Mh Rais, Mama yetu Samia Suluhu Hassan, Wakumbuke Walimu hasa wa Shule za Msingi katika kipindi chako cha Urais

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
1,612
1,002
Mheshimiwa Rais, Kwa Watanzania wengi wewe ni Mama yetu kipenzi, Kwa Watumishi wote wewe ndiyo mboni yao.

Mheshimiwa Rais, kwa muda mfupi uliokaa madarakani kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umefanya mengi makubwa na mazuri.

Katika sekta ya Afya umeboresha miundo mbinu yake ikiwa ni umaliziaji na ujenzi wa Zahanati, Vituo vya Afya, kuweka vifaa Tiba ikiwa ni pamoja ujenzi wa nyumba za Watumishi wa sekta za Afya.

Katika Sekta ya Elimu pia umeboresha miundo mbinu yake kwa kiwango kikubwa saana, madarasa yamejengwa kwa idadi ambayo haijawahi kutokea, kwa sasa hakuna Mwanafunzi anayesomea chini ya mti na kama yupo basi Mkurugenzi wa Halamashauri hiyo hakutendei haki Mheshimiwa Rais.
Ujenzi na umaliziaji wa mabweni, maabara za sayansi na mabwalo ya kulia chakula umefinyika karibia shule zote za Tanzania. Hakika Mwenyezi amungu aendelee kukupa nguvu za kuwatumikia Watanzania.

Kuna miradi mingi inaendelea ikiwa ni pamoja na miradi ya ujenzi wa barabara, SGR, miundo mbinu ya maji/mabwawa/Visima , mageuzi katika Kilimo pamoja na mambo mengi ambayo umeendelea kuyasimamia. Itoshe kusema Watanzania wengi wanakuombea Afya njema ili kuendelea kuwahudumia.

Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, nikiwa kama Mtanzania, mtoto wako wa Kitanzania, natambua mambo mengi uliyo nayo, natambua kila Mtanzania angetamanj ukamilishe jambo analopenda kwa kuwa binadamu ndivyo tulivyo hivyo jukumu la kuamua lipi utekeleze liko mikononi mwako pamoja na Serikali unayoiongoza.

Mhe Rais, Mama yetu, OMBI LANGU KWAKO, NAOMBA UIKUMBUKE SEKTA YA ELIMU KATIKA UPANDE WA NYUMBA ZA WALIMU HASA KWA SHULE ZA MSINGI ZILIZO VIJIJINI KABISA AMBAKO HAKUNA HATA NYUMBA ZA KUPANGA.

Mhe Rais, kuna Watumishi wako ambao ni Walimu wako vijijini ( hasa katika shule shikizi zilizoanzishwa miaka ya kuanzia 2000+ ) wanakosa hata nyumba za kupanga kutokana na ukweli kwamba Wakazi wa maneno yale wengi wanajenga nyumba za kuishi na familia zao tu.

Mhe Rais, nakuomba ikikupendeza wewe na Washauri wako azisha mradi ( program) Maalum wa ujenzi wa nyumba za Walimu wanaoishi maeneo ambayo hata nyumba za kupanga hazipo. Kama ambavyo Serikali imefanya vizuri katika program za umaliziaji maboma ya madarasa na maabara naamini kukiwa na program Maalum ya ujenzi wa nyumba za Walimu waliopo katika mazingira magumu ambako hata nyumba za kupanga ni shida itasaidia saana Watumishi hawa waweze kutekeleza majukumu yao vyema.

Imani yangu ni kuwa Mhe Rais utasikia kilio hiki cha Walimu hasa wa Shule za Msingi na kupunguza ukubwa wa tatizo.

#Mungu ibariki Tanzania
#Mungu mbariki mama yetu Samia Suluhu Hassan.
#Tanzania ndio nchi yetu.
 
The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
17,484
12,224

Kama salary haitoshi acha Kazi..

Umewahi kumuona Mwalimu amepauka kama mwanakijiji?

Labda Rais mjinga ndio atahangaika na watu ambao Hata mil.hawazidi out of 60mil.
 
Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
1,612
1,002
Kama salary haitoshi acha Kazi..

Umewahi kumuona Mwalimu amepauka kama mwanakijiji?

Labda Rais mjinga ndio atahangaika na watu ambao Hata mil.hawazidi out of 60mil.
Uwe unasoma ndiyo unajibu,
Wapi pamezungumziwa habari za Mshahara hautoshi?
Serikali imejenga/kumalizia maboma ya nyumba za Walimu wa Shule Secondary sehemu nyingi au