Serikali yaanza mazungumzo kwa ajili ya kununua ndege nyingine ya mizigo

Hivi ni Serikali ndio inafanya Mazungumzo au ni Rais / Dr. ndio huwa ana-negotiate masuala ya Bei?

Tusichanganye Serikali hapa kwenye suala la mtu, Mazungumzo yote na hata mchakato wa manunuzi unakuwaga na supporting docs, pia unakuwa wa Uwazi na Ushirikishwaji kwa wadau.
 
Hii nchi tuijenge sote. Badala ya kusaidia kwenda mbele, wengi tunapinga kila kinachofanyika. Ni dhambi kubwa aisee.
Ukiangalia sana sababu ni kukosekana hela za kuchezea kwenye siasa. wana siasa walikuwa kama miungu. Miamala imekata wengine wameamua kuwa wazushi kwa kwenda mbele
 
Rudia kusoma post, vinginevyo labda mtoa mada awe amwekea maneno Mh Selasini, katika post yake mtoa mada ameonyesha wazi kwamba Mh. Selasini amependekeza kununuliwa ndege ya mizigo kwa ajili ya kusafirisha mazao ya kilimo kwenda kwenye soko la Ulaya.
 
Hii nchi hatuna sababu kabisa ya kuwa masikini.Tuna utajiri mkubwa mno.Sasa hii hoja ya Selasini inazidi kuumiza moyo.Tumecheleweshwa sana na wezi,wavivu na wazembe nchi hii.
 
Serikali imesema inapanga kununua ndege ya mizigo itakayosafirisha shehena ya bidhaa za maua na mbogamboga kwa lengo la kuongeza fursa za uwekezaji na biashara kwa wakulima nchini .

Mapango huo unaokusudia kuongeza na kuimarisha sekta ya usafirishaji kwa njia ya anga ndani na nje ya Tanzania utawezesha safari za moja kwa moja za bidhaa hizo kwenda na kutoka nje ya nchi.

Hayo yamesemwa na Rais Magufuli jana Jumamosi katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza wakati wa shughuli ya mapokezi ya ndege aina ya Bombardier Q-400

Alisema mikakati hiyo ndiyo maana Serikali inajenga vyumba vya barafu vya kuhifadhi maua na mbogamboga katika uwanja wa Mwanza, Songwe na Mbeya.
 
Na hii ndege nayo ikitua utasikia inatolewa kubeba mizigo ya watu bureeeeee bwerereeee!!
Nchi ya kitajiri sana hii....
 
Uwezo wake wa kufikiri unaishia hapo mkuu.
 


Wanunuzi wakizingua serikali itaweza kununua!?
 
Hii inanikumbusha enzi za DASAIR ya Uganda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…