Rais Samia: Serikali kufanya uchunguzi sababu halisi za mafuriko na kuchukua hatua

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,507
8,130
Rais Samia Suluhu ameongelea hali ya mafuriko nchini. Ametoa pole waliokumbwa na mafuriko ikiwemo Rufiji, Morogoro na Arusha. Pia ametoa pole kwa ajali ya wanafunzi iliyotokea leo jijini Arusha.

Rais amesema tangu mvua zianze tangu kuanza kwa mvua ambapo Rufiji Serikali imepeleka chakula na dawa, pia kujenga tents za kuwahifadhi ikiwemo kutumia miundombinu ya shule kama madarasa.

Rais Samia amesema wameelekeza nguvu kukabiliana na mahitaji ya haraka na amewataka viongozi wote kuwajibika ipasavyo. Rais Samia amesema pamoja na maeneo kukumbwa na mafuriko kila mara kutokana na asili yake ya mabonde Serikali itaendelea kuchukua hatua na kuimarisha jitihada za kupambana na mafuriko.

Rais samia amesema baada ya mvua hizi na hali ya kawaida kurejea, Serikali itafanya uchunguzi wa kina kubaini sababu halisi za mafuriko hayo na kuweza kuchukua hatua zitakazoondoa tatizo hilo kwa muda mrefu.
 
Safi sana! Hatimaye Raisi Raisi Samia ameanza kutuelewa na kutupilia mbali maelezo ya kisiasa!

TUNASISITIZA

Tunapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kwamba, uongozi wa CCM umekuwa ukijaribu kutumia kila njia kuonyesha hili tatizo halijasababishwa na Bwawa la Nyerere, pamoja na kuwapa TANESCO na wasemaji wa serikali na viongozi maagizo waseme nini ili kukwepa lawama.

Tunaukumbusha umma kwamba wanasiasa sasa ndio wamekuwa mainjinia wa kutoa ufafanuzi, na mainjinia wako kimya. Wenye akili wote wanajua kwamba tatizo ni kwamba Bwawa la Nyerere lilijazwa maji kupita kiasi na bila mpangilio, na walipogundua hili wakaamua kufungulia maji mengi kulinusuru bwawa na kuepuka mafuriko makubwa hata zaidi ambayo yangeleta maafa makubwa sana ikiwa Bwawa lingepata madhara. Hii ingekuwa habari ya ulimwengu na aibu kubwa kwa Tanzania, kashfa mbaya kwa uongozi wa Tanzania. Lakini hamtaki kukiri hili na kusema ukweli. Mbaya zaidi, mnawalaumu wananchi wa Rufiji kuwa wao ndio wamewasababishia haya matatizo.

Tunajua maelezo yote haya yanatokana na maelekezo toka juu kuhusu kutoa maelezo juu ya mafuriko ya Rufiji kwa sababu tu ya kuilinda serikali na CCM. Tunawaelewa, lakini wote mnaofanya hivi mnapaswa kuelewa mnashiriki dhambi ya wanasiasa. Tunatumaini dhamiri zao zitawishitaki.

Tungenda serikali itujibu ndio au hapana kwa maswali haya mawili;

  1. Je, ni kweli kwamba maji yalipofunguliwa Bwawa la Nyerere yalifunguliwa katika flow rate ambayo ilijulikana ingepeleka maji mengi downstream ambayo yangesababisha mafuriko?
  2. Je, ni kweli kwamba katika kipindi cha mwaka mzima cha masika na kiangazi, ikiwa maji yangeruhusiwa kupita kwa kiwango cha wastani unaokubalika, mafuriko yasingetokea kwa sababu ya dry and wet season flow rates balancing effect lakini hilo halikufanyika kwa kutaka Bwawa la Nyerere lijae haraka?
Tunataka muelewe kwamba si kila mtu ni mjinga wa kukubali maelezo ya kisiasa ambayo mnatoa, na maelezo yenu hayabadili ukweli kwamba mafuriko yanayotokea Rufiji ni uzembe tu wa kuruhusu viongozi wa kisiasa kujifanya wanajua kuliko wataalamu wetu, na kuelekeza mambo yafanyike kwa kuipromote serikali iliyopo madarakani na CCM

Tunajua kwamba Tanzania hatuna utamaduni wa kukiri makosa na kuomba msamaha. CCM sio chama cha kufanya hivyo, na sidhani kama Chadema wakija kuchukua nchi watakuwa na utamaduni huo. Kwa hiyo hili sio suala la kuwalaumu CCM dhidi ya Chadema, sio suala la kisiasa, bali ni ukweli kuhusu uzembe mliofanya na kuathiri maelfu ya Watanzania masikini.

