Grahams
JF-Expert Member
- Mar 19, 2016
- 21,322
- 65,238
UTANGULIZI
Kila mwanadamu ana masimulizi ya matukio kadhaa katika safari yake ya maisha, matukio hayo yanaweza kuwa ni mkusanyiko wa harakati za kiuchumi, kisiasa ama kijamii alizopitia msimuliaji. simulizi hizo, zinaweza kuwa ni matukio yake binafsi, ndugu ama marafiki zake wa karibu ambapo yanaweza kuacha somo kwa wengine.
Kutokana na changamoto za kifedha, kukosa muda, ama changamoto za kiafya, Wazee wengi hushindwa kuandika vitabu kwaajili ya kusimulia harakati zao.
Katika uzi huu, nitakuwa nasimulia matukio hayo kadri nitakavyokuwa nakumbuka, maana kwa jinsi tulivyokula chumvi nyingi, sio rahisi kukumbuka yote
Iwapo utakuwa na tukio, usisite kusimulia matukio hayo ili wengine wajifunze, na kwa kuwa wazee wengi tuna tatizo la kumbukumbu (tusingependa kutaja mwaka husika wa tukio), hivyo matukio na masimulizi hayo ni muhimu kuyaita matukio ya mwaka 47......
MUENDELEZO....

Tukio la dhuluma katika biashara
Mwaka 47 niliingia kwenye biashara ya uuzaji wa vipodozi kwaajili ya Wanawake na Wanaume waliopenda kuongeza mng’ao wa ngozi zao. Biashara hii ilikuwa ni ya pamoja(partnership), Mimi na rafiki yangu Nkya (sio jina halisi) ambapo tulikuwa tunachukua mzigo wa vipodozi Congo DR na kuuingiza Nchini ambapo tulikuwa tukiuza kwa jumla. Tukija na mzigo, ilikuwa wale wenye maduka ya vipodozi, walikuwa wanakuja wanachukua kwetu, kwahiyo tulikuwa hatukai na mzigo zaidi ya siku mbili tangu ufike. Kwa kweli, biashara ilitulipa sana miaka ile.
Mathalani, kipodozi unanunua Congo DR, kwa shilingi 5,000 ya Tanzania, lakini ukija kuuza huku Tanzania kwa bei ya jumla, ilikuwa tunauza kwa 25,000 na wao wakija kuuza rejareja, walikuwa wanauza shilingi 35,000 hadi 50,000
Wanawake wanatumia pesa nyingi sana kwenye matunzo ya ngozi pamoja na nywele zao, iwapo utafanikiwa kubuni biashara ambayo wateja wako watakuwa wanawake, nina kuhakikishia huwezi kulala njaa.
Tulijiweka utaratibu kwamba tukiingiza mzigo, baada ya mauzo ilikuwa tunatenga hela ya mtaji pembeni, gharama za usafiri, kupoza maafisa huko njiani kisha tunagawana faida. Na kwenye hiyo faida, tunachukua almost 50% ya faida, kisha 50% nyingine tunaiongeza kwenye mtaji, ili kukuza biashara.
Wakati fulani, biashara ilipokuwa imeshamiri na yenye faida, mbia mwenzangu, akaingia tamaa, akatokomea mitini na mtaji pamoja na faida yote ya biashara.
Nikaanza kumtafuta, bila mafanikio, nakwenda nyumbani kwake kila siku naambiwa hayupo, baadaye wakahama mtaa kabisa, hivyo nikashindwa kujua kwa kumpata kabisa.
Wazo likanijia, kumtafuta maeneo tulipokuwa tunachukulia mzigo, nikawa naenda kumtafuta kimya kimya, hadi nikafanikiwa kukutana naye. Jamaa akanijibu mbovu pale, na kunitishia juu.
Safari ya kulipa kisasi…. Usione kobe ametulia, ujue anatunga sheria…
Ni watu wachache sana wenye uwezo wa kusamehe pale wanapodhulumiwa, Kwasisi Wanaume kisasi chetu huwa ni kwenye fedha,Watoto na Mke. Ukituumiza kupitia moja wako katika hayo, ujue ni lazima kisasi kitalipwa. Mimi pia nilichagua kulipa kisasi.
Baada ya ugomvi wetu na Bwana Nkya, nilimwacha akasahau miezi 6 hivi ikapita.
Baadaye nilirudi tena eneo tulipokuwa tunachukulia mzigo, nikakusanya taarifa nilizokuwa nahitaji, hasa kujua mzigo mwingine alikuwa amepanga kuuchukua lini, na angepita barabara ipi kuusafirisha na angetumia gari ya nani kuubeba. Mind you, biashara hii tulifanya bila kuwa na makaratasi (Someni na muelewe hivyo hivyo tu).
Baada ya kujiridhisha kuhusu hayo yote, siku 23 baadaye mzigo wa jamaa ulikamatwa, na ukataifishwa na jamaa alikaa mahabusu zaidi ya miezi 6
Hakuna bidhaa adimu kwa sisi Watanzania kama uaminifu, ni Watanzania wachache sana wanaoweza kufanya biashara ya pamoja bila kudhulumiana.
Mnaweza kufanya biashara za pamoja, lakini wekeni vizuri kwenye maandishi (Mikataba).
Otherwise, unaweza kupoteza jasho lako kwa dhuruma ya mtu uliyeaminiana naye.