Serikali: Kwa sasa Tanzania ina wagonjwa 66 wa Corona nchi nzima ndani ya mikoa 10 na mikoa 16 haina wagonjwa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,490
2,000
4BBA2040-ED1B-404C-90BA-EF0A6407733A.jpeg

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema hadi kufikia leo mchana, kulikuwa na wagonjwa 66 wa #COVID19 katika mikoa 10 hapa nchini.

Akihutubia Bunge JijinI Dodoma, Waziri Majaliwa amesema mikoa 16 ikiwemo Arusha, Pwani, Manyara, Katavi, Rukwa na Kagera haina mgonjwa wa Corona.

Ameongeza kuwa, licha ya mlipuko wa #CoronaVirus wameweza kukaa Dodoma kwa takribani miezi miwili na nusu, na wameweza kutekeleza majukumu mbalimbali ya Bunge.

Amempongeza Rais Magufuli kwa msimamo wake uliofanya Tanzania kuwa mfano wa kuigwa duniani kwa namna aliyoshughulikia ugonjwa huo.
 
Boeing 757

JF-Expert Member
May 18, 2020
272
500
Alice in wonderland .tutaelewa SOMO tu na hizi siasa za bongo. Na si walisema mashine zinadanganya?😥
Na si kuna kiongozi alisema tusali tumeshinda corona Yaani hakuna tena covid?
Na pia ...... Anyway nisije kupanik bure.
 
Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
5,696
2,000
"Kwa taarifa ya leo mpaka mchana, kutoka katika vituo vya kutolea huduma vya Serikali na Binafsi wagonjwa wa Corona nchini wamebaki 66 katika Mikoa 10, katika Mikoa 16 haina wagonjwa ikiwemo Arusha, Kagera, Katavi, Manyara, Pwani, Rukwa" - Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Kwa hiyo wameongezeka kutoka wagonjwa 4 hadi wagonjwa 66 ndani ya wiki moja?

Kweli wanasiasa ni waongo!
 
Gulwa

JF-Expert Member
Jun 16, 2008
5,124
2,000
Alice in wonderland .tutaelewa SOMO tu na hizi siasa za bongo. Na si walisema mashine zinadanganya?😥
Na si kuna kiongozi alisema tusali tumeshinda corona Yaani hakuna tena covid?
Na pia ...... Anyway nisije kupanik bure.
Alice in wonderland .tutaelewa SOMO tu na hizi siasa za bongo. Na si walisema mashine zinadanganya?😥
Na si kuna kiongozi alisema tusali tumeshinda corona Yaani hakuna tena covid?
Na pia ...... Anyway nisije kupanik bure.
Utakuwa ni mjinga kumwamimi mvutabangi
 
Maelau

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
1,370
2,000
Alice in wonderland .tutaelewa SOMO tu na hizi siasa za bongo. Na si walisema mashine zinadanganya?😥
Na si kuna kiongozi alisema tusali tumeshinda corona Yaani hakuna tena covid?
Na pia ...... Anyway nisije kupanik bure.
Aisee, umenikumbusha mbali. Umekisoma kitabu cha Alice ? Basi mimi nimekisoma nikiwa darasa la nne mwaka 1985, swahili version. Kinavutia balaa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom