pilato93

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
4,876
2,000
unaibiwaje wakati pesa inaenda kujenga madarasa watakayo soma watoto.wako na wajuu zako.
acha roho mbaya mkuu, changia maendeleo ya nchi yako.
Madarasa kila siku inapitishwa michango huku ya madarasa hawa ni wahuni tu na wezi
 

twahil

JF-Expert Member
May 31, 2011
4,100
2,000
Tunakubaliana na Serikali tozo zibaki ila ziangaliwe katika utozaji. Kusema ziondolewe kabisa ni kuihujimu Serikali ya Mama Samia imeshindwe kupeleka huduma za jamii kwa wananchi na kisha waanze kuisema.
 

twahil

JF-Expert Member
May 31, 2011
4,100
2,000
Hana ujanja, miradi aliyoachiwa na Magufuli ni mingi na inahitaji pesa nyingi amejua akicheza haitakamilika.

Kuanzia SGR, Nyerere Dam, Kigongo Busisi, daraja la kule Mikocheni baharani baso miradi mingine ya barabara, maji safi na salama, umeme vijijini, inahitajika kama kawaida.

Kama Magufuli alikuwa anawapora watu pesa zao isivyo halali, basi Samia anachukua pesa kwa watu kihalali kwa msaada wa sheria kandamizi zilizopitishwa na bunge feki.
Magufuli alikuwa anakopa sana kutoka nje. Ndani ya muda mfupi deni limeshuti sana. Mama hawezi kukopa hivyo, zaidi inabidi tugharamie kwa kulipa kodi.
 

whyme

JF-Expert Member
Jul 4, 2020
1,114
2,000
Usitegemee chochote kwa mwanasiasa, tafuta pesa kwa namna unayoijua uijali familia yako na watu wako wa karibu sana, uinjoi maisha, basi! haya matakataka mengine ya wanasiasa hayana umuhimu
 

Babe la mji

JF-Expert Member
Dec 14, 2019
378
1,000
Huyu mama yenu atakua na mwisho mbaya haijawahi tokea .Sasa kama inaua biashara za watu utawezaje kikuza uchumi kwa aina hii ya viongozi ni hasara kwa Taifa .
 

Patra31

JF-Expert Member
Apr 24, 2020
2,997
2,000
Hii kodi unaitafsiri isivyo.

Unajua kabla ya hii tozo sijui kodi mlikuwa mmeichukia serikali ya JPM kwa sababu ya namna zake za kukusanya kodi? Alipolazimisha kila duka lililoka mjini liwe na zile mashine za risiti? Kuanzia vile vigrocery vidogo kabisa hadi maduka makubwa? Ali mradi yapo tu mjini ilibidi yalipe kodi tu na kufunga zile mashine.

Now mi nilikuwa pro-JPM kindakindaki na nasikitika nchi imempoteza kiongozi very capable namna ile. Lakini miongoni mwa vitu sikukubaliana naye ilikuwa namna alivyodeal na private sekta namna ile. Hii nchi bado haijafikia kiwango cha private sekta kubeba mizigo yote ya nchi.

Hii nchi bado, inabidi wote tushiriki kuijenga na walau kwa hizi tozo hata yule asiyefikika kwa mifumo rasmi ya ukusanyaji kodi atashiriki.
Kwan wakati wa JPM tulikuwa hatulipi kodi kwenye miamala yetu? VAT iliyokuwa inakatwa tunapofanya miamala ilikiwa ni nn? Kodi kila mtu alikuwa analipa toka mwanzo ila hii ya sasa ni kuumizana ya unalipa kodi mara mbili tena unakatwa kodi kubwa kuliko anayokukata mtoa huduma
 

Benny Haraba

JF-Expert Member
Dec 7, 2012
6,814
2,000
Magufuli alikuwa anakopa sana kutoka nje. Ndani ya muda mfupi deni limeshuti sana. Mama hawezi kukopa hivyo, zaidi inabidi tugharamie kwa kulipa kodi.
Hatukatai kulipa kodi ila gharama za tozo nikubwa mno jaribu kumtumia mtu 25,000 upate majibu, laki moja kuituma kwenye mabenki wanakukata 6,130
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
87,211
2,000
Katika muendelezo uleule wa kudanganyadanganya wananchi serikali ya Samia imeanza kupiga chenga juu ya kupunguza tozo kubwa sana za miamala ya fedha.

