Serikali ya Tanzania inalijua hili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya Tanzania inalijua hili?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Quemu, Aug 13, 2009.

 1. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2009
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Wakati najiandaa kuja nyumbani na kuelekea jimboni kwangu Masasi kwenda kutangaza azma yangu ya kusimama uso kwa uso na mbunge wa sasa hapo mwakani, ilinilazimu kwanza nipitie kitengo cha afya cha county ninayoishi huko kwa Obama kwenda kuchoma masindano ya kinga. Yes, na mimi natangaza kama mzee wa Kyela. Ingawaje mimi sina uwezo wa kumwaga mazagazaga ya teknolojia huko jimboni kwangu.

  Kwa kawaida huwa sichomi hayo masindano ya kinga kila mara ninapojiandaa kuja nyumbani. Lakini safari hii imenilazimu kwa sababu nimejipatia 'precious cargo' hivi karibuni, na nisingependa niibebeshe mzigo wa mibacteria pindi nirudipo kutoka kwenye harakati zangu za kisiasa.

  Anyway, harakti zangu pembeni. Sasa kilichoteka macho yangu ni hii doc (hapo chini) ambayo inaonyesha aina ya kinga za magonjwa ambayo msafiri anashauriwa apewe aendapo nchi inayoitwa Tanzania.

  Yaani tunaongoza kwa case za TB kutokana na data za WHO. Isitoshe, jamaa wanashauri kuwa wasafiri wakimbilie Nairobi incase of serios medical conditions. Hii inamaanisha kuwa Kenya wana health care system mzuri sana kutushinda. Halafu eti tunawaita watani wetu wa jadi....mtani gani wa jadi anakushinda kwa karibu kila kitu.

  Oh well, hebu jioneeni wenyewe..


  [​IMG]

  [​IMG]


  [​IMG]
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Aug 13, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,417
  Trophy Points: 280
  Nini cha kushangaza hapo?
   
 3. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kama lugha imekupiga chenga sema wanaojua wakusaidie, hata hivyo aliyeileta hii ange-summarise ili hata hakina ngumbalu kama huyu wakaambulia japo kidogo.
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Aug 13, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,417
  Trophy Points: 280
  Badala ya kunisimanga si unisaidie basi....
   
 5. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Njooni tu home..tupo Watz 41m tunaishi kwa amani na upendo!

  Wala msiogope..wakenya wengi karibu na mpaka wa Tz na hata toka Mombasa pia huja KCMC kupata tiba kule..ni bora kuliko za kule kwao!
   
 6. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  N' jombba wewe rudi tu homu,wala uchijali!hiyo fomu chichi wametuchingijia.wizara ina rekords zake nzuri tu
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kila kilichosemwa hapo ni kweli, na we are in the highest risk category kwa kuwa na TB, si tanzania pekee bali nchi yoyote yenye zaidi ya 100 cases kwa lakimoja ya population.

  Hali ndio hiyo na hatuwezi kutakaa...

  Labda tukipunguza ushabiki wa siasa na kufanya mambo kwa vitendo ndio tutaweza address the real issues zinazotusumbua

  If you analyse critically, we have spent majority of last to weeks posts humu kumuongelea mwakalinga na dakitari... lets direct the same intensity and efforts kwenye solution za kweli za watanzania

  MTM
   
 8. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #8
  Aug 13, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Quemu,

  Watu wa West kama hawajui kuhusu nchi au jambo fulani basi wanafanya kama ndio hoi ile mbaya.

  Japo Nairobi wanaweza kuwa na efficiency kubwa zaidi ya Dar lakini Tanzania kwa ujumla naamini iko nafuu kuliko Kenya kwenye huduma ya afya, hasa kama wewe sio tajiri sana.

  Hayo ya Kyela, naona na wewe umeingia kwenye propaganda za watu bila hata kujitambua. Labda mpaka siku zikigeuziwa kwako ndio utajua nini maana ya JF na upotoshaji wake. Mafanikio mema kwenye harakati zako.
   