Ushauri wetu kwenu ni kwamba, badala ya kutumia ubongo wa wanasiasa ku-manage maji ya bwawa la Nyerere, tumieni computer programe kama inavyotakiwa - flow in rate-retention-flow out rate. Mngefanya hivi, angalau mngewapa tahadhari wananchi miezi minne hata mitano kabla ya mafuriko, kama kweli tatizo lilikuwa ni natural weather issue.
 
Na tunatoa demonstration:

Wanachotaka kutuambia wanasiasa ni kwamba, uwepo wa Bwawa la Nyerere hautazuia mafuriko hata miaka ya mbele. Sasa hilo si kweli. Kila itakapotokea mafuriko wakati Bwawa la Nyerere lipo ujue kuna uzembe umefanyika.

Kumbuka, masika Tanzania ni kama miezi minne, na kiangazi ni kama miezi nane. Kwa nini uwe na mafuriko ukiwa na bwawa size ya Bwawa la Nyerere? Tumia akili.

Angalia hesabu hii ya kutunga utaelewa kilichofanya mafuriko yatokee Rufiji. Hizi sio namba halisi;

Ikiwa kuingia maji bila mafuriko ni 10 cubic meters/hr
Kujaa maximum = 6000 cubic meters
Kutoka maji bila mafuriko ni 10 cubic meters/hr
Kutoka maji yakaleta mafuriko ni 15 cubic meters/hr
Unachofanya ni kwamba unatoa maji kwa 13 cubic meters/hr wakati bwawa limefika say 3000 cubic meters capacity

Sasa kwa kuwa maji hayaendi kwa batches ni continuous flow, yaani hizo cubic meters zinakuwa katika flow rates, computer program itakuwa based na principle ya hesabu ya integration na optimization, yaani katika theory ya dy/dx, ambayo imejengwa nchini ya premise ya flow in rate-retention-flow out rate. Nikienda zaidi ya hapa nitawachanganya

In fact, katika kusema mafuriko yalitokea pia 1974 wanazidi kujionyesha walivyo mbumbumbu, kwa sababu unapotengeneza water level management system ya dam, unaangalia data za miaka hata 60 nyuma ili kuwa na scenario kwamba Rufiji inaweza kuwa na maximum flow rate ya kiasi gani, na bado ile maximum flow rate unaipiga factor inaitwa safety factor katika engineering. Yaani kama maximum flow rate ni ya mwaka 1974 na lilkuwa 15 cubic meters/hr, basi wewe unaikuza kwa 15% kama factor of safety. Kama kulikuwa na mafuriko makubwa zaidi ya yale ya 1974, basi unatumia maximum flow rate ya hayo mafuriko, na pia kuyapiga factor of safety.

Na pia unatumia climate change prediction model kuangalia huko mbele hata miaka 100 ijayo, what could be the maximum Rufiji flow rate, given your historical data za flow rate katika misimu ya mvua nyingi. In fact, kujua Rufiji ilipata mafuriko 1974 na kadhalika ilipaswa iwe sababu kwa nini mafuriko hayakupaswa kutokea baada ya kujengwa Bwawa la Nyerere. Hakuna injinia mjinga kiasi cha kusema mafuriko yalishawahi kutokea huko nyumba ndio maana na sasa yametokea, wakati tumejenga Bwawa la Nyerere.

Sasa usiniambie tumejenga Bwawa la Nyerere kwa ushauri wa waganga wa kienyeji wa kutabiri mvua.

Hawa watu walisubiri bwawa limefika 5800 cubic meters ndio wakashituka, jamani eeh, maji yanajaa kupita kiasi. Ikabidi, ili kuokoa Bwawa wafungulie maji kwa zaidi ya 15 cubic meters/hr, kiwango ambacho ni juu ya flow rate ya mafuriko. Na walijua kabisa wanafungulia maji juu ya kiwango cha mafuriko kwa sababu wasipofanya hivyo Bwawa litazidiwa. Halafu wakasema nyie wananchi ndio mmesababisha.

Sasa go east or west, mafuriko ya Rufiji tukiwa na Bwawa la Nyerere ni uzembe na ujinga wa viongozi wa siasa kulazimisha mambo wasiyoyajua. Na TANESCO hawawezi kukwepa lawama.
 
Tuko macho we samia ole wako ujifanye ati bwawa la Nyerere ndio chanzo!

Tunajua janja zako, unataka kupiga gia kubwa za angani. Hatudanganyiki.

Sasa wewe samia nakuagiza ukalitazame hili na uachane na janja za kitapeli.

Rufiji ina mafuriko toka enzi na enzi.

Ukitupara tutakupara kweli kweli. Tuko macho dhidi ya janja janja.

AIONE PACHA WAKO: FaizaFoxy
 
Rais Samia Suluhu ameongelea hali ya mafuriko nchini. Ametoa pole waliokumbwa na mafuriko ikiwemo Rufiji, Morogoro na Arusha. Pia ametoa pole kwa ajali ya wanafunzi iliyotokea leo jijini Arusha.

Rais amesema tangu mvua zianze tangu kuanza kwa mvua ambapo Rufiji Serikali imepeleka chakula na dawa, pia kujenga tents za kuwahifadhi ikiwemo kutumia miundombinu ya shule kama madarasa.

Rais Samia amesema wameelekeza nguvu kukabiliana na mahitaji ya haraka na amewataka viongozi wote kuwajibika ipasavyo. Rais Samia amesema pamoja na maeneo kukumbwa na mafuriko kila mara kutokana na asili yake ya mabonde Serikali itaendelea kuchukua hatua na kuimarisha jitihada za kupambana na mafuriko.

Rais samia amesema baada ya mvua hizi na hali ya kawaida kurejea, Serikali itafanya uchunguzi wa kina kubaini sababu halisi za mafuriko hayo na kuweza kuchukua hatua zitakazoondoa tatizo hilo kwa muda mrefu.
Rais amefanya vizuri kusema utafanyika utafiti sababu za mafuriko. Awe makini kuwadhibiti wapigaji maana tayari wamehasema yatajengwa mabwawa mawili mto rufiji eti kudhibiti mafuriko. Sasa isije kua danganyatoto maana hao wahuni wameonyesha tayari uamuzi tena hadi mkandarasi wameonesha kashapatikana. Wenye kuelewa wametuambia mafuriko kabla hata kujengwa bwawa la nyerere mvua zikizidi yalikua ni kawsida. Sasa wahuni wanataka kuletea taifa gharama isiyokua lazima kwa tamaa zao.
 
Naona shekeli za bunge la ujerumani zinafanya kazi vizuri hapa JF, mliserma ili bwawa lijae labda mvua za ernino mbili, mkaongeza bwawa litasababisha ukame mkubwa, sasa mnabadili gia angani kuwa bwawa linasababisha mafuriko.

Kweli kwenye udhia penyeza rupia, mtu anatumia usomi wake kukashfu bwawa la Nyerere!!!
 
Rais Samia Suluhu ameongelea hali ya mafuriko nchini. Ametoa pole waliokumbwa na mafuriko ikiwemo Rufiji, Morogoro na Arusha. Pia ametoa pole kwa ajali ya wanafunzi iliyotokea leo jijini Arusha.

Rais amesema tangu mvua zianze tangu kuanza kwa mvua ambapo Rufiji Serikali imepeleka chakula na dawa, pia kujenga tents za kuwahifadhi ikiwemo kutumia miundombinu ya shule kama madarasa.

Rais Samia amesema wameelekeza nguvu kukabiliana na mahitaji ya haraka na amewataka viongozi wote kuwajibika ipasavyo. Rais Samia amesema pamoja na maeneo kukumbwa na mafuriko kila mara kutokana na asili yake ya mabonde Serikali itaendelea kuchukua hatua na kuimarisha jitihada za kupambana na mafuriko.

Rais samia amesema baada ya mvua hizi na hali ya kawaida kurejea, Serikali itafanya uchunguzi wa kina kubaini sababu halisi za mafuriko hayo na kuweza kuchukua hatua zitakazoondoa tatizo hilo kwa muda mrefu.
Mafuriko Jangwani hayo.................... 
90ddaf77-4dab-401e-b9da-e33173584a5f.jpg
 
Back
Top Bottom