Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,498
51,092
Katika muendelezo uleule wa kudanganyadanganya wananchi serikali ya Samia imeanza kupiga chenga juu ya kupunguza tozo kubwa sana za miamala ya fedha.

Baada ya kelele kubwa na kukasirishwa kwa wananchi juu ya tozo kubwa za miamala ya fedha, serikali ya Samia ilijifanya kupoza kelele hizo kwa kuahidi kulifanyia kazi suala hilo. Lakini inaonekana hiyo ilikuwa ni tekniki ya kupoza hali huku wakiendelea kuwakamua wananchi pesa zao.

Hata Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa anasema tozo hizo haziwezi kuondolewa kwa sababu eti ziko kisheria.

Hoja hiyo ni hoja Muflisi kwa sababu hata Kikokotowo kilikuwepo kisheria lakini kiliahirishwa kutumika.

Tunaitaka serikali iitishe kikao cha dharura cha bunge ili bunge lipunguze hizo tozo mara moja.

Watanzania hatuwezi kuishi kwa kudanganywadanganywa

IMG-20210801-WA0124.jpg
 
Hana ujanja, miradi aliyoachiwa na Magufuli ni mingi na inahitaji pesa nyingi amejua akicheza haitakamilika.

Kuanzia SGR, Nyerere Dam, Kigongo Busisi, daraja la kule Mikocheni baharani, bado miradi mingine ya barabara, maji safi na salama, umeme vijijini, inahitajika kama kawaida.

Kama Magufuli alikuwa anawapora watu pesa zao isivyo halali, basi Samia anachukua pesa kwa watu kihalali kwa msaada wa sheria kandamizi zilizopitishwa na bunge feki.
 
MAMA anaupiga mwingi. Anafungulia nchi ili tuanze kuokota hela kwenye michanga.

Madini kafungulia, mabeberu wanapakua kwa kasi ya ajabu ili tuongeze pato la taifa. Kwa kitaalamu inaitwa ECONOMIC INCREMENTS.

Halafu pia MAMA hataki kodi za DHULUMA ndio maana kawaachia majizi na matakatishaji fedha ili uchumi wetu upanuke na kukua. Tunataka kuanza kuokota pesa.

Pesa ndio kila kitu. Kwa sasa tumehamia kwenye TOZO ili kupanua WIGO wa kuokota pesa.
 
safi sana
nimefurahi sana kuendelea kuijenga nchi yangu.
nitaendelea kulipa tozo kama kawaida.
lipa tozo kwa maendeleo yako
 
Ni mbinu zao tu za kuuwa miamala kwa mitandao, maana sasa hivi matangazo ya huduma za Mabenki yameshamiri.
 
wewe siunataka maji na hospitali yenye dawa lkn pia unataka barabara safi, sasa unadhani nani atakuletea hivyo vitu vyote? vishuke kutoka mbiguni?!
lipa tozo ufaidi matunda yako mwenyewe, acha kudeka.
 
wewe siunataka maji na hospitali yenye dawa lkn pia unataka barabara safi, sasa unadhani nani atakuletea hivyo vitu vyote? vishuke kutoka mbiguni?!
lipa tozo ufaidi matunda yako mwenyewe, acha kudeka.
 
Back
Top Bottom