Shaka: Wanaotaka Urais 2025 wasahau, ni Rais Samia bara ni Rais Mwinyi visiwani mpaka 2030

Utamaduni huwa unabadilika kulingana na uhitaji wa nyakati. CCM inapigia debe utamaduni huu lakini ipo siku utawatokea puani.

Suppose wamechagua mgombea lakini kwenye angu yake ya kwanza akaonekana ameshindwa kazi, je atavumiliwa mpaka miaka 10 iishe?

Leo yupo SSH tunasifia kesho hatujui ataletwa nani.
Utamaduni wa kishenzi. Huyo shaka sio Great Thinker na wala Alichoongea sio Fikra Tunduizi. Hapa tuna Makabila ambayo yalikuwa na utamaduni kutahiri wanawake. Ni kwa nini leo huo utamaduni unanangwa? Watu wenye akili hawapingi utamaduni huo bali kwa mazingira ya sasa ya Dunia wanahitaji Kiongozi mwenye maono. Huyo anayemshabikia anapondwa hata na watoto wadogo mitaani. Mambo ya kutueleza eti ndio maana aliweza kuchaguliwa Makamu wa Raisi wakati ule hiyo sio sababu ya kuthibitisha uwezo wake. Umakamu wa Raisi ni Uteuzi na sio Uchaguzi. Aende akawasome akina Martha Kalua huko Kenya. Hao ndio Wenye Bongo za kuweza kuongoza Taifa.
 
2025 hatutaki mtu zaidi ya Rais Samia Suluhu Hassan,

Kazi anazofanya huyu Mama hapa Upinzani kuweka mtu ni kujipotezea gharama bure kabisa,
Huu ndo ujinga unaodumaza nchi. Kwanza kazi gani hiyo? Wengine hawawezi kufanya? Kama Taifa tunahitaji kujaribu chama kingine na brain zingine. Siyo kila mwaka akina Lukuvi tu.
 
Hebu Shaka kama kweli anaamini huyo Mamake Ni Kiongozi bora ni kwa nini Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi kachagua kwenda Uganda badala ya Tanzania? Kenya hajaenda kwa sababu wao ni Pro-America kwenye Vita ya Ukraini. Lakini ukiwatoa hao kwa East Africa, Tanzania ndio ilitakiwa ipewe hiyo nafasi aliyopwa Mseveni. Russia inafahamu mchango wa Tanzania katika kujiachanisha na Makucha ya Ukoloni na Ubeberu. Sasa angalia Mrusi kaishia Uganda. Maana yake ni nini? Maana yake wenzetu huko Duniani wanajua Kiongozi wa Nchi Kichwani na sio Formality. Kama hilo halijitoshelezi kutuonyesha kuwa huko Duniani wanatuona hatuna kichwa cha Uraisi basi sisi ni Vilema wa Kufikiri.
 
Utamaduni huwa unabadilika kulingana na uhitaji wa nyakati. CCM inapigia debe utamaduni huu lakini ipo siku utawatokea puani.

Suppose wamechagua mgombea lakini kwenye angu yake ya kwanza akaonekana ameshindwa kazi, je atavumiliwa mpaka miaka 10 iishe?

Leo yupo SSH tunasifia kesho hatujui ataletwa nani.
Mjomba kwa nchi ila akae nani pale atasifiwa na kupambwa tuu maana ccm huwezi kuona mabaya kabisa na ukiona mabaya utakosa teuzi
 
Maadui wakubwa wa waafrika ni viongozi wao
Nahisi ni watu wenyewe tuu haiwezekani Africa nzima tuwe na viongozi wabovu kwani huwa tunawakodi nje? wanawakilisha tabia zetu tulivyo tuu maana yakifanyika ya hovyo tunakaa kimya tuu
 
hatutaki mtu anayeipoza nchi kama huyu aliyepo sasa, yaani nchi imepoa imelala fofofo..wapigaji wanajitokeza kila siku na vikauli vya hovyo kama hivi. Tunaomboleza kufiwa bado mijitu mingine inatuamshia maumivu mapya. Bora watulie hivyohivyo hadi 2025, tutaonyeshana uhalisia :cool:
 
Mtu kama Shaka au Kinana hawawezi kutoa Kauli Juu ya Uongozi wakaaminika. Kila Mtanzania anajua huyo Kinana marehemu Magufuli alikuwa ameishia naye wapi. Na Shaka tunafahamu Marehemu Magufuli alikuwa amempiga Pini kwa Tuhuma za Rushwa.
 
View attachment 2322973
Katibu wa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema hakuna shaka Rais Samia Suluhu Hassan ataendelea kuwavusha watanzania hadi 2030 kutoka na uwezo mkubwa uliounesha katika uongozi na utendaji uliotukuka.

Akizungumza katika kongamano maalum la kumpongea Rais Samia huko Unguja hii leo, Shaka amesema Rais Samia pamoja na Rais Dkt. Hussein Mwinyi ni viongozi shupavu walioonesha ari kubwa kuwatumikia watanzania.

Shaka amesisitiza kutokana na kazi nzuri ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 inatoa uhalali kwao kuendelea kuiongoza nchi yetu panapo kudra za Mwenyezi Mungu mpaka 2030 ikiwa pia ni utii wa katiba ya CCM, kanuni na utamaduni tuliojiwekea.

Aidha, Shaka amesema wale wenye ndoto ya Urais 2025 kwa bara na visiwani wasahau kwakuwa CCM inamila, katiba,desturi ,Utaratibu na miongozo mbalimbali zinazotawala muda wa Rais kudhaminiwa na Chama cha Mapinduzi.

===
Mlimpamba mwendazake vivi hivi hatimaye Mungu akaamua ugomvi ,
Acheni uchuro wa kuwaza uchaguzi miaka3 ijayo ni upuuzi mkubwa wazeni Ni jinsi gani mtapambana kuimarisha uchumi na kutatua cgangamoto mbalimbali zinazowakabili waTanzania
 
Huu Ugomvi Wa Form Bila Shaka Mnaleta Uchuro Ndani Ya Chama
Mungu Ataamua Huu Ugomvi Kama Wakati Wa Mzilankende Mnyago
 
Muda Ukifika Ndani Ya Ccm Kutawaka Moto Mkubwa Sana
Mtu kama Shaka au Kinana hawawezi kutoa Kauli Juu ya Uongozi wakaaminika. Kila Mtanzania anajua huyo Kinana marehemu Magufuli alikuwa ameishia naye wapi. Na Shaka tunafahamu Marehemu Magufuli alikuwa amempiga Pini kwa Tuhuma za Rushwa.
 
Mlimpamba mwendazake vivi hivi hatimaye Mungu akaamua ugomvi ,
Acheni uchuro wa kuwaza uchaguzi miaka3 ijayo ni upuuzi mkubwa wazeni Ni jinsi gani mtapambana kuimarisha uchumi na kutatua cgangamoto mbalimbali zinazowakabili waTanzania
Hovyo kabisa hao Jamaa. Nchi ina Changamoto ya Bei ya Mafuta na hoja hiyo badala ya kujibiwa maelezo yanayopita Mzingo wa Mashaka wao wanakuja kutueleza mambo ya uchaguzi ambao Ni wa 2025! Hizi Ni Akili au matope?
 
Muda Ukifika Ndani Ya Ccm Kutawaka Moto Mkubwa Sana
Itapendeza kama kweli watajitokeza majasiri kama hao. Ni lazima ili huo ujinga wa kupangisha watu Uongozi wa Nchi ukomeshwe watokeze watu majasiri ambao hawaogopi kupoteza maslahi yao.
 
Back
Top Bottom