Superbug
JF-Expert Member
- Jan 31, 2018
- 12,417
- 30,927
Serikali iwakopeshe mishahara walimu wa shule binafsi kipindi hiki Cha Corona kwa RIBA ndogo sana.
Ikumbukwe kwamba Hawa ni WATANZANIA wenzetu japo Kuna wachache sio WATANZANIA.
Serikali ione huruma kwa maelfu ya WATANZANIA watakaoathirika kutokana na janga hili. Binafsi nimetoa machozi kwaajili Yao nimevaa viatu vyao imeniuma Sana.
Madam ni mwajiriwa wa shule X basi hiyo ni dhamana yake alipwe mshahara na serikali halafu shule zitakapofunguliwa ada zikianza kukusanywa basi watarejesha kwa makato kama ya HESLB wanavyofanya ila iwe riba ndogo sana maana sio kosa lao.
Na mkataba useme wazi hatahama shule hiyo mpaka deni liishe.
Naiomba serikali iliangalie hili watu wake wanaanza kuadhirika huku mitaani.
Naamini serikali itasikia kama inavyosikia mengine.