Ujenzi wa miradi mbalimbali ya barabara unaofanywa na Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania TANROADS umetajwa kuwa neema Kwa kufungua Nchi

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
664
829
Ujenzi wa miradi mbalimbali ya barabara unaofanywa na Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania TANROADS umetajwa kuwa neema, manufaa na kufungua fursa mpya kwa watanzania hasa kwa kuunganisha Nchi na mikoa kwa barabara nzuri za lami.

Kauli hiyo imetolewa mkoani Rukwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mheshimiwa Profesa Makame Mbarawa Aprili 30-2023 muda mfupi baada ya kutembelea na kujionea mradi wa Ujenzi Wa Barabara Ya Matai - Kasesya (50km) kwa kiwango Cha Lami unatekelezwa na Serikali ya awamu ya sita kupitia TANROADS.

Amesema mradi huo unatekelezwa awamu ya kwanza Kipande Cha Matai – Tatanda (25km) kwa gharama ya Shillingi Billioni 37.353 za Kitanzania, na kwamba mradi ni wa miezi 15, ambapo umeanza tarehe 6 Juni 2022 na unategemewa
kukamilika Septemba mwaka 2023.

"Tunajenga hii miradi kwa lengo la kufungua hii mikoa na Nchi yetu, Rais Dkt Samia ameleta fedha, wajibu wetu ni kusimamia Mkandarasi, wito wangu TANROADS makao makuu mpo hapa, mkuu wa mkoa upo hapa tunawaomba msimamie barabara hii kuanzia siku ya mwanzo, tukisimamia hapa sawa sawa huko mbele mambo yatakuwa mazuri" Ameongeza Waziri Mbarawa.

Kwa Upande wake Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila amesema mradi huo unaojengwa na Mkandarasi kutoka China M/s China Geo –
Engineering Corporation Ltd (CGC) unaanzia kwenye Mzani wa Matai kupitia vijiji vya Kizombwe, Sopa hadi Tatanda.

Amesema Utekelezaji wa mradi huo umedhamiria kukuza uchumi wa nchi na kuleta maendeleo kwa wananchi kwa kupunguza muda na gharama za usafiri, kuunganisha mazao ya kilimo na
ufugaji kuelekea soko la Sumbawanga, mikoa jirani ya Songwe na Mbeya na nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Zambia.

Aidha kwa sasa mradi umefikia 19.3% na Utekelezaji wake unahusisha pia Madaraja matatu mapya katika mto Matai, Mpala na Kanyele na Makalavati makubwa 8 na makalavati madogo 126 pamoja na
Barabara yenye urefu wa Kilomita 25 yenye upana wa mita 9.5; mita 1.5 kila
upande kwa ajili ya watembea kwa miguu na mita 6.5 kwa ajili ya magari.
 

Attachments

  • IMG-20230501-WA0416.jpg
    IMG-20230501-WA0416.jpg
    101.8 KB · Views: 5
  • IMG-20230430-WA0463(1).jpg
    IMG-20230430-WA0463(1).jpg
    90.9 KB · Views: 5
  • IMG-20230430-WA0453(2).jpg
    IMG-20230430-WA0453(2).jpg
    89.6 KB · Views: 5
  • IMG-20230501-WA0406(1).jpg
    IMG-20230501-WA0406(1).jpg
    72.2 KB · Views: 4
  • IMG-20230501-WA0417(1).jpg
    IMG-20230501-WA0417(1).jpg
    51.5 KB · Views: 4
  • IMG-20230501-WA0409(1).jpg
    IMG-20230501-WA0409(1).jpg
    62.2 KB · Views: 5
  • IMG-20230501-WA0419(1).jpg
    IMG-20230501-WA0419(1).jpg
    113.2 KB · Views: 4
  • IMG-20230501-WA0410(1).jpg
    IMG-20230501-WA0410(1).jpg
    104.3 KB · Views: 4
  • IMG-20230501-WA0414(1).jpg
    IMG-20230501-WA0414(1).jpg
    76 KB · Views: 4
  • IMG-20230501-WA0405(1).jpg
    IMG-20230501-WA0405(1).jpg
    77.2 KB · Views: 4
  • IMG-20230501-WA0408.jpg
    IMG-20230501-WA0408.jpg
    70 KB · Views: 4
  • IMG-20230501-WA0413(1).jpg
    IMG-20230501-WA0413(1).jpg
    62.3 KB · Views: 4
  • IMG-20230501-WA0411(1).jpg
    IMG-20230501-WA0411(1).jpg
    101 KB · Views: 4
Back
Top Bottom