Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,501
- 9,280
Serikali imetangaza awamu ya pili ya ajira ya walimu 5,000 ili kufikia idadi ya walimu 13,000 kutokana na kibali kilichotolewa na Rais John Magufuli.
Septemba 7, mwaka jana Rais John Magufuli alitoa kibali cha ajira mpya za walimu 13,000 wa shule za msingi na sekondari pamoja na mafundi sanifu wa maabara za shule.
Akihutubia mkutano wa pili wa Umoja wa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi Tanzania Bara jijini hapa jana, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tamisemi, Joseph Nyamhanga alisema awamu ya pili ya ajira ya walimu 5,000 itafanyika mapema mwaka huu.
Nyamhanga alisema awamu hiyo ya pili inafanyika baada ya ajira ya awamu ya kwanza ya walimu 8,000 kutangazwa. Walimu hao wameripoti kazini hasa maeneo ya vijijini tangu Desemba mwaka jana.
Alisema walimu 5,000 watakaoajiriwa awamu ya pili watapelekwa vijijini na kwenye maeneo yenye uhitaji mkubwa kwa shule za msingi na sekondari.
“Kuna shule za msingi na sekondari zaidi ya 2,500 ambazo hazikupangiwa walimu kwenye awamu ya kwanza ya ajira za walimu 8,000,” alisema.
Alisema shule zitapata walimu katika awamu ya pili na umuhimu utawekwa kwa shule zenye uhitaji hasa za vijijini.
Alisema Serikali imeweka utaratibu wa kuingia mkataba na walimu hao kwamba hawatahama kwenye kituo chao cha kazi hadi ipite miaka mitatu.
Nyamhanga alisema Serikali imetoa maelekezo kwa walimu wenye matatizo ya kiafya, lakini alisisitiza kuwa wale wenye visingizio hawataruhusiwa kuhama.
Naye Naibu Katibu Mkuu Elimu wa Tamisemi, Gerald Mweli aliwataka walimu wakuu waache kuweka barua zenye nembo ya Serikali au halmashauri kwenye makundi ya Whatsapp.
“Matumizi ya mitandao ya kijamii. Tusiweke kila kitu kwenye makundi ya Whatsapp, hatutamvumilia mtu nimeona niseme hili kabla ya kuanza kuchukua maamuzi magumu,” alisema Mweli.
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Walimu Wakuu Tanzania Bara, Rehema Ramote amesema pamoja na juhudi za Serikali za kujenga vyumba vya madarasa, nyumba za Walimu na matundu ya vyoo bado kuna changamoto katika shule nyingi za msingi.