 9. M

  Mong'oo Member

  #9
  Aug 13, 2009
  Joined: Oct 13, 2008
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani hiyo form hawaja-update. Wizara wanajitahidi kwa kweli upande. Jamani hata homa ya mafua ya nguruwe Muhimbili walikuwa na wagonjwa kadhaa wageni. Kama sikosei vyombo vya habari waliripoti wameruhusiwa.
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Aug 13, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kabisa, lakini kutokana na ubora wa huduma Nairobi, i think its better to spend more while certain of the quality kuliko less and unsure of the outcome. We need to improve alot especially kwenye service industry


   
 11. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #11
  Aug 13, 2009
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Hamna cha kushangaza NN. Ni kwamba tu, hii fomu inadhihirisha jinsi gani nhci yetu ilivyojaa na utitiri wa magonjwa ambayo pengine tungeweza kuyadhibiti kama tungekuwa na health care system mzuri. Au wewe unaonaje?
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Aug 13, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,417
  Trophy Points: 280
  Oh yeah niko na wewe mia kwa mia. Na wala sio pengine tungeweza kuyadhibiti. Tunaweza kabisa kuyadhibiti lakini kwa sababu moja ama nyingine hatufanyi hivyo. Ni mambo ya kuweka vipaumbele tu.
   
 13. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #13
  Aug 13, 2009
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Tayari niko home mzee. Hayo magonjwa mimi hayanitishi. Kwani si sote tumekulia kwenye humu humu!

  Nimehamua tu kuiweka hii fomu kukumbusha ni ngazi gani nchi yetu ipo kwenye masuala ya afya
   
 14. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #14
  Aug 13, 2009
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Ha bana...wazushi wache wapige kelele na propaganda zao. Lakini nia na azma iko kidete kabisa. Ntakula sahani moja na mbunge wa jimbo langu hapo mwakani. Kesho ndo nafunga safari ya kwenda Masasi rasmi... Lazima kuwe na 'sheriff' mpya mwakani

  Tukirudi kwenye mada - hiyo efficiency ndiyo inawafanya wa west waone Kenya ni bora zaidi kwenye hicho kitengo. Kwani kwa comparison, mazingira ya Kenya yakoje kiusafi kulingana na Tanzania?
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Aug 13, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,417
  Trophy Points: 280
  Unajua wengi wetu sisi tuko so hung up on what the west think of us. Really, who the hell cares what they think of us? Badala ya sisi kufanya mambo yenye tija kwetu sisi tuna mind wanatudhaniaje. Muhimu ni kuangamiza hayo magonjwa. Yanatuathiri sisi.
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Aug 13, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Ebanaeee... hapo watu washageuza dili na usipoangalia watasubiri donors waje kutusaidia kutokomeza magonjwa hatari
   
 17. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #17
  Aug 13, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Wiser words were never spoken!
  Kumbe kajamaa kako sharp! Sasa, NN, mbona hautaki tujue kuwa vitu unavipata?

  Amandla..........
   
 18. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #18
  Aug 13, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hilo ndilo la muhimu kwetu. Hata hivyo kwa mfumo wa sasa, haiwezekani kuboresha mfumo wetu wa afya hata tukitembea uchi 24/7. Wafanyakazi wa afya wamekuwa miungu watu na wagonjwa wanaonekana kama nyau wanaokuja kuwasumbua. Viongozi wa ngazi mbali mbali wako busy na per diems na ufisadi wa kila aina. Kwa hiyo ni ndoto kuwa na efficient system for delivery of health care. Hakuna lolote linaloweza kufanyika kwa sasa.

  Yanayosemwa kwenye hii mada ni kweli. Hata hivyo ni sehemu ya uonzo wa mfumo mzima. Dawa ni kufumua huo mfumo na kuusuka upya. Kwa kizazi kinachotawala sasa hakuna uwezekano huo. Labda itokee miujiza au Watanzania wazinduke na kutupilia mbali hawa watawala waliojisahau. Laiti ndoto hizo za kuuona hukombozi huo zingenikuta ningali hai!
   
 19. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #19
  Aug 13, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Na wamedhihirisha kwenye fomu hizi. Kama hali ingekuwa hivi, nadhani watanzania wengi tungekuwa tumeshakufa hivi sasa
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Aug 13, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,417
  Trophy Points: 280
  Hehehe...Fundi Utumbo (just kidding). Hivi do you really think mimi ni kilaza hivyo? Come on man....you should know better....
   
Loading...