Shaka: Wanaotaka Urais 2025 wasahau, ni Rais Samia bara ni Rais Mwinyi visiwani mpaka 2030

CM 1774858

JF-Expert Member
May 29, 2021
4,277
3,103

Katibu wa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema hakuna shaka Rais Samia Suluhu Hassan ataendelea kuwavusha watanzania hadi 2030 kutoka na uwezo mkubwa uliounesha katika uongozi na utendaji uliotukuka. Akizungumza katika kongamano maalum la kumpongeza Rais Samia huko Unguja leo hii, Shaka amesema Rais Samia pamoja na Rais Dkt. Hussein Mwinyi ni viongozi shupavu walioonesha ari kubwa ya kuwatumikia watanzania.

Shaka amesisitiza kutokana na kazi nzuri ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025, inatoa uhalali kwao kuendelea kuiongoza nchi yetu panapo kudra za mwenyezi Mungu mpaka 2030. Ikiwa pia ni utii wa katiba ya CCM, kanuni na utamaduni tuliojiwekea.

Aidha, Shaka amesema wale wenye ndoto ya Urais 2025 kwa bara na visiwani wasahau kwakuwa CCM inamila, katiba, desturi, utaratibu na miongozo mbalimbali zinazotawala muda wa Rais kudhaminiwa na Chama cha Mapinduzi.

===
 

TrioNeTwork

Senior Member
Aug 7, 2022
109
104
View attachment 2322973
Katibu wa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema hakuna shaka Rais Samia Suluhu Hassan ataendelea kuwavusha watanzania hadi 2030 kutoka na uwezo mkubwa uliounesha katika uongozi na utendaji uliotukuk...
2025 hatutaki mtu zaidi ya Rais Samia Suluhu Hassan,

Kazi anazofanya huyu Mama hapa Upinzani kuweka mtu ni kujipotezea gharama bure kabisa,
 

katitu

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
1,739
1,311
View attachment 2322973
Katibu wa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema hakuna shaka Rais Samia Suluhu Hassan ataendelea kuwavusha watanzania hadi 2030 kutoka na uwezo mkubwa uliounesha katika uongozi na utendaji uliotukuka.

Akizungumza katika kongamano maalum la kumpongea Rais Samia huko Unguja hii leo, Shaka amesema Rais Samia pamoja na Rais Dkt. Hussein Mwinyi ni viongozi shupavu walioonesha ari kubwa kuwatumikia watanzania.

Shaka amesisitiza kutokana na kazi nzuri ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 inatoa uhalali kwao kuendelea kuiongoza nchi yetu panapo kudra za Mwenyezi Mungu mpaka 2030 ikiwa pia ni utii wa katiba ya CCM, kanuni na utamaduni tuliojiwekea.

Aidha, Shaka amesema wale wenye ndoto ya Urais 2025 kwa bara na visiwani wasahau kwakuwa CCM inamila, katiba,desturi ,Utaratibu na miongozo mbalimbali zinazotawala muda wa Rais kudhaminiwa na Chama cha Mapinduzi.

===
Unajua huyu jamaa kafirisika kichwani kwa yeye ndo anatuchagulia rais au ni sisi watanzania
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

12 Reactions
Reply
Top Bottom