Share nasi matukio yako ya ukuaji

Share nasi matukio yako ya ukuaji

Dah hatari sana .
Mpende sana mama lakini nahisi sasa umebadilika maana hamkawii nyie watu wa hivi tukikutana bar mnatutegeshea tunaenda maliwato mnakojolea kwenye vinywaji vyetu

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Mama bahati mbaya alifariki, ila Vitu ambavyo namwomba Mungu mbegu zetu hizi zinazoonekana kupitia kwa Mke wangu zisinisumbue kama mimi nilivyokuwa msumbufu.... Hahahahah.. nakumbuka wakati tupo kwenye kuhangaika kwenye maisha kuna jamaa alivamia Pombe za bure kwenye sherehe aisee kalewa chakari, tukanunua mayai ukakoroga na unga wa ngano kidogo aisee tukammwagia jamaa kwenye suruali hahahahahaha. Mwamba alivyoaamka akasema hadi luisMkinga mwanangu hujanitetea.. aisee nilicheka kinoma kuamini tulimwonyesha video yake wakati tunafanya hivyo vituko.
 
Nikiwa primary school nilikuwa mpole na mkimya sana hali iliyopelekea kupendwa sana na baadhi ya walimu, ilifikia hatua nikawa miongoni mwa wanafunzi wanaoachwa kuadhibiwa hata likiadhibiwa darasa zima( wengine wanaachwa kwa sababu mbalimbali kama za kiafya). Darasa la 5 akahamia mwl mmoja wakike ana mwanae wakwanza wakiume mwenye jina kama langu, alikuwa mkali sana ila hakuwai kunipiga kabisa alikuwa ananipenda kwa sababu n mtulivu na nna jina kama la mwanae.

Nikawa siadhibiwi kazi yangu ni kuleta fimbo nzuri kwa ajili ya kuadhibu wengine na kwa akili za kitoto na nilivyokuwa mtiifu kufuata maelekezo nilikuwa naleta fimbo nzuri kweli kweli. Nilikuwa na chimbo langu mtoni kwenye mti mmoja ulikuwa umenyooka haswa na fimbo zake hazivunjiki haraka.

Hii ikanijengea chuki kwa baadhi ya wanafunzi wenzangu na ukizingatia mimi huwa siadhibiwi.
Usiku mmoja nimelala nikaota nimefuata fimbo kama kawaida, kabla sijafika kwenye ule mti nikaona mzuka/mzimu unatisha umevalia mavazi meupe juu mpaka chini, nikasita kuendelea nikaanza kurudi nyuma, ghafla ukaanza kunifuata na kunifukuza ile nageuka ili nikimbie vizuri nikashtuka usingizini.

Alooh kuanzia ile siku nilikoma kwenda kufuata fimbo kwenye ule mti, nikawa nachukia ile kazi kadri siku zilivyosogea nikawa napeleka vifimbo vya hovyo na mwshowe nikaambiwa naona kazi imekushinda, akapewa mtu mwingine. Ile ndoto kuna namna ilikuwa na ujumbe maana ilinitisha kweli kweli.
Umetisha mkuu,hiyo story yako ya primary ni kama mimi tu,nilikuwa mpole sana hata wachapwe darasa Zima mi nlikuwa sichapwi,nilikuwa napangiwa tu kufanya usafi ofisi za walimu.
 
Kuna mtaa wa msisiri kinondoni pembeni kuna soko kubwa tu.
Soko lipo katikati ya mitaa mingi ila upande wa tulipo kuwa tunakaa kabla hujafik ndanindan unakutans na butcher safi tu kipind hiko.

Ilikuwa jioni tupo sokoni sijui tulifata nini kushangaa shangaa me nilikuwa nachezea zipu y kibukta changu cha jeans na zipu ya chuma si kigovinda changu kikanasa kwenye zipu

Nilitoa kilio sitokuj sahau soko lote likaja kwangu yule mwenye butcher alivyo kuja akasema kama ni govinda basi wanitahiri pale pale alooooo nilipiga yowe mpk wakanibeba kunipeleka home ndy kwenda kutolewa.

Nilitahiriwa week after hilo tukio mana walisema tushapata sababu nzuri ya kukukata.
 
Shuleni nilikua mkimya na mtulivu sana kiasi kwamba asilimia kubwa ya wanafunzi wenzangu walijua sisikii vizuri, kwasababu sikua na desturi ya kuongea hata kama ukiniuliza kitu labda tuwe tuna fahamiana

Basi bhana nikawa napendwa sana na mademu pamoja na walimu , nikawa natolewa mifano hadi pared kwa utulivu na kujipenda kwangu hususani na dalasan sikua vibaya Sana nikawa najipakualia minyama Tu.

Siku moja mwalimu wa fildi alikua anatoa somo class sasa mi nilikua nimekaa na manzi mmoja anaongea sauti ya chini huku pindi lina endelea , akaongea neno nika tabasamu ticha akaniona nakuniita mbele kwa ghadhabu huku akisema Mimi nafundisha wewe unanicheka shika chini hapo.

Hapo nika sita na kusema mwalimu mimi sija cheka umeniona nikitabasamu mwalimu akagoma na kuniforce niadhibiwe aloooh dalasa zima likainuka na kupinga Mimi kuazibiwa .
 
Daaah nimekumbuka mbali sana. Enzi ya asante Mkapa, RIP Big Benji, nikiwa darasa la pili nilikua napenda sana kwenda vibanda umiza vile vilikuwa vinaonyesha movies. Sasa ratiba ilikua hivi asubuhi mpaka sa6 mchana ni picha za kihindi huwa ni ndefu hivyo huwa mbili tu, sa7 picha za kibongo hadi sa10 au kizungu inategemea, sa10 hadi sa1 usiku ya kihindi ya kumalizia siku. Baada ya hapo watu hutawanyika lakini kwenye ule ubao wa kuwekea makava ya muvi nilikua nasoma kwa chini kila siku wanaandika leo usiku kutakuwa na pilau. Sasa nafikiri ni curiosity na utoto wa kutojua pilau ni nini? Siku moja nikasema leo siondoki, baada ya picha ya kihindi ya jioni kuisha nitasubiri mpaka na mimi leo nile hilo pilau nikidhani ni msosi. Sasa binamu zangu ambao tulikuwa na umri sawa wakati wanaondoka bandani baada ya picha ya kihindi nikawa nawashawishi tubaki wote tule pilau wakasema watoto hawaruhusiwi sikukata tamaa, nyuma ya lile banda kuna matobo yalikuwepo ambayo unaweza kuona ndani, nikasema nitajibanza kwa nyuma ya banda hadi mda wa pilau ufike wakipakua nitaenda na hakuna atakayenifukuza(masikini ningejua ningeondoka na binamu zangu).
Basi muda ukafika nikastaajabu kuona wake kwa waume, wababa kwa wamama, na mabraza na masista du wa mtaani wanaingia bandani, hapo ishafika saa4 usiku, laahula VHS ikafunguliwa wakatia mkanda wa tofali daaah nilichokiona (ilikua siku yangu ya kwanza kucheki porno) na kwa kuwa nilikua nachungulia toka nyuma ya banda nikawa naona na wale waliokaa nyuma walichokuwa wanafanya ni laana.
Sasa bana msala ulianza pale lile zoezi la pilau lilipoisha nisijue ishakua sa6 usiku na nimeshatafutwa kinyama bila mafanikio, na binamu zangu walipoulizwa wakasema nilikua nasubiri pilau, wewe sikia tu kama sikuzimia siku hii kutokana na kipigo sitazimia tena mshua alinidunda kama anaua nyoka.
Sasa nilipokua naulizwa umekula wapi pilau? Mimi kimya. Hapa nyumbani hauli? Mimi kimya. Mama anadakia huyo jeuri unaona hajibu, asijue ni mambo ya ajabu nimetoka kutazama nashindwa hata kuyaelezea. Siwezi sahau hii siku asubuhi nilipelekwa hospitali baada ya kupata homa kali na vijipu sababu ya kipigo.

Uliona nini kule nyuma kaka
 
1____uharibifu mali ya umma mtaani kulikuwa na bomba la kupump Danida ni bomba lilikuwa linatumika kijiji kizima,

,usiku mida ya saa mbili tulipangana na rafiki yangu tukaharibu bomba, tulifanikiwa kulifungua lilifyatuka pira ni refu hatari,tulifungua na kuvuta pira asubuhi wananchi wanashangaa bomba pira lipo nje limeharibika kaharibu nani hawajui

Na halikutengenezwa hadi leo maana ni gharama ,nikilionaga nacheka, tulifanyaga siri, tungegundulika tungepewa adhabu kali mno na serikali.


2____Wizi nilikuwa na marafiki zangu wawili tukavamia shamba la viazi la watu,viazi vilikuwa havijakomaa, tuling'oana nusu shamba,

Kumbe mwenyewe yupo ng'ambo anagomba kuwa tuache kuharibu viazi vyake,sie tupo bize,

Usiku nimetulia home nasikia hodi,mmama mwenye viazi kaja kunichukua yupo na wale waizi wenzangu,

Akatupeleka shamba akatuambia tukusanye mbegu zote,tulikusanya kila mmoja na mbegu zake na kila mmoja akaenda kutukabidhi kwa wazazi wetu na zile mbegu tupanda then tumpelekee viazi,

Baba(ra) alinikamata nikajifanya kumponyoka kukimbia alinikimbiza alivyonikamata alinipiga vibaya mno, hii ilikuwa ni mara ya kwanza na mwisho kupigwa na baba,


3___Kupigwa na wavulana

Home kulikuwa kuna duka,sasa wakija dukani kununua vitu nawachokoza then nakimbilia ndani, siku hiyo nimetania na mama yupo nikajua mama atanitetea, tania kimbilia ndani mama akanitoa kunikabidhi kwa mvulana kuwa anipige,tukadundana nilivyoona vinanishinda nikajizimisha mama alivurugwa,


4____kupigana na mvulana huyu nilikuwa namtania Jose likichwa siku akanifuma njiani na kuniambia tania kama unavyotaniaga ukiwa kwenu, nilikaa kimya,akaanza kunipiga mwenyewe sio mnyonge tulipigana akaniangusha chini,nikalala kujifanya nimezimia, pembeni kulikuwa na betri mbovu zile kubwa za tochi, niliokota nikampiga nayo jichoni na kukimbia, baba alimtibiaga, hadi leo yule mkaka ana alama isiyofutika jichoni,

5___kufungulia bomba usiku maji ya mwagike,

Ni uwanjani wa umma kuliwekwa bomba la koki na walikuwa wanafunga na boksi na kufuri, mie na group langu tulikuwa tuna vizia mida ya jioni hivi tunaenda penyeza vidole tunafungulia maji yanamwagika usiku kucha,



Kiufupi tu,nilikuwa mkorofi,muharibifu kufungua vitu na kuvitengeneza tena, Baba alikuwa ananiita jike dume

Ahsante mama kwa kunipambania,maana bila fimbo/ukali wa mama sijui ningekuwaje

Kweli we kikorofi
 
Sasa nimeelewa kwanini unapenda matumizi ya fake ID, kumbe toka mtoto ulipenda kujificha 😂
Yani izo ndo zangu za kujificha Sasa Kivumbi ule mchezo wa kuchezesha vikopo mara vichupa Tena sipend mtu aje niwe pekeyangu,moja had lilinikata mguuni Nina alama Hadi Leo nilishonwa mzee kagoma had akaona aache tu😃😃😃
Kupika Sasa wee hunitoi, Mimi ndo mpishi mkuu sikumoja tukapika tukaenda kuiba malimao ya kachumbari mm ndo mpandaji juu acha nitobolewe na miba kwenye goti nililiavkimya kimya maana wenyew wangesikia 😂😂😂😂nikapata kidonda kikubwa 😂😂😂😂
 
Du hii balaa aisee!
1. Je, alizeti ilikuwa ya kula hadi ukawanyima wenzako? Kuna mahali fulani niliona watoto walikuwa wanakaanga alizeti. Mlikuwa mnakaanga mnakula?

2. Pole kwa kukatishwa mgegedo. Ina maana mama alipoondoka hukupata tena genye za kuendelea kugegeda? Hahahaha!

Back to story sharing................
Kipindi nikiwa shule ya msingi, tulikuwa na ujinga wa kujificha juu ya miti. Tuliamini kwamba mtu ukipanda juu ya mti aliye chini hakuoni. Utoto bhana!

Sasa siku moja mimi na mwenzangu tukajificha juu ya mti ili kukwepa kuonekana kwa walimu. Kumbe mti tuliojificha upo mbali na mahali alipokuwa mwalimu mkuu akiwapa adhabu wanafunzi wenzetu (huku tumevaa mashati meupe). Eeh bwane ehh, kumbe mtu akiwa mbali na miti anakuona vizuri tu aisee!

Basi mwalimu alipotuona akamtuma mwanafunzi mmoja mkubwa atufuate. Ile kushtuka huyu hapa! Tukashuka harakaharaka tukataka kukimbia lakini tukajua hata tukimbie hatuwezi kufua dafu. Sanasana tutakuwa tunajiongezea idadi ya makosa. Na huyo mwalimu aliyemtuma kutushusha hana masikhara aisee. Tukaone isiwe taabu tukajisalimisha tukakamatwa mateka akatupeleka kwa mwalimu.

Siku hiyo tulikula fimbo kidogo nijikojolee. Tangu siku hiyo tukaona tena kupanda kwenye miti hakutusaidii. Tukawa wanafunzi watiifu hadi tulipohitimu shule.

Utoto raha sana aisee!

Haha pole mkuu
 
Wakati nikiwa chalii, kwa mtoto wa kiume kuwa na m.avuzi ilikuwa dili sana, ila Mimi na mdogo wangu hatukuwa nayo.

Sasa kwenye kupiga story kitaa, wadau wakawa wanasema ukikojoa kwenye jiko asubuhi utaamka na msitu wa kufa mtu. Usiku baada ya kula, tukavizia wengine wameenda kulala, Mimi na dogo tukaenda kukojolea jiko.

Asubuhi palivyokucha kabla hata hatujapata muda wa kujikagua m.avuzi kama yameota au la, tuliamshwa na Mshua. Ile ndio ilikuwa mara ya kwanza kuiona bad side ya Mshua.

Ofcourse alinipatia somo pia, kwamba m.avuzi yanaambatana na maumivu. Tokea yameota rasmi, shida haziishi, majukumu yanazidi n.k

Manina wewe
 
Kuna mtaa wa msisiri kinondoni pembeni kuna soko kubwa tu.
Soko lipo katikati ya mitaa mingi ila upande wa tulipo kuwa tunakaa kabla hujafik ndanindan unakutans na butcher safi tu kipind hiko.

Ilikuwa jioni tupo sokoni sijui tulifata nini kushangaa shangaa me nilikuwa nachezea zipu y kibukta changu cha jeans na zipu ya chuma si kigovinda changu kikanasa kwenye zipu

Nilitoa kilio sitokuj sahau soko lote likaja kwangu yule mwenye butcher alivyo kuja akasema kama ni govinda basi wanitahiri pale pale alooooo nilipiga yowe mpk wakanibeba kunipeleka home ndy kwenda kutolewa.

Nilitahiriwa week after hilo tukio mana walisema tushapata sababu nzuri ya kukukata.
😂😂😂😂
 
Wakati nikiwa chalii, kwa mtoto wa kiume kuwa na m.avuzi ilikuwa dili sana, ila Mimi na mdogo wangu hatukuwa nayo.

Sasa kwenye kupiga story kitaa, wadau wakawa wanasema ukikojoa kwenye jiko asubuhi utaamka na msitu wa kufa mtu. Usiku baada ya kula, tukavizia wengine wameenda kulala, Mimi na dogo tukaenda kukojolea jiko.

Asubuhi palivyokucha kabla hata hatujapata muda wa kujikagua m.avuzi kama yameota au la, tuliamshwa na Mshua. Ile ndio ilikuwa mara ya kwanza kuiona bad side ya Mshua.

Ofcourse alinipatia somo pia, kwamba m.avuzi yanaambatana na maumivu. Tokea yameota rasmi, shida haziishi, majukumu yanazidi n.k
😂😂😂
 
Yani izo ndo zangu za kujificha Sasa Kivumbi ule mchezo wa kuchezesha vikopo mara vichupa Tena sipend mtu aje niwe pekeyangu,moja had lilinikata mguuni Nina alama Hadi Leo nilishonwa mzee kagoma had akaona aache tu😃😃😃
Kupika Sasa wee hunitoi, Mimi ndo mpishi mkuu sikumoja tukapika tukaenda kuiba malimao ya kachumbari mm ndo mpandaji juu acha nitobolewe na miba kwenye goti nililiavkimya kimya maana wenyew wangesikia 😂😂😂😂nikapata kidonda kikubwa 😂😂😂😂
Pole ulikuwa na heka heka nyingi kuliko umri umri wako. Hapo kwenye kupika itabidi ufanye namna nile pishi lako maana kwenye comment tu chakula n kitamu sijui uhalisia itakuwaje.
 
Umetisha mkuu,hiyo story yako ya primary ni kama mimi tu,nilikuwa mpole sana hata wachapwe darasa Zima mi nlikuwa sichapwi,nilikuwa napangiwa tu kufanya usafi ofisi za walimu.
Jina lako linasadifu uyasemayo na uhalisia wako, bado ni mpole au ndio ushafunguliwa dunia kuwa unachotaka?
 
Kipindi Cha utoto nilikuwa najiuliza jiko la mafuta linawashwa kwa juu ambazo ndo Kuna zile tambi zake Sasa kwanini tusiwashe kwa chini ambapo Kuna mafuta na tambi zilipoanzia labda Moto utapanda juu na kuendelea kuwaka Kama kawaida
Basi siku moja nikachukua kiberiti nikafungua lile bakuli lake ambako Kuna mafuta na tambi zake nikawasha kile kiberiti na kutumbukiza Kisha kufunika nikisubiri Moto uwake juu ya tambi lahaula tofauti na nilivyotegemea Moto ulishika Kasi jiko lote liliwaka na bado kidogo niunguze nyumba biLA ya msaada ya majirani
 
Back
Top Bottom