Share nasi matukio yako ya ukuaji

Share nasi matukio yako ya ukuaji

Nikiwa Darasa La Sita Wakati Nywele Sehemu Nyeti Zikianza Chipuka Nilianza Tabia Ya Uzururaji Nakumbuka Kuna Cku Nilitoka Nyumbani Saa 9 Mchana Mm Na Rafk Yangu.Aisee Tulizurura Sana Ikafka Saa 2 Ucku Nikaenda Kwa Rafk Yangu Mwngne Alikuwa Na Laptop Nikaanza Chezea Laptop Yake Mpaka Saa 5 Ucku Huku Nyumbani Hali Si Shwari Natafutwa Na Viboko Vimechumwa Viko Ndani Aisee Niliporud Nilifungiwa Ndani Niliisoma Namba Kwa Kirumi Hyo Tabia Ilifika Ukomo Siku Hyo

Mbokoo[emoji23][emoji23]
 
Hi ilikua mbaya sana

Kuna jamaa alihamishwa kikazi kwenda mkoani mwingine
Akaja home akawwkeza vyombo vyake
Kwahyo siku mojamoja tuliingia na kufanya usafi kule ndani
Siku moja nkaanza kupekua vitu vyake
Pekuuuuaaaa mabegi mabox na matakataka yoote
Si nkakuta na cd ya x bwana!
Kiboro full kudinda nkiangalia ile cover yake tu😅😅

Nkaona nipande nayo sebleni
Nkamkuda mdogo wangu wakike mmoja
Nkamtonya angalia hi cd nmeikuta kule chini
Akasema weka tuangalie
Tukapunguzz sauti tukatia mzigo ndani

Tukaangalia SEBULENI mimi na mdogo wangu cd ya x
Sijui tungefumwa ingekuaje😅😅😅
 
1. Nipo msingi miaka ya 1990's. Tulikuwa tunapikiwa uji shuleni ila sukari ilikuwa inawekwa ndogo. Nikawa naiba sukari home na kwenda nayo shule. Kumbe Baba akashtuka. Hakujisumbua nami alichofanya ni siku 1 nimevua kaptura yangu ya shule yeye akaishonea tu mifuko ya kaptura yangu ya shule, hivyo mifuko haikuwepo tena. Siku hiyo sina hilo wale lile. Nimeiba sukari Ile naweka tu kwenye kaptura yangu. Hahaaa yote imemwagika chini. Hahaaaaaa, nikala mbio hatari.

2. Nimekulia kotaz kule kwenye kiwanda cha Mkulazi Morogoro. Tukacheza mpira kati ya mitaa miwili. Mpira haujaisha tokana na ngumi. Jamaa mmoja akanipiga na kunitegua kidole cha Mkono wa kulia. Kidole cha katikati kilipinda. Sikusema nyumbani wala mueleza mtu kumbe kuna watu waliona nikipigana na walimwambia mzee wangu. Jioni tunakula ugali kumbe mshua anaangalia mikono yangu. Ile nanawa tu tuanze kula, mzee akanishika mkono na kuniuliza umefanyaje kwenye huu mkono. Hahaaa, mzee akaninyoosha kile kidole bila ganzi.

3. Kulikuwa na nyuki wameweka mzinga wao kwenye yale mambomba ya kutolea moshi kwenye zile nyumba za zamani. Tupo darasa la kwanza, si tukaenda kuwapiga mawe na kuwachokonoa? Hahaaaaaa, nilikuwa natapika, naharisha na kucheua harufu ya asali zaidi ya wiki maana sio kwa kung'atwa kule.

4. Nyumbani kwetu tumezaliwa wanaume 4 na msichana mmoja. Msichana ndio alikuwa mkubwa wetu ila sisi tumefuatana. Sio kwa kupigana kule. Si mama akitutuma au wakati wa kula au kusafiri. Tulizipiga na niliyefuatana naye siku 1 tukienda Machame na wazee hadi wachaga wa kule Kikavu wakawa wanatushangaa. Kuna siku nusra nimuue kaka yangu mkubwa kwa kumpiga nondo ya kichwa tokana na kunitania wakati tunacheza mpira. Hadi sasa ana alama kwenye utosi.
 
