Serikali iziachie taasisi kama UDART na DART zijiendeshe zenyewe na ziteue watendaji wanofaa hata kama ni kutoka nje

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
Maofisa watendaji wakuu wa taasisi yoyote ile ni maofisa waaandamizi kabisa wa kampuni au taasisi yoyote ya umma.

Kwa miaka mingi kumekuwepo na teuzi na tenguatengua za watendaji wa makampuni na taasisi mbalimbali za serikali jambo linoonyesha kuwa kuna tatizo kwani taasisi hizo ama zimeitia hasara kubwa serikali kuwa kutotengeneza faida yoyote au kushindwa kujiendesha kwa ufanisi na hivyo kusababisha hasara kwa kuilazimisha serikali kuweka fedha zake katika taasisi hizo.

Baadhi ya matatizo ya wazi kabisa la kwanza ni siasa kwamba teuzi za maofisa hawa zisiwe ni nafasi za kisiasa kwamba Rais ndie anayeteua watendaji hawa. Kuna kiongozi mmoja alisikika akisema yeye alifanya usaili wa afisa mtendaji mkuu wakiwa baa wanapata moja moto moja baridi jambo ambalo kimsingi si sawa.

Tatizo jingine ni kwamba kuteua afisa mtendaji mkuu kisiasa katika taasisi kama za UDART na DART kisiasa kunaleta tatizo jingine kwamba nafasi zao si za kudumu kulingana na muda na ukomo wa raisi aliepo madarakani pamoja na utekelezaji na utendaji wa kiongozi huyo mara atakapokuwa ameanza kazi yake katika taasisi hiyo.

Tujaribu kuangalia baadhi ya majukumu ya Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi yoyote ya umma au binafsi;

1. Kuipanua kampuni kibiashara na kuiwezesha kusimama kibiashara.

2. Kuongeza mapato na faida kwa kampuni na kuhakikisha mapato na faida havipungui.

3. Kuongeza bei za mapato kwa wanahisa yaani "share prices".

4. Kusimamia uendeshaji wote wa kampuni "overall operations" ya kampuni. Hapa haimaanishi kuwa afisa mtendaji ndie mkatisha tiketi au yeye ndie aneangalia mabasi yapo salama kuingia barabarani lakini ni kuhakikisha wale wanosimamia vitengo vinohusu hayo wapo kiganjani na hawachomoki.

Hayo ni majukumu ya msingi kabisa ya afisa mtendaji mkuu ila jambo kubwa kabisa ni kuhakikisha kampuni inapata faida kiuendeshaji na ahakikisha asimamia faida hiyo yaani profitability.

Chambuzi nyingi zaonyesha kuwa maofisa watendaji wakuu wakisimamia uzuri kampuni zao huweza kuimarisha uendeshaji kwa asilimia 45 na wengine asilimia 15 huongeza faida kubwa katika kampuni kwa mfumo mzuri waloweka wa namna kampuni itavyokwenda kiufanisi.

Afisa mtendaji mkuu mara nyingi akiingia mzigoni kwanza huangalia modeli ya biashara yaani model of business na huweza kuamua kupunguza watu, idadi ya karakana, kutafuta "suppliers" wenye bei nafuu, na pia kuhakikisha kuna mifumo imara ya kuingiza mapato kama ambavyo mkuu Meneja wa Makampuni alivyopendekeza katika mapendekezo yake kwa bosi mpya wa DART.

Sasa tukiingia kwa undani tujaribu kuangalia majukumu halisi ya Afisa Mtendaji Mkuu;

1. Kushughulikia maamuzi makubwa ya uendeshaji wa kampuni kuanzia maono au vision, stratejia, ukuaji mzima wa kampuni na pia kuangalia taasisi au shirika na mstakabali wake, tamaduni au culture na la msingi ni namna ya kupata fedha za kujenga taasisi, idara na kupata watu wazuri watakamsaidia kuendesha kampuni kisasa na kiufanisi zaidi. Hivyo hapa ashughulikia mwelekeo wa kampuni kistratejia.

2. Kutekeleza mikakati na kupendekeza mabadiliko. Hatua hii huja baada ya kuandaa maono yaani vision ya wapi afisa huyu ataka kampuni ielekee. Hivyo atawasimamia mameneja wa chini yake khasa OPS manager ambae ndie kama "Right hand man" wake. Mameneja wengine kama logistics na yule wa human resources nao watakuwa na wajibu huohuo wa kufuata vision iloandaliwa na CEO yasemaje.

Kwa mfano HR manager hawezi tu kuajiri watu wa hovyo kuja kuiba kwenye kampuni au CEO hawezi kuingilia pale ambapo mtu sahihi amepatikana wa kujaza nafasi fulani lakini kwa sababu yupo kimada sehemu yule kijana msomi na mtaalam akosa nafasi.

Mfano mwingine ni kwamba meneja ugavi yaani logistics hawezi kuingia mikataba ya kitapeli na kampuni ambayo haina anuani wala namba ya VAT lakini yalipwa fedha nyingi kuleta bidhaa mbalimbali kwenye kampuni.

Majukumu yanofuata ndo kiini cha mada hii kutaka kampuni au taasisi za umma zijiendeshe zenyewe na ziwe na uwezo wa kuteua afisa mtendaji wanemwona afaa.

Mara nyingi taasisi hizi zinakuwa na bodi ya wakurugenzi ambayo moja ya majukumu yake ni kumtafuta afisa mtendaji anefaa kwa kuja kuendesha kampuni. Jukumu hili limepokwa na siasa na maofisa wengi watendaji wanoteuliwa na raisi huteuliwa kisiasa zaidi au tu kutokana na utashi wa raisi alieko madarakani. Hivyo umuhimu mkubwa wa kuifanyia mabadiliko katiba yetu ili nafasi za watendaji wakuu wa taasisi za umma ziwe zatokana na bodi za taasisi hizi kufanya uteuzi wa watu wanoona wafaa.

Endapo bodi zitakuwa na uwezo wa kuteua CEOs wake wanofaa kutafungua njia kwa kupata watu wenye vipaji na itaalam wakiwemo wale kutoka nje ya nchi na hata kama alistaafu atapewa mkataba ambapo atasaidia kufundisha wale wanochipukia ambayo baadae watashika nafasi hizo.

Pia hali hiyo itapelekea bodi ya kampuni kumwajibisha afisa mtendaji endapo atakuwa na poor performance kwasababu ni lazima CEO huyo alete taarifa ya maendeleo ya kampuni khasa mpango wa stratejia ambao utampa feedback kutoka kwenye bodi pale itapomaliza kusoma ripoti hiyo.

Ufanisi wa kazi yaani performance hii ni jambo kubwa sana kwa CEO kulifanya maana ndo kiini cha yeye kuwepo hapo. Hivyo CEO atafahamu kuwa bodi iko shingoni na pia yeye atawajibika kwa mwenendo wa kampuni kifedha na kiundeshaji na ni lazima ofisini kwake atakuwa na ubao unoonyesha metrix inoonyesha performance , assessments, maoni na stratejia ya biashara inavyoenda.

Kwa mfano kwa DART metrix ya kuhusu training ya wafanyakazi itasaidia kufahamu ni dereva yupi ni bora kiutendaji, hagongi magari hovyo na yupo up to date na training metrix. Pia itasaidia kufahamu ni mfanyakazi yupi yupo nyuma kwa training na ni kozi zipi zafaa kuwepo around.

Mwisho ni kwa CEO kuwa smart na mfano wa kuigwa kutengeneza utamaduni mzuri kwenye mazingira ya kazi ili kuleta utamaduni kwa wafanya kazi kupenda kufanya kazi kwa kujituma na kuwa mwaminifu. Hii itasaidia kuwafanya watumishi kuona kuwa wana kiongozi ambae twaita in "firm but fair" na kampuni itakuwa imara kiuendeshaji na kiufanisi hivyo kuleta faida na kujipannua zaidi kibishara.

Kampuni ilo na CEO mzuri na mchapakazi itavutia wawekezaji ambao watataka kuwekeza fedha zao humo na kuifanya kampuni kuwa kubwa na yenye mtandao nchi nzima.

Hivyo tukitaka hawa maofisa watendaji wakuu wawe huru na wasiteuliwe kisiasa ni lazima maamuzi magumu yafanywe ili kuleta ustawi kwa kila mtanzania watu wapate ajira, wengine wasome zaidi na tuondoe kabisa siasa katika mambo ya msingi.
 
Katiba ya Nchi hii ndio kiini cha huu uozo wote uliopo hapa nchini. Njia pekee ya kuondokana na majanga hayo ni kubadilisha kabisa Katiba yote na kuweka Katiba nyingine Mpya itakayotokana na Maoni, mawazo na fikra za wananchi wengi zaidi.
 
Katiba ya Nchi hii ndio kiini cha huu uozo wote uliopo hapa nchini. Njia pekee ya kuondokana na majanga hayo ni kubadilisha kabisa Katiba yote na kuweka Katiba nyingine Mpya itakayotokana na Maoni, mawazo na fikra za wananchi wengi zaidi.
Twaweza kutumia njia walotumua Tunisia kuhusu katiba.
 
Waruhusu wananchi wanunue hisa na uongozi wa kampuni uwajibike kwa wana hisa. Kampuni hiyo iilipe serikali kwa kukodi kutumia miundombinu yake. Ikiendesha hiyo kiserikali tutafika 2050 bado tunapiga kelele UDART.
 
CCM kila kitu kwao mzaha!
Hivi kweli mtu kama kindamba ni wa kuweka UDART kweli?
Hii ni dharau sana kwa umma wa Tz wanaoteseka kwa usafiri wa hii kampuni!
 
Back
Top Bottom