Ukifatilia haya mambo ya muhimu unaitwa mzee yaani vijana wa nchi hii ni bongofleva tu akilini mwao na wasanii ndio hivyo tena wanaipigia promo ccm so painful.
 
Urithi kwa namna gani? Wanyama wanazaliana kila mwaka.

Mimi nimekuwa positive kwasababu unless kufanyike utafiti utakaotoa majibu negative, sioni ubaya wa kuuza na kutengeneza fedha za kuboresha huduma kwa jamii.
Zamani mikumi nakumbuka nimewahi kuwaona faru na mbuni sasa unawaona mara nyingi kwenye zoo tu na huko nako wanauzwa!
 
Ulitaka kutupia watanzania lawama za export utakuwa mjinga wa halo ya juu. Wakenya serikali yao kwenye suala la ku add value na kutafuta masoko imewajengea mazingira mazuri kulinganisha na hapa kwetu mbali watu tukio wapa shamans ya kutuongoza wamekuwa ni wachumia tumbo.

Huwezi kusema eti utalii ni hospitality. Ndugu kubali kuwa hapa wewe ni mweupe. Kwa kukusaidia utalii na hospitality ni vitu viwili tofauti japo vinashabihiana. Kwahiyo msitake kuhalalisha wizi wa wanyama kwa sababu zisizo na mashiko.

Watalii hufuata vivutio na si hospitality kama unavyodai na kwa taarifa yako hizo nchi ulizo zitaja kuongoza kwa kupokea watalii wengi ni kwa sababu ya gharama kuwa chini ukilinganisha na Africa kwahiyo ni rahisi watu kwenda kutoka nchi za jirani kwenda kula bata spain, france n.k.

Hivi ulisha wahi kujiuliza kwanini asilimia kubwa ya watalii kutoka America wanapokuja Tanzania wanaokwenda mbugani na si Zanzibar?
 
Tupe jina la Kamishnaa ....TAWRI EIA??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…