma,badhi yameiva,mengine mabichi na machanga humo humo.
Cha kubebea,hamna! Kuvua tu shati. Litafuliwa litakate,hapo sikuwa naelewa. Kuna mitalo ya maji humo balaa. Nikikanyaga, muguu huo,umezama. Hatua chache mbele,mzima mzima.
Naangalia sehemu ya kutokea,siioni. Maembe hapo yanamwagika na kupungua tu. Suruali na viatu,mwenyewe jiulize. Nilibahatika kukatiza barabara,nikaenda. Sikupita getini,nilipita njia za panya.
Mi sinajua naenda kwa majama,af ndo ilikuwa mara yangu ya kwanza kulewa sasa. Maembe yalobaki hayazidi hata 10.
Nimepita nkaingia darasani hapo ni mda wa kujisomea. Kumbe,kuna mwarimu hapo alikuwa amekuja kusaidia kurudia,kakaa kwenye viti vya wanafunzi. Naingia na maembe na suruali na viatu vimelowa, dah! Fedheha ya maisha nilopata nadhani ni ile tu. Nikatonywa,mi sielewi. Nadhani ile kutembea iliongeza wenge.
Maembe sikumpa mtu,nikaweka tu juu ya dawati.
Nashuka kuelekea bwenini, dah! Nkapoteza ramani mazima.
Kesho yake sasa, ndo naitwa na kupewa off siku 7,na kurudi na mzazi.
*****, naanzaje sasa! Khah!!!!!! Acha tu niishie hapa
2. Tukio la pili,nikiwa nasoma kama darasa la 2 au la tatu,acha niende kuiba asali🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣. Aiseee!
Nikatafuta mti mrefu,nkapata. Kuna mizinga ilikuwa karibu na kwetu ya jirani. Mi sijui asali ntapata au sipat. Na lengo likawa tu nitoe kifuniko cha mzinga(ile mikubwa ya zamani), kweli kikadondoka. Kuangalia,nkaona hapa ntashambuliwa. Akili za kitoto bwana. Nikajisemea ngoja tu nichovye na kile kijiti. Hata basi nililamba! Kilichonikuta sitokaa nisahau. Ila nachojua karibia mtaa mzima walisikia kilio na kuwahi. Kila sehemu ya mwili,nilidungwa. Baada ya mda sasa,mwili mzima unawaka moto, mdomo unapima kama kilo 10.
Fika ofisini kesho! Lile Bomba lazima mtengeneze1____uharibifu mali ya umma mtaani kulikuwa na bomba la kupump Danida ni bomba lilikuwa linatumika kijiji kizima,
,usiku mida ya saa mbili tulipangana na rafiki yangu tukaharibu bomba, tulifanikiwa kulifungua lilifyatuka pira ni refu hatari,tulifungua na kuvuta pira asubuhi wananchi wanashangaa bomba pira lipo nje limeharibika kaharibu nani hawajui[emoji23][emoji23]
Na halikutengenezwa hadi leo maana ni gharama ,nikilionaga nacheka[emoji23], tulifanyaga siri, tungegundulika tungepewa adhabu kali mno na serikali.
2____Wizi nilikuwa na marafiki zangu wawili tukavamia shamba la viazi la watu,viazi vilikuwa havijakomaa, tuling'oana nusu shamba,
Kumbe mwenyewe yupo ng'ambo anagomba kuwa tuache kuharibu viazi vyake,sie tupo bize,
Usiku nimetulia home nasikia hodi,mmama mwenye viazi kaja kunichukua yupo na wale waizi wenzangu[emoji23],
Akatupeleka shamba akatuambia tukusanye mbegu zote,tulikusanya kila mmoja na mbegu zake na kila mmoja akaenda kutukabidhi kwa wazazi wetu na zile mbegu tupanda then tumpelekee viazi,
Baba(ra) alinikamata nikajifanya kumponyoka kukimbia alinikimbiza alivyonikamata alinipiga vibaya mno, hii ilikuwa ni mara ya kwanza na mwisho kupigwa na baba,
3___Kupigwa na wavulana
Home kulikuwa kuna duka,sasa wakija dukani kununua vitu nawachokoza then nakimbilia ndani, siku hiyo nimetania na mama yupo nikajua mama atanitetea, tania kimbilia ndani mama akanitoa kunikabidhi kwa mvulana kuwa anipige[emoji23],tukadundana nilivyoona vinanishinda nikajizimisha[emoji1787][emoji1787] mama alivurugwa,
4____kupigana na mvulana huyu nilikuwa namtania Jose likichwa siku akanifuma njiani na kuniambia tania kama unavyotaniaga ukiwa kwenu[emoji23], nilikaa kimya,akaanza kunipiga mwenyewe sio mnyonge tulipigana akaniangusha chini,nikalala kujifanya nimezimia, pembeni kulikuwa na betri mbovu zile kubwa za tochi, niliokota nikampiga nayo jichoni na kukimbia, baba alimtibiaga, hadi leo yule mkaka ana alama isiyofutika jichoni,
5___kufungulia bomba usiku maji ya mwagike,
Ni uwanjani wa umma kuliwekwa bomba la koki na walikuwa wanafunga na boksi na kufuri, mie na group langu tulikuwa tuna vizia mida ya jioni hivi tunaenda penyeza vidole tunafungulia maji yanamwagika usiku kucha,
Kiufupi tu,nilikuwa mkorofi,muharibifu kufungua vitu na kuvitengeneza tena, Baba alikuwa ananiita jike dume[emoji23]
Ahsante mama kwa kunipambania,maana bila fimbo/ukali wa mama sijui ningekuwaje[emoji1317]
Kivipi? Kipi hujaelewa?mkuu umefika advance kweli... maana nimejitahidi kuelewa ulicho andika akili inagoma...!
