Serikali yaanza mazungumzo kwa ajili ya kununua ndege nyingine ya mizigo

Hivi ni Serikali ndio inafanya Mazungumzo au ni Rais / Dr. ndio huwa ana-negotiate masuala ya Bei?

Tusichanganye Serikali hapa kwenye suala la mtu, Mazungumzo yote na hata mchakato wa manunuzi unakuwaga na supporting docs, pia unakuwa wa Uwazi na Ushirikishwaji kwa wadau.
 
Hii nchi tuijenge sote. Badala ya kusaidia kwenda mbele, wengi tunapinga kila kinachofanyika. Ni dhambi kubwa aisee.
Ukiangalia sana sababu ni kukosekana hela za kuchezea kwenye siasa. wana siasa walikuwa kama miungu. Miamala imekata wengine wameamua kuwa wazushi kwa kwenda mbele
 
Inaonekana uwezo wako wa kuchambua mambo ni mdogo. Huyu kaomba soko la mazao yao, mwingine kakimbilia kununua ndege. Ndege bila kuwa na soko unafikiri ni suluhu la mkulima. Selasini kaomba serikali itafute masoko ya mazao ya wakulima ya ndege yanakuja baada ya kupata soko
Rudia kusoma post, vinginevyo labda mtoa mada awe amwekea maneno Mh Selasini, katika post yake mtoa mada ameonyesha wazi kwamba Mh. Selasini amependekeza kununuliwa ndege ya mizigo kwa ajili ya kusafirisha mazao ya kilimo kwenda kwenye soko la Ulaya.
 
Hii nchi hatuna sababu kabisa ya kuwa masikini.Tuna utajiri mkubwa mno.Sasa hii hoja ya Selasini inazidi kuumiza moyo.Tumecheleweshwa sana na wezi,wavivu na wazembe nchi hii.
 
Serikali imesema inapanga kununua ndege ya mizigo itakayosafirisha shehena ya bidhaa za maua na mbogamboga kwa lengo la kuongeza fursa za uwekezaji na biashara kwa wakulima nchini .

Mapango huo unaokusudia kuongeza na kuimarisha sekta ya usafirishaji kwa njia ya anga ndani na nje ya Tanzania utawezesha safari za moja kwa moja za bidhaa hizo kwenda na kutoka nje ya nchi.

Hayo yamesemwa na Rais Magufuli jana Jumamosi katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza wakati wa shughuli ya mapokezi ya ndege aina ya Bombardier Q-400

Alisema mikakati hiyo ndiyo maana Serikali inajenga vyumba vya barafu vya kuhifadhi maua na mbogamboga katika uwanja wa Mwanza, Songwe na Mbeya.
 
Na hii ndege nayo ikitua utasikia inatolewa kubeba mizigo ya watu bureeeeee bwerereeee!!
Nchi ya kitajiri sana hii....
 
Inaonekana uwezo wako wa kuchambua mambo ni mdogo. Huyu kaomba soko la mazao yao, mwingine kakimbilia kununua ndege. Ndege bila kuwa na soko unafikiri ni suluhu la mkulima. Selasini kaomba serikali itafute masoko ya mazao ya wakulima ya ndege yanakuja baada ya kupata soko
Uwezo wake wa kufikiri unaishia hapo mkuu.
 
Naye Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, amesema serikali imekuwa ikihamasisha wakulima na wadau wengine kuongeza uzalishaji wa zao la parachichi hususan aina ya hass, kutekeleza mkakati wa kuainisha maeneo yote yanayofaa kwa kilimo hicho nchini pamoja na kuongeza uzalishaji wa miche ya maparachichi aina ya hass na kuilinda ili isiharibiwe na aina nyingine za mapachichi.


Wanunuzi wakizingua serikali itaweza kununua!?
 
Kama mchakato wa kununua ndege ya mizigo umeishaanza sidhani kama kuna ubaya tukishauri aina ya ndege itakayotufaa kubeba mizigo ya kiraia na pale itakapohitajika mizigo ya kijeshi. Nashauri inunuliwe McDonnell Dougrass 10....DC*KC-10.💪View attachment 1262139
Hii inanikumbusha enzi za DASAIR ya Uganda
1576438161224.png
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom