jaap

JF-Expert Member
Dec 25, 2018
1,388
2,000
MAMA anaupiga mwingi. Anafungulia nchi ili tuanze kuokota hela kwenye michanga.

Madini kafungulia, mabeberu wanapakua kwa kasi ya ajabu ili tuongeze pato la taifa. Kwa kitaalamu inaitwa ECONOMIC INCREMENTS.

Halafu pia MAMA hataki kodi za DHULUMA ndio maana kawaachia majizi na matakatishaji fedha ili uchumi wetu upanuke na kukua. Tunataka kuanza kuokota pesa.

Pesa ndio kila kitu. Kwa sasa tumehamia kwenye TOZO ili kupanua WIGO wa kuokota pesa.
Kwanini asiongeze Tozo kwenye Madini na bidhaa zinazo toka nje ya nchi mfano mabati, saruji, na bidhaa za vyakula
 

barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
31,583
2,000
Katika muendelezo uleule wa kudanganyadanganya wananchi serikali ya Samia imeanza kupiga chenga juu ya kupunguza tozo kubwa sana za miamala ya fedha.

Baada ya kelele kubwa na kukasirishwa kwa wananchi juu ya tozo kubwa za miamala ya fedha, serikali ya Samia ilijifanya kupoza kelele hizo kwa kuahidi kulifanyia kazi suala hilo. Lakini inaonekana hiyo ilikuwa ni tekniki ya kupoza hali huku wakiendelea kuwakamua wananchi pesa zao.

Hata Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa anasema tozo hizo haziwezi kuondolewa kwa sababu eti ziko kisheria.

Hoja hiyo ni hoja Muflisi kwa sababu hata Kikokotowo kilikuwepo kisheria lakini kiliahirishwa kutumika.

Tunaitaka serikali iitishe kikao cha dharura cha bunge ili bunge lipunguze hizo tozo mara moja.

Watanzania hatuwezi kuishi kwa kudanganywadanganywa

View attachment 1876301
Safi
 

jaap

JF-Expert Member
Dec 25, 2018
1,388
2,000
Huyu maza ni mnyanganyi hana tofauti na mwenda zake
Bora mwendezake alikuwa ana nyanganya vitu tuna viona, huyu ameiga mfumo wa serikal ya awam ya 4 ya matumiz yanayozidi kipato, kwenye bajet yake bajet ya maendeleo ni ndogo na bajet ya matuzi ya kiofis ni kubwa, chai na vitafunwa, ukarabati wa ikulu Kwa billion 9 zimerud tena, semina , Safar za nje zimerud tena.
 

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
6,478
2,000
Hadi unatia aibu. Yan umeisha jua watu wanakwepa kodi badala ya kutafta njia ya kuwafanya wasikwepe kodi ww unakuja na njia ya kuongeza tatizo.
Ebu niambia ni jinsi gani mtumiaji wa miamala alikuwa anakwepa kulipia kodi(VAT) kwenye miamala aliyokuwa anaifanya?
VAT ni ndogo Sana huwezi kwepa, Serikali kamatieni hapo hapo.Nyie mnaolia Lia kama vifaranga ukute hujawahi dai risiti yoyote toka umeanza kufanya manunuzi.
 

Patra31

JF-Expert Member
Apr 24, 2020
2,974
2,000
VAT ni ndogo Sana huwezi kwepa, Serikali kamatieni hapo hapo.Nyie mnaolia Lia kama vifaranga ukute hujawahi dai risiti yoyote toka umeanza kufanya manunuzi.
Ujajibu swali langu. Acha kuruka ruka.
Kwaiyo unataka kusema kuwa wameongeza kodi ya miamala ili kufidia magepu ya watu wanaokwepa kutoa lisiti? Hiv unaona hiyo n hoja ya kuisema mbele za watu wenye akili timamu?
 

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
6,478
2,000
Ujajibu swali langu. Acha kuruka ruka.
Kwaiyo unataka kusema kuwa wameongeza kodi ya miamala ili kufidia magepu ya watu wanaokwepa kutoa lisiti? Hiv unaona hiyo n hoja ya kuisema mbele za watu wenye akili timamu?
Ndio nimejibu hivyo.Hicho unachouliza ndio jibu lenyewe.Unataka haki ila hutaki wajibu wako,sasa utatimiza wajibu kwa njia hizo
 

Chura

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
359
500
Akiongeza taxation kwenye madini vipi?
Hana ujanja, miradi aliyoachiwa na Magufuli ni mingi na inahitaji pesa nyingi amejua akicheza haitakamilika.

Kuanzia SGR, Nyerere Dam, Kigongo Busisi, daraja la kule Mikocheni baharani, bado miradi mingine ya barabara, maji safi na salama, umeme vijijini, inahitajika kama kawaida.

Kama Magufuli alikuwa anawapora watu pesa zao isivyo halali, basi Samia anachukua pesa kwa watu kihalali kwa msaada wa sheria kandamizi zilizopitishwa na bunge feki.
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
5,240
2,000
Wataachia tu..., sio kwamba wataacha sababu wanawapenda wananchi bali sababu yale mapato watashangaa sio mengi..., LABDA tu kama wanataka kuua mfumo wa mobile money kwa kufanya watu watumie Bank

 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom