Shaka: Wanaotaka Urais 2025 wasahau, ni Rais Samia bara ni Rais Mwinyi visiwani mpaka 2030

Haijaandikwa popote, Kwa Katiba ya CCM Wala ya nchi.

Kamati kuu iliweka ustaarabu na desturi hiyo Kwa mgombea urais aliyepitishwa na chama term ya kwanza.

Huyu hajawahi pitishwa na kamati kama mgombea urais Bali kama Makamo.

Hivyo watu waruhusiwe kuchukua fomu, apitaye na apite.
Mkuu, hapo umenena na nakubaliana na hoja yako kabisa vinginevyo wamekalili nguvu ya upinzani iko wapi lakini pia ni kikali kuwa ukishapitishwa na Chama, basi ushindi lazima vinginevyo nikujifariji tu.
Nami nasema nafasi hiyo igombewe na wanaohitaji badala ya kutaka kuminya nafasi hiyo.
 
Kwakuwa maamuzi ni ya mkutano mkuu kumpitisha mgombea,basi kiongozi shaka asubili muda na wakati utakapotimia na afahamu hakuna mkutano mkuu uliowahi kumpitisha Rais Samia kugombea nafasi hiyo bali ameupata kwa kudra za Mungu kama alivyowahi kunena mwenyewe.binafsi naona kuna haja ya nafasi hiyo ya urais, chama kuruhusu wanachama wake kugombea kama ilivyokuwa kwa marais waliopita na wala hakujawahi kuwa na utamaduni,mila,desturi,taratibu,kanuni,sheria au katiba yenyewe ndani ya Ccm inayoeleza juu ya taratibu za kugombea nafasi hiyo nyeti ndani ya nchi endapo tu Rais aliyeko madarakani atarithi nafasi hiyo kutoka nafasi aliyepo tofauti na hivyo Shaka aeleze ni wapi pameandikwa utaratibu huo alioutaja.
Naamini muda ukiwadia,wapo wanachama watajitokeza kumpokea Rais Samia kijiti vinginevyo itolewe fomu moja kama ilivyowahi kutokea nyakati za nyuma jambo ambalo si demokrasia wala afya kwa chama.
2025 ccm tutatumia busara ya kuprint fomu moja kwa ajili ya Samia, na mkutano mkuu utampitisha Samia kwa kishindo.
 
Naona unampigia chapuo, binafsi nitamfanyia tathimini baadaya yakukaa madaraka miaka miwili,lakini hadi sasa,mm kama mdau,sioni kama anafaa kuendelea kupewa nafasi hiyo ya uraisi ifikapo 2025 vinginevyo kuwe na mwelekeo mpya.
Nasubili miaka miwili ifike.
2025 ccm tutatumia busara ya kuprint fomu moja kwa ajili ya Samia, na mkutano mkuu utampitisha Samia kwa kishindo.
 
Hata wakati wa mwendazake mlisema hivyo hivyo ila 2020 moto ukawaka mpaka akatumia polisi,tiss na tume kujitangazia ushindi wa kishindo.

Waamuzi wa kumuajiri rais ni wananchi lakini kwa makusudi watanzania wameporwa haki hiyo. Tutakuja kuelewana tu mbele ya safari.
 
View attachment 2322973
Katibu wa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema hakuna shaka Rais Samia Suluhu Hassan ataendelea kuwavusha watanzania hadi 2030 kutoka na uwezo mkubwa uliounesha katika uongozi na utendaji uliotukuka.

Akizungumza katika kongamano maalum la kumpongea Rais Samia huko Unguja hii leo, Shaka amesema Rais Samia pamoja na Rais Dkt. Hussein Mwinyi ni viongozi shupavu walioonesha ari kubwa kuwatumikia watanzania.

Shaka amesisitiza kutokana na kazi nzuri ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 inatoa uhalali kwao kuendelea kuiongoza nchi yetu panapo kudra za Mwenyezi Mungu mpaka 2030 ikiwa pia ni utii wa katiba ya CCM, kanuni na utamaduni tuliojiwekea.

Aidha, Shaka amesema wale wenye ndoto ya Urais 2025 kwa bara na visiwani wasahau kwakuwa CCM inamila, katiba,desturi ,Utaratibu na miongozo mbalimbali zinazotawala muda wa Rais kudhaminiwa na Chama cha Mapinduzi.

===
2025 Mama hanampinzani amebeba matumaini ya wengi, ndani ya mwaka mmoja amejenga madarasa 15000, amejenga vituo vya afya vijijini na miji midogo, amefanya kazi ya miaka 5 ndani ya mwaka mmoja na anaendelea kufanya
 
View attachment 2322973
Katibu wa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema hakuna shaka Rais Samia Suluhu Hassan ataendelea kuwavusha watanzania hadi 2030 kutoka na uwezo mkubwa uliounesha katika uongozi na utendaji uliotukuka.

Akizungumza katika kongamano maalum la kumpongea Rais Samia huko Unguja hii leo, Shaka amesema Rais Samia pamoja na Rais Dkt. Hussein Mwinyi ni viongozi shupavu walioonesha ari kubwa kuwatumikia watanzania.

Shaka amesisitiza kutokana na kazi nzuri ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 inatoa uhalali kwao kuendelea kuiongoza nchi yetu panapo kudra za Mwenyezi Mungu mpaka 2030 ikiwa pia ni utii wa katiba ya CCM, kanuni na utamaduni tuliojiwekea.

Aidha, Shaka amesema wale wenye ndoto ya Urais 2025 kwa bara na visiwani wasahau kwakuwa CCM inamila, katiba,desturi ,Utaratibu na miongozo mbalimbali zinazotawala muda wa Rais kudhaminiwa na Chama cha Mapinduzi.

===
Maneno yenye hekima na ndio ukweli huo.
 
Kweli umelambishwa. Huoni kinachoendelea hapo jirani uchaguzi uliopita.
Huu ujinga unafanya wenye tume wanyanyase sana wagombea wengine.
KATIBA MPYA na Tune huru tunataka Haki na ukweli.
 
Maneno yenye hekima na ndio ukweli huo.
Hata hayati JPM tulifanya hivo hivi hata wengine walidhiriki kumfananisha na Muumba na alikuwa atawale maisha ila mwenye haki alifanya aaliyoona yeye. ! Punguzeni sifa na kumpamba huwez kujua wako wanapata tabu na Muumba anawajali pia.
 
View attachment 2322973
Katibu wa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema hakuna shaka Rais Samia Suluhu Hassan ataendelea kuwavusha watanzania hadi 2030 kutoka na uwezo mkubwa uliounesha katika uongozi na utendaji uliotukuka.

Akizungumza katika kongamano maalum la kumpongea Rais Samia huko Unguja hii leo, Shaka amesema Rais Samia pamoja na Rais Dkt. Hussein Mwinyi ni viongozi shupavu walioonesha ari kubwa kuwatumikia watanzania.

Shaka amesisitiza kutokana na kazi nzuri ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 inatoa uhalali kwao kuendelea kuiongoza nchi yetu panapo kudra za Mwenyezi Mungu mpaka 2030 ikiwa pia ni utii wa katiba ya CCM, kanuni na utamaduni tuliojiwekea.

Aidha, Shaka amesema wale wenye ndoto ya Urais 2025 kwa bara na visiwani wasahau kwakuwa CCM inamila, katiba,desturi ,Utaratibu na miongozo mbalimbali zinazotawala muda wa Rais kudhaminiwa na Chama cha Mapinduzi.

===
Comrade Shaka mwenyewe tunahisi ni moja ya watu wanaomhujumu Rais Samia asigombee 2025. Ona mfano Comrade Kinana anavyotoa kauli ili Rais Samia akose uungwaji mkono 2025. Juzi hapa kasema traffic wapungue na tangu hiyo kauli itoke watu wengi wanakufa, foleni mfano barabara ya Morogoro toka Bwawani mpaka mikese ilikuwa haipitiki. Kikubwa wanajikusanyia pointi kusema Rais Samia hawezi, ona watu wanakufa wengi kwa ajali, huku Makamba akihakikisha bei ya mafuta inapanda kila kukicha, huku waziri wa kilimo akihakikisha wananchi wanauzia chakula shambani lengo ni kutengeneza taharuki nchi iwe vibaya na mwisho alaumiwe Rais Samia.
 
Urais ni uwezo na Si Zawadi mtu azawadiwe!!!

Kwamba wakiruhusiwa wengine kuchukua fomu watavuruga amani kivp?

What if mgombea wa CCM akionekana hatoshi dhidi ya upinzani?

Nisikuchoshe maana 2025 hapatakuwa na uchaguzi pia mwaka huo ni mbali Sana Bado.
Kuna watu wanatoa Maoni mpaka unaghabika kiasi cha kutamani umtwange mtu Risasi. Hivi kweli huyu Shaka angalikuwa anajua Uongozi unatolewa Kwa wananchi kuamua kupitia Sanduku la Kura huyo Shaka angalitamani huyo mama agombee kweli kupitiq Chama Chao? Hivi kweli Uongozi wa Nchi umeshafikishwa kwenye level hiyo ya kugawiana zamu hata kama uwezo wa mtu ni Zero. Leo nilikuwa naongea na Mzee mmoja alipigana Vita ya Kagera na ni Mwana-CCM lakini hataki kabisa kumsikia huyo mwanamama! Anasema anaibiwa sana na sababu ni kwamba hajui Hesabu.
 
Binafsi sina shida ata akikaa miaka 100 ila kila rais anasifiwa amefanya makubwa sasa mbona nchi inasogea mwendo wa tractor? Mbona nchi zenye improvements inayoonekana hawapendi kusifusifu namna hii?

Rais Samia akitaka kuacha legacy nzuri sio kusikiliza hao praise team nahisi atuachie katiba ngumu zaidi ya ile rasimu ya Warioba ili atakaetumia public fund vibaya tuu kitanzi tuu hadharani au kifungo cha maisha maana hamna iliyoendelea kilelema hapa duniani
Ndio maana kila wakati nasema huyu mama naye IQ yake ni Zero. Magufuli alikuwa huwezi kumsifia namna hiyo na asikueleze ukweli. Namkumbuka Kangi Lugora alimaliza kusifia lakini akamtumbua. Sasa huyu ukichanganya na Jinsia yake kuwa wanawake wanapendwa kusifiwa hapo ndio wamemfikisha kabisa. Utashangaa watu wamemwambia ukweli kuwa Turn out ya wananchi kwenye Mikutano yake haitishi yeye kaona huo sio ukweli. Anataka wamwambie anapata Nyomi. Bure kabisa!
 
Utamaduni huwa unabadilika kulingana na uhitaji wa nyakati. CCM inapigia debe utamaduni huu lakini ipo siku utawatokea puani.

Suppose wamechagua mgombea lakini kwenye angu yake ya kwanza akaonekana ameshindwa kazi, je atavumiliwa mpaka miaka 10 iishe?

Leo yupo SSH tunasifia kesho hatujui ataletwa nani.
 
Back
Top Bottom