Baada ya kelele kubwa na kukasirishwa kwa wananchi juu ya tozo kubwa za miamala ya fedha, serikali ya Samia ilijifanya kupoza kelele hizo kwa kuahidi kulifanyia kazi suala hilo. Lakini inaonekana hiyo ilikuwa ni tekniki ya kupoza hali huku wakiendelea kuwakamua wananchi pesa zao.

Hata Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa anasema tozo hizo haziwezi kuondolewa kwa sababu eti ziko kisheria.

Hoja hiyo ni hoja Muflisi kwa sababu hata Kikokotowo kilikuwepo kisheria lakini kiliahirishwa kutumika.

Tunaitaka serikali iitishe kikao cha dharura cha bunge ili bunge lipunguze hizo tozo mara moja.

Watanzania hatuwezi kuishi kwa kudanganywadanganywa

View attachment 1876301
Dawa ni moja tu , kubeba pesa na kuzipeleka kwa bodaboda
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,652
2,000
Wewe siunataka maji na hospitali yenye dawa lkn pia unataka barabara safi, sasa unadhani nani atakuletea hivyo vitu vyote? vishuke kutoka mbiguni?

lipa tozo ufaidi matunda yako mwenyewe, acha kudeka.
Sasa hiyo tozo tunalipa wananchi wanyonge pekee?

Mbona hao wabunge pamoja na mamilioni wanayolipwa, lakini hawalipi PAYE kutoka kwenye mishahara yao??
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,652
2,000
Mara nyingi tozo zinakuwa ndani ya jedwali na waziri ana mamlaka ya kuzibadilisha hata bila kushirikisha bunge, sema tu wameamua kupotezea........washatufanya mazwazwa.
Lakini wanachosahau ni kuwa hata hayo makampuni ya simu yatakufa

Hivi unajua kuwa wananchi weshaanza kususia hizo huduma za simu, ikiwemo hiyo miamala ya simu?

Kwa hiyo serikali itakosa hizo tozo za dhuluma walizozianzisha na makampuni ya simu yata-colapse.

Huo ndiyo ukweli mchungu ambao inabidi serikali waumeze
 

pilato93

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
4,876
2,000
Tunakubaliana na Serikali tozo zibaki ila ziangaliwe katika utozaji. Kusema ziondolewe kabisa ni kuihujimu Serikali ya Mama Samia imeshindwe kupeleka huduma za jamii kwa wananchi na kisha waanze kuisema.
Tozo ziondolewe hawakufikilia sawa sawa ni kumuongezea
 

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
4,578
2,000
Safi kabisa naipongeza serikali kwa kusimamia sheria, hiyo ni nguzo muhimu kwa utawala bora !
 

Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
7,109
2,000
Lakini wanachosahau ni kuwa hata hayo makampuni ya simu yatakufa

Hivi unajua kuwa wananchi weshaanza kususia hizo huduma za simu, ikiwemo hiyo miamala ya simu?

Kwa hiyo serikali itakosa hizo tozo za dhuluma walizozianzisha na makampuni ya simu yata-colapse.

Huo ndiyo ukweli mchungu ambao inabidi serikali waumeze
VODA wameshalalamika biashara yao ya huduma za kifedha kushuka hasa maeneo ya vijijini, kuna hatari makampuni yakaanza kuhamisha mitaji na kuathiri maendeleo kwenye sekta nzima ya mawasiliano.....tutarudi enzi za kupanda juu ya miti ili uweze kupata network.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,566
2,000
safi sana
nimefurahi sana kuendelea kuijenga nchi yangu.
nitaendelea kulipa tozo kama kawaida.
lipa tozo kwa maendeleo yako

Mama anakusanya pesa ili kulipa madeni aliyoacha dhalimu. Hakuna maendeleo yoyote ya maana atafanya zaidi ya kulipa madeni yenye riba kubwa yaliyokopwa na dhalimu ili kusaka political millage? Uzuri mimi Sasa hivi miamala yangu nafanya kupitia bank na sio huko kwenye miamala ya simu, na nyingine natuma hard cash.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,566
2,000
wewe siunataka maji na hospitali yenye dawa lkn pia unataka barabara safi, sasa unadhani nani atakuletea hivyo vitu vyote? vishuke kutoka mbiguni?!
lipa tozo ufaidi matunda yako mwenyewe, acha kudeka.

Uzeni zile raslimali mlizokuwa mnapiga nazo watu risasi kuwa mnazilinda. Tunataka tuone ule utajiri mnaosema tunao mpaka wazungu wanatuonea wivu. Au huo utajiri wa rasilimali ni hizi line zetu za simu?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom