Darasa la nne lilikua na uhaba wa dawati, tukaitwa mbele wote, mwalimu akaanza kupanga moja moja mpaka dawati lijae, bahati mbaya mimi nikawa wa mwisho nikaambiwa nitafute dawati lolote nikae, hapo kila dawati lina wanafunzi wa tano, kila ninapoenda nakataliwa , niliumia sana ila kwa vile nilikua mnyonge tokea chekechea sikujali sana, mwalimu alilazimisha nikae kwenye dawati la wanafunzi wembamba hivyo rukwa sita ila mimi nilikua nakaa upande.
Wiki ile ikaisha nikapata wazo , mpaka darasa la nne liishe nitateseka sana , jumapili kanisa letu lilikua karibu na shule, ibada yetu watoto ilikua ibada ya pili , niliwahi asubuhi sana nikaenda shuleni, nikaenda kuchukua dawati darasa la kwanza nikaleta darasa la nne nikaliweka nyuma kabisa.
Jumatatu ikafika japo nina wasi wasi lakini niko nafurahia kukaa dawati nzima peke yangu!
Sikuulizwa ila mpaka natoka darasa la nne nilikua nakaa kwa ku enjoy sana.