D

ah hapa mkuu zote nondo

Kwahyo kidore kikanyooka😥😥😥 hayo maumivu mzee
 
Kulikuwa na kamchezo ka kuruka sarakasi kwa kudanda kwenye Tairi la Gari nusula nivunje shingo sija sahau !
 
Daaah nimekumbuka mbali sana. Enzi ya asante Mkapa, RIP Big Benji, nikiwa darasa la pili nilikua napenda sana kwenda vibanda umiza vile vilikuwa vinaonyesha movies. Sasa ratiba ilikua hivi asubuhi mpaka sa6 mchana ni picha za kihindi huwa ni ndefu hivyo huwa mbili tu, sa7 picha za kibongo hadi sa10 au kizungu inategemea, sa10 hadi sa1 usiku ya kihindi ya kumalizia siku. Baada ya hapo watu hutawanyika lakini kwenye ule ubao wa kuwekea makava ya muvi nilikua nasoma kwa chini kila siku wanaandika leo usiku kutakuwa na pilau. Sasa nafikiri ni curiosity na utoto wa kutojua pilau ni nini? Siku moja nikasema leo siondoki, baada ya picha ya kihindi ya jioni kuisha nitasubiri mpaka na mimi leo nile hilo pilau nikidhani ni msosi. Sasa binamu zangu ambao tulikuwa na umri sawa wakati wanaondoka bandani baada ya picha ya kihindi nikawa nawashawishi tubaki wote tule pilau wakasema watoto hawaruhusiwi sikukata tamaa, nyuma ya lile banda kuna matobo yalikuwepo ambayo unaweza kuona ndani, nikasema nitajibanza kwa nyuma ya banda hadi mda wa pilau ufike wakipakua nitaenda na hakuna atakayenifukuza(masikini ningejua ningeondoka na binamu zangu).
Basi muda ukafika nikastaajabu kuona wake kwa waume, wababa kwa wamama, na mabraza na masista du wa mtaani wanaingia bandani, hapo ishafika saa4 usiku, laahula VHS ikafunguliwa wakatia mkanda wa tofali daaah nilichokiona (ilikua siku yangu ya kwanza kucheki porno) na kwa kuwa nilikua nachungulia toka nyuma ya banda nikawa naona na wale waliokaa nyuma walichokuwa wanafanya ni laana.
Sasa bana msala ulianza pale lile zoezi la pilau lilipoisha nisijue ishakua sa6 usiku na nimeshatafutwa kinyama bila mafanikio, na binamu zangu walipoulizwa wakasema nilikua nasubiri pilau, wewe sikia tu kama sikuzimia siku hii kutokana na kipigo sitazimia tena mshua alinidunda kama anaua nyoka.
Sasa nilipokua naulizwa umekula wapi pilau? Mimi kimya. Hapa nyumbani hauli? Mimi kimya. Mama anadakia huyo jeuri unaona hajibu, asijue ni mambo ya ajabu nimetoka kutazama nashindwa hata kuyaelezea. Siwezi sahau hii siku asubuhi nilipelekwa hospitali baada ya kupata homa kali na vijipu sababu ya kipigo.
 
1____uharibifu mali ya umma mtaani kulikuwa na bomba la kupump Danida ni bomba lilikuwa linatumika kijiji kizima,

,usiku mida ya saa mbili tulipangana na rafiki yangu tukaharibu bomba, tulifanikiwa kulifungua lilifyatuka pira ni refu hatari,tulifungua na kuvuta pira asubuhi wananchi wanashangaa bomba pira lipo nje limeharibika kaharibu nani hawajui[emoji23][emoji23]

Na halikutengenezwa hadi leo maana ni gharama ,nikilionaga nacheka[emoji23], tulifanyaga siri, tungegundulika tungepewa adhabu kali mno na serikali.