Hahaaaaa, sipati picha hilo yowe lilikuwaje.Kuna mtaa wa msisiri kinondoni pembeni kuna soko kubwa tu.
Soko lipo katikati ya mitaa mingi ila upande wa tulipo kuwa tunakaa kabla hujafik ndanindan unakutans na butcher safi tu kipind hiko.
Ilikuwa jioni tupo sokoni sijui tulifata nini kushangaa shangaa me nilikuwa nachezea zipu y kibukta changu cha jeans na zipu ya chuma si kigovinda changu kikanasa kwenye zipu
Nilitoa kilio sitokuj sahau soko lote likaja kwangu yule mwenye butcher alivyo kuja akasema kama ni govinda basi wanitahiri pale pale alooooo nilipiga yowe mpk wakanibeba kunipeleka home ndy kwenda kutolewa.
Nilitahiriwa week after hilo tukio mana walisema tushapata sababu nzuri ya kukukata.
HahaaaaaNiko darasa la pili.
Tuko kwenye nyumba ya udongo hamna umeme na choo kiko nje.
Nikabanwa haja kubwa ile kabisa choo cha kuendesha. La haula. Siwezi toka kuna giza tororo nje, ikabidi nitafute plan B. Wazo likaja nishushe mzigo kwenye gazeti nitupe kesho yake. Tafuta gazeti wapi. Nikapata jalada gumu la juu la daftari. Shusha mzigo nikautupia kwa dirishani upande wa pili. Maana kuna wapangaji wengine upande wa pili na kuna sehem panatupwa uchafu.
Kwenye kurusha nikarusha vibaya ukawa usawa wa mpangaji mmoja. Mbaya kuliko yote jalada la daftari lina majina yangu yote matatu. Kushtuka asbh nasikia bi mkubwa anaulizwa mtoto wako ni flani? (Yakitajwa majina yote matatu ya kwenye jalada). Hiyo aibu ilinifanya niwakwepe majirani wote kwa miezi kadhaa. Nilitamani nijifiche nisionekane maana kila mtu akajua mzigo ni wa fulani
sio Tanga hiyo...handeni huko🤣🤣🤣 nahisi tumesoma wote wewe mwambaShuleni nilikua mkimya na mtulivu sana kiasi kwamba asilimia kubwa ya wanafunzi wenzangu walijua sisikii vizuri, kwasababu sikua na desturi ya kuongea hata kama ukiniuliza kitu labda tuwe tuna fahamiana
Basi bhana nikawa napendwa sana na mademu pamoja na walimu , nikawa natolewa mifano hadi pared kwa utulivu na kujipenda kwangu hususani na dalasan sikua vibaya Sana nikawa najipakualia minyama Tu.
Siku moja mwalimu wa fildi alikua anatoa somo class sasa mi nilikua nimekaa na manzi mmoja anaongea sauti ya chini huku pindi lina endelea , akaongea neno nika tabasamu ticha akaniona nakuniita mbele kwa ghadhabu huku akisema Mimi nafundisha wewe unanicheka shika chini hapo.
Hapo nika sita na kusema mwalimu mimi sija cheka umeniona nikitabasamu mwalimu akagoma na kuniforce niadhibiwe aloooh dalasa zima likainuka na kupinga Mimi kuazibiwa .
Dah daktari kama daktari yaani Tanzania ufe kwa mawazo utakuwa umejitakia tuNakumbuka enzi za Utoto miaka ya 1998 kulikuwa na ule mchezo wa Kulinda pale unapoona mwenzako kakamatawa na wale wanaokamatwa kwa kuguswa wanasimama nyuma yako halafu wewe unakuwa umeshilikia mkono mmoja kwenye mti na mwingine anakuwa ndio Mlinzi kumzuia yule anayekuja kuwaokoa waliotekwa, Sasa kuna siku Mimi ndio nilikuwa Mlinzi nazuia jamaa asiwaokoe Jamaa alikuja kwa kasi alinipiga kichwa mpaka nikapasuka mdomo. Nikaenda kushonwa nyuzi saba. Kule Dispensary Dk aliyekuwa ananishona mikono yake ilikuwa inanuka M@vi nadhani alitoka chooni halafu hakunawa na sabuni. [emoji28][emoji28][emoji28]
Nakumbuka enzi za Utoto miaka ya 1998 kulikuwa na ule mchezo wa Kulinda pale unapoona mwenzako kakamatawa na wale wanaokamatwa kwa kuguswa wanasimama nyuma yako halafu wewe unakuwa umeshilikia mkono mmoja kwenye mti na mwingine anakuwa ndio Mlinzi kumzuia yule anayekuja kuwaokoa waliotekwa, Sasa kuna siku Mimi ndio nilikuwa Mlinzi nazuia jamaa asiwaokoe Jamaa alikuja kwa kasi alinipiga kichwa mpaka nikapasuka mdomo. Nikaenda kushonwa nyuzi saba. Kule Dispensary Dk aliyekuwa ananishona mikono yake ilikuwa inanuka M@vi nadhani alitoka chooni halafu hakunawa na sabuni. [emoji28][emoji28][emoji28]
Ilikuwa 1998 hiyo 😂😂😂Dah daktari kama daktari yaani Tanzania ufe kwa mawazo utakuwa umejitakia tu
Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
[emoji16][emoji16][emoji16]1. Mwalimu alikuwa anakaa kwenye koti na kukihamisha na kudondoka chini pwaa. Darasa zima lika Cheka. Ila Mungu c athumani adhabu alipewa mwingine . Maana nisogeza kiti na kusogea mbele.