Kihenzile aitaka TAA kuvunja Mkataba na Mkandarasi anayejenga kiwanja cha Ndege Ruvuma

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
943
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile ameelekeza mamlaka wa viwanja vya ndege Tanzania (TAA) kuvunja mkataba na Mkandarasi anayejenga jengo la abiria la kiwanja cha ndege cha Ruvuma kutoka na Mkandarasi huyo kushindwa kukamilisha jengo hilo kwa wakati.​

Naibu Waziri David Mwakiposa Kihenzile ameyasema hayo baada ya kutembelea na kukagua maboresho makubwa yaliyofanywa katika uwanja wa Ndege wa Songea.

“Serikali imewekeza bilioni 37 katika uwanja wa ndege huu, hivyo ni muhimu jengo la abiria likamilike kwa haraka. Nauelekeza uongozi wa TAA kuvunja mkataba na Mkandarasi anayejenga Jengo la Abiria kwani ameshindwa kukamisha kwa wakati ,Alisema Kihenzile

Jengo hilo la abiria lilitakiwa kukamika mwezi wa sita mwaka jana lakini mkapa sasa lipo asilimia 30 na Ujenzi wake unathamani ya shilingi milioni mianne ishilini na tatu (423) lakini ujenzi umesimama kutokana na changamoto za mkandarasi

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Songea Kapenjama Ndile amesema kuwa uwanja wa Ndege wa Songea ni muhimu kwa usafishaji wa Mizigo na Abiria kutoka nchi jirani kama vile Msumbiji na Malawi pia usafirishaji wa mazao ya Mboga mboga na matunda kama vile parachichi hivyo wananchi wa Songea na Mikoa jirani ni Muhimu kutumia uwanja huu ,alisema Ndile

Awali Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Songea Mhandisi Danstan Komba akisoma taarifa ya uwanja wa ndege huo amesema kuwa ujenzi wa Barabara ya ndege (Run way) umekamilika ,ujenzi wa barabara ya kiungio (Taxing Way) umekalika,Ujenzi wa kiuto cha nishati umekalika hivyo bado jengo la abiria .

Uwanja wa ndege wa Songea ni mojawapo ya viwanja vya ndege vilivyojengwa kuanzia mwaka 1974 kikiwa na barabara ya kutu ana kuruka ndege kwa kiwango cha changarawe, lakini sasa serikali umeboresha uwanja huo na wakuwa uwanja wa kisasa.


GHKRURhXcAABP0b.jpg
 
CCM imeshindwa kuliongoza hili taifa. Kitu pekee kinachotakiwa ni kuiamini CHADEMA na kuikabidhi nchi ili taifa liweze kurejeshwa katika nidhamu na matumaini. Wananchi wanazidi kuchoka drama za serikali yake.

Sasa kama ni kuvunja mkataba unafikiri mkataba unavunjwa bure? Kwanini mlimpa tender unqualified personnel wakati mnajua wazi kabisa ni kazi ya serikali ambayo anatakiwa aikamilishe kwa wakati maalumu?

Tupunguze pressure na visingizio. Hiyo ni systemic failure na siyo mkandarasi kama mnavyosingizia.
 
Back
Top Bottom