Ila na wewe mchokozi aise! Kama hivi visa unafifikiliaje?
1. 200.....hapo nipo F5, boarding, nkatoloka. Maisha ya kuaa ndani huku ulikuwa dei,hayakuwa sawa. Kukawa na mshikaji nilisoma nae, kumbe kwao kuna rubisi,kali af tamu balaa. Nikanywa weeee,kumbe moshi unapanda mi sielewi. Njia ya kwenda kwao,kuepuka kukutana na mtu,ni sehemu ya kufugia ng'ombe wa maziwa,pamezinguushiwa senyenge.
Kukawa na maembe sasa. Ile narudi mida ya saa moja,mi naenda tu,nikasema niwapelekee washikaji hata maembe. Nkacuma,badhi yameiva,mengine mabichi na machanga humo humo.
Cha kubebea,hamna! Kuvua tu shati. Litafuliwa litakate,hapo sikuwa naelewa. Kuna mitalo ya maji humo balaa. Nikikanyaga, muguu huo,umezama. Hatua chache mbele,mzima mzima.
Naangalia sehemu ya kutokea,siioni. Maembe hapo yanamwagika na kupungua tu. Suruali na viatu,wewenyewe jiulize. Nilibahatika kukatiza barabara,nikaenda. Sikupita getini,nilipita njia za panya.
Mi sinajua naenda kwa majama,af ndo ilikuwa mara yangu ya kwanza kulewa sasa. Maembe yalobaki hayazidi hata 10.
Nimepita nkaingia darasani hapo ni mda wa kujisomea. Kumbe,kuna mwarimu hapo alikuwa amekuja kusaidia kurudia,kakaa kwenye viti vya wanafunzi. Naingia na maembe na suruali na viatu vimelowa, dah! Fedheha ya maisha nilopata nadhani ni ile tu. Nikatonywa,mi sielewi. Nadhani ile kutembea iliongeza wenge.
Maembe sikumpa mtu,nikaweka tu juu ya dawati.
Nashuka kuelekea bwenini, dah! Nkapoteza ramani mazima.
Kesho yake sasa, ndo naitwa na kupewa off siku 7,na kurudi na mzazi.
*****, naanzaje sasa! Khah!!!!!! Acha tu niishie hapa
2. Tukio la pili,nikiwa nasoma kama darasa la 2 au la tatu,acha niende kuiba asali🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣. Aiseee!
Nikatafuta mti mrefu,nkapata. Kuna mizinga ilikuwa karibu na kwetu ya jirani. Mi sijui asali ntapata au sipat. Na lengo likawa tu nitoe kifuniko cha mzinga(ile mikubwa ya zamani), kweli kikadondoka. Kuangalia,nkaona hapa ntashambuliwa. Akili za kitoto bwana. Nikajisemea ngoja tu nichovye na kile kijiti. Hata basi nililamba! Kilichonikuta sitokaa nisahau. Ila nachojua karibia mtaa mzima walisikia kilio na kuwahi. Kila sehemu ya mwili,nilidungwa. Baada ya mda sasa,mwili mzima unawaka moto, mdomo unapima kama kilo 10.