Serikali imewakosea nini walimu wa Tanzania kugoma kuwalipa Fedha za likizo ya malipo Disemba 2023

Adharusi

JF-Expert Member
Jan 22, 2012
14,402
7,310
Tukiwa tunaelekea kwenda kumaliza mwaka wa fedha wa 2023/24 .Walimu wa Tanzania shule za msingi na Sekondari hawajalipwa fedha za Likizo ya mwezi DISEMBA 2023 imekua ni kuwaida serikali kuwalipa walimu fedha za likizo kwa namna inavyojisikia sio kwa mujibu wa sheria ,kanuni na taratibu..

Imekua ni kawaida Mwalimu kulipwa fedha ya mwezi June, kulipwa mwezi wa tisa au Kumi ,au kutolipwa kabisa ..

Wakati watumishi wengine wa Umma wakilipwa kila mwezi EDA kuanzia mamilioni hadi malaki ,lakini walimu kulipwa fedha za likizo ni mpaka wajisikie wakati serikali ni moja ,pato ni Moja kwanini walimu wanategwa na wananyimwa stahiki zao ..

Kwanini wasaidizi wa Rais wanaendelea kumuangusha Rais wetu ambae amejipambanua kuwajali watanzania wote.

Kama Waziri wa Fedha ni mmoja kwanini watumishi wengine wanalipwa fedha za likizo kwa wakati kabla ya kwenda likizo lakini Mwalimu wa shuke ya sekondari au Msingi fedha ya stahiki yake inageuka deni

Huko wapi Mchengerwa uliejipambanua kutetea walimu wa Tanzania, jiulize kwanini wewe posho zako hazichelewi lakini fedha ya likizo ya mwalimu inalipwa kama DENI

KAMA KWENU SIO KIPAUMBELE IONDOLEWE STAHIKI HIYO KWA WALIMU WA TANZANIA
 
Back
Top Bottom