2____Wizi nilikuwa na marafiki zangu wawili tukavamia shamba la viazi la watu,viazi vilikuwa havijakomaa, tuling'oana nusu shamba,

Kumbe mwenyewe yupo ng'ambo anagomba kuwa tuache kuharibu viazi vyake,sie tupo bize,

Usiku nimetulia home nasikia hodi,mmama mwenye viazi kaja kunichukua yupo na wale waizi wenzangu[emoji23],

Akatupeleka shamba akatuambia tukusanye mbegu zote,tulikusanya kila mmoja na mbegu zake na kila mmoja akaenda kutukabidhi kwa wazazi wetu na zile mbegu tupanda then tumpelekee viazi,

Baba(ra) alinikamata nikajifanya kumponyoka kukimbia alinikimbiza alivyonikamata alinipiga vibaya mno, hii ilikuwa ni mara ya kwanza na mwisho kupigwa na baba,

3___Kupigwa na wavulana

Home kulikuwa kuna duka,sasa wakija dukani kununua vitu nawachokoza then nakimbilia ndani, siku hiyo nimetania na mama yupo nikajua mama atanitetea, tania kimbilia ndani mama akanitoa kunikabidhi kwa mvulana kuwa anipige[emoji23],tukadundana nilivyoona vinanishinda nikajizimisha[emoji1787][emoji1787] mama alivurugwa,

4____kupigana na mvulana huyu nilikuwa namtania Jose likichwa siku akanifuma njiani na kuniambia tania kama unavyotaniaga ukiwa kwenu[emoji23], nilikaa kimya,akaanza kunipiga mwenyewe sio mnyonge tulipigana akaniangusha chini,nikalala kujifanya nimezimia, pembeni kulikuwa na betri mbovu zile kubwa za tochi, niliokota nikampiga nayo jichoni na kukimbia, baba alimtibiaga, hadi leo yule mkaka ana alama isiyofutika jichoni,

5___kufungulia bomba usiku maji ya mwagike,

Ni uwanjani wa umma kuliwekwa bomba la koki na walikuwa wanafunga na boksi na kufuri, mie na group langu tulikuwa tuna vizia mida ya jioni hivi tunaenda penyeza vidole tunafungulia maji yanamwagika usiku kucha,

Kiufupi tu,nilikuwa mkorofi,muharibifu kufungua vitu na kuvitengeneza tena, Baba alikuwa ananiita jike dume[emoji23]

Ahsante mama kwa kunipambania,maana bila fimbo/ukali wa mama sijui ningekuwaje[emoji1317]
 
Enzi tunajipikilisha mchanga na vikopo vya blue band huku mnapuliza moto km vile mchanga unaiva,
nilikua na tumpe
tuko vitoto
mara kanishawishi tukaunge vikojoleo vyetu.
Si tukazama choo cha jirani.
Ile tunagusishana tu.
Katokea jirani gani sijui kazama ajisaidie.
Tulitoka baru mle ndani na yeye alikula kikumbo mpaka kaanguka kwenye ngazi.
Hapo tumpe kala njia yake mi yangu.
Tunamskia tu jamaa anasema
"Tumpe ntakusemea kwa mamaako ulikua unafanya matusi"
Si hapo hatuna time.
Dah shughuli yote ya upishi wa wali wetu wa mchanga ikaishia hapo.
Matukio mengine yanakuja.
 
Mimi niliruhusiwa kuhudhuria mahafali muda wa kurudi niliambiwa ni saa 9 kamili niwe home nikachelewa nikafika home saa 10 nikajificha naogopa kipigo had saa 12,nasikia ndani wanavoulizana nimejibanza dirishani nimejificha baba akapata uoga akaenda had shule kuniulizia karudi namuona muda huo ni saa 1 usiku wamepika hawajala wanaulizana nawasikia, Mimi nikaanza kuzunguka nyumba natafuta pa kupitia nikakosa

Mama akaenda kuuliza Kwa majirani wakasema waliniona wakat narudi jioni inakuwaje nisiwepo wakaanza msako majirani wote na wazazi wangu, nikakimbia najificha kwenye miti eneo la jirani wakipita huku naelekea upande mwingine msako ulikuwa mkali had saa 5 usiku watu hawajalala [emoji2][emoji2][emoji2]Mimi Sina nguvu ninauoga na njaa inaniuma balaa,mbu washaniuma wa kutosha [emoji23][emoji23][emoji23] walivoniona wakaanza kunikimbiza "huyo huyo" walinibeba juu juu kama mwizi,majirani wakamuwahi baba kumuomba anisamehe asinipige maana wanajua shughuli yake
Yaani hilo tukio linafanana kama langu.

Sema mimi niliagizwa kwa mtu nikaogopa kwenda.
 
Enzi tunajipikilisha mchanga na vikopo vya blue band huku mnapuliza moto km vile mchanga unaiva,
nilikua na tumpe
tuko vitoto
mara kanishawishi tukaunge vikojoleo vyetu.
Si tukazama choo cha jirani.
Ile tunagusishana tu.
Katokea jirani gani sijui kazama ajisaidie.
Tulitoka baru mle ndani na yeye alikula kikumbo mpaka kaanguka kwenye ngazi.
Hapo tumpe kala njia yake mi yangu.
Tunamskia tu jamaa anasema
"Tumpe ntakusemea kwa mamaako ulikua unafanya matusi"
Si hapo hatuna time.
Dah shughuli yote ya upishi wa wali wetu wa mchanga ikaishia hapo.
Matukio mengine yanakuja.
Aiseeee
 
Mimi niliruhusiwa kuhudhuria mahafali muda wa kurudi niliambiwa ni saa 9 kamili niwe home nikachelewa nikafika home saa 10 nikajificha naogopa kipigo had saa 12,nasikia ndani wanavoulizana nimejibanza dirishani nimejificha baba akapata uoga akaenda had shule kuniulizia karudi namuona muda huo ni saa 1 usiku wamepika hawajala wanaulizana nawasikia, Mimi nikaanza kuzunguka nyumba natafuta pa kupitia nikakosa

Mama akaenda kuuliza Kwa majirani wakasema waliniona wakat narudi jioni inakuwaje nisiwepo wakaanza msako majirani wote na wazazi wangu, nikakimbia najificha kwenye miti eneo la jirani wakipita huku naelekea upande mwingine msako ulikuwa mkali had saa 5 usiku watu hawajalala [emoji2][emoji2][emoji2]Mimi Sina nguvu ninauoga na njaa inaniuma balaa,mbu washaniuma wa kutosha [emoji23][emoji23][emoji23] walivoniona wakaanza kunikimbiza "huyo huyo" walinibeba juu juu kama mwizi,majirani wakamuwahi baba kumuomba anisamehe asinipige maana wanajua shughuli yake
Bora ungejitokeza hiyo saa kumi. Saa kumi na saa 9 ni majirani tu [emoji1787]
 
1. Kutoa vivuko vya kwenye mifereji ya maji pembezoni mwa barabara usiku na kutandaza viroba. Kwa hilo Mungu anisamehe. Nilikuwa na wenzangu tunafanya hivyo. Kuna vivuko vilikuwa vinawekwa vya mbao kwenye ile mifereji midogo ya maji pembezoni mwa barabara. Tulikuwa tunavitoa na kulaza viroba tupu tunavyovishikisha na matofali pembeni ili mtu akipita na baiskeli au kwa miguu aanguke nasi tunamcheka.

2. Kujificha kwenye kona na kusubiri watu wapite tuwashtue weeeeeeeee. Kuna kipindi tukawa na mabomba ya Sindano tukawa tunayaweka maji na kumwagia watu huku tunawashtua. Kuna Bibi mmoja tulikuwa tunamuonea. Tunaenda kugonga mlango tukijua ameachwa peke yake nyumbani alafu akitoka tu, tunammwagia kwa kutumia bomba la sindano alafu tunamshtua weeeeeeee.

3. Miaka ya 1990's nikiwa Primary. walianza kuuza viazi vya kukaanga pamoja na nyanya roast shuleni. Sasa mimi sikuwa naenda shuleni na pesa kwani shule ilikuwa karibu na nyumbani. Nikaingia tamaa, ile narudi kunywa chai saa 4 nikawa naiba Shilingi 5 na 10 za wazee walizokuwa wanaweka juu ya kabati lao la nguo chumbani mwao niende kununua na kutambishia wenzangu. Kweli za nwizi ni 40, siku ya 40 yangu ilipofika. Nimerudi shule saa 4 nikanywa chai nikasema niingie chumbani kwa wazee kama kawaida kumbe Baba hakuenda kazini alikuwa amelala kitandani na alishusha Neti so sikumuona. Nikavuta kiti na kupanda kwenye kiti na kuinua mkono juu ya kabati kama Kawa nijichukulie maokoto. Hamada, mshua huyu. Hahaaaaa, nilitimua mbio kutoka chumbani kwao. Sijafika mlango wa nje nikateleza. Hahaaaaa jamaa alinipigia kwa hasira kwani mzee hakuwa anatupiga ila alinipiga kwa hasira siku hiyo.
 
1. Mwalimu alikuwa anakaa kwenye koti na kukihamisha na kudondoka chini pwaa. Darasa zima lika Cheka. Ila Mungu c athumani adhabu alipewa mwingine . Maana nisogeza kiti na kusogea mbele.
Ilipogundulika ni mimi. Nikaambiwa nije na mzazi. Nilishambuliwa na ofisi nzima ya walimu. Na kurudi nyumba kama season nyingine ya adhabu.

2. Tupo na Wana Huwa tunatabia yankuchokoza mbwa wa geti Kali, tunachungulia kwenye upenyo tunabweka wuuu,wuuu, mbwa anabweka hatari, siku hazigandi tunaona Raha wenzangu wakawa wanapanda kwenye geti na kumfanya mbwa afyatuke kwenye mnyororo wake akaukata. Aloooo, bwana Yesu saidia nilikimbia kimya kimya niliposimama nikaamza kulia.
Jamaa yetu alipigwa bite za kutosha akalazwa na kuchomwa sindao za mbwa kichaaa.
Wengine ikawa adhabu mkienda kumwona fimbo 12.

3. Mechi za ndondo kapu kati ya mtaa na mtaa, Kuna watoto wa mabibo jeshin wakaja kucheza kwetu , tukafungwa tukaleta uhuni kuwa tupo mtaani kwetu tukachomoa goli ilikuwa matawi ya mnazi lilikuwa upande wetu tukarusha kwenye nyumba mojawapo ikaingia ndani, ugomv8 ugomvi jamaa yetu mmoja mjukuu wa Mary chipungahelo akagungulia mbwa wake wahuni wakakimbia woote, tukajua tumemaliza
Saa mbili usiku wakaja tena na brothers zao wengine walikiwa sijui MP wale waliangusha kichapo, kwa watu wengine sisi kwenye ugomvi tukampiga dogo mmoja baba yake.mjeshi nahisi aliumia vibaya jichoni. Mpaka sasa nichongo. Ulikuwa mzozo mkubwa sana. Lakini kesi sijui iliishaje .
4. Kuiba /kupora kofia ya police, akiwa anacheza kamali. Aisee cjawahi kuona police anakuwa mpole kiasi kile l, hii kesi yake tulipona kwa sababu aloyekuwa kwenye kesi alikuwa mjukuu wa Mkubwa.
5. Kesi zilivyokuwa nyingi nikapelekwa kijijini kama adhabu. Shule moja inaitwa igowole ipo mufindi. Mkataba wa kwenda Kule nikifanya ujinga wowote, mzazi hayupo na hakuna wa kunitetea, Kule nikakutana na watoto wanatoka morogoro wamepinda balaa, tunakumbuka shule ilikuwa na miradi tofauti, walimu wetu ndo walikiwa wanafaidi direct na ile.miraid, gafla wanafunzi wakagoma na maandano na mgomo mimi nikawa moja ya VIONGOZi wagomaji kwa stand 1. Migomo ya zamani ni kupasua vioo vya madarasani shuleni, nyumba za walimu, kubomoa ghala za misosi na pamoja na kuchoma mifugo na kuharibu mazao.. mishale ya saa 6 kwenda saa 7 fujo zimekolea kumbe FFU WALIKUJA KIMYA KIMYA C GIZANI. GAFLA UNASHANGAA MTU KAVAA KIOO KAMA ANAENDA KUVUA KAMBALE mabomu wa machozi mawili tumedakwa kama kuku wote. Wengine tukalal porini kwenye magogo baridi inatupiga... Aisee nimechoka kuandika

Ila Mungu alikuwa anasikikiza sana Sala za Mama, maana Kuna siku alikuwa anasali sitting room anasema Mungu huyu mtoto nakukabidhi wewe, ikiwezekana kama sio mpango wako asiwe wangu mpeleke Sehemu sahihi kama Yusuph. Alooooo
Hahahahaaa nimecheka sana mwisho hapo eti mpeleke sehemu sahihi kama Yusuph, bimkubwa hahahhaaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom