Biteko aagiza Bodi ya ETDCO ivunjwe, Menejimenti isukwe upya

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko ameagiza kuvunjwa kwa Bodi ya kampuni tanzu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme (ETDCO).

Ametoa maagizo hayo kufuatia wizi na utendaji mbovu wa Kampuni hiyo huku akiagiza kuundwa upya kwa menejimenti ya kampuni hiyo kutokana na utendaji kazi mbovu, wizi fedha za umma ndani ya Shirika pamoja na wizi wa vifaa vya umeme uliokithiri.

Dk Biteko ametoa maagizo hayo wakati wa kikao kazi kati yake na uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na kampuni zake tanzu, wakurugenzi wa Tanesco wa kanda na mameneja wa mikoa kilichofanyika leo Alhamisi Machi 28, 2024 jijini Mwanza kikiwa na lengo la kujadili utendaji kazi wa sekta ya nishati .

Ametoa uamuzi huo ikiwa imepita siku moja, tangu aiagize Bodi ya Tanesco kumuondoa Meneja Mkuu wa ETDCO kutokana na utendaji mbovu wa kazi ndani ya taasisi na kusuasua kwa utekelezaji wa miradi ya umeme ukiwemo wa usafirishaji umeme kutoka Tabora hadi Urambo na Tabora hadi Mpanda.

Amesema baadhi ya watendaji wa shirika hilo na kampuni zake tanzu wameshindwa kutekeleza maelekezo yake aliyoyatoa Desemba 2, 2023, alipowataka kupambana na rushwa, kujenga mahusiano na wananchi wanaowahudumia, kuimarisha uaminifu ndani na nje ya taasisi, kuacha visingizio na kutatua matatizo ya umeme.

Pia ameagiza watumishi wote wanaojihusisha na wizi ndani ya shirika wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria ikiwemo kuwaweka pembeni kwa kuzingatia miongozo ya utumishi wa umma kwa kuwa wao ni sababu ya Watanzania kutokupata umeme wa uhakika.
 
Huyu waziri ndiyo hovyo kabisa. Hakuna anachokifanya. Yupo yupo tu.

Mxiuuuuuu!
 
Legacy ya Makamba kwisha habari yake

Makamba alijaza majizi tu kwenye bodi
 
Back
Top Bottom