Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema hadi kufikia leo mchana, kulikuwa na wagonjwa 66 wa #COVID19 katika mikoa 10 hapa nchini.
Akihutubia Bunge JijinI Dodoma, Waziri Majaliwa amesema mikoa 16 ikiwemo Arusha, Pwani, Manyara, Katavi, Rukwa na Kagera haina mgonjwa wa Corona.
Ameongeza kuwa, licha ya mlipuko wa #CoronaVirus wameweza kukaa Dodoma kwa takribani miezi miwili na nusu, na wameweza kutekeleza majukumu mbalimbali ya Bunge.
Amempongeza Rais Magufuli kwa msimamo wake uliofanya Tanzania kuwa mfano wa kuigwa duniani kwa namna aliyoshughulikia ugonjwa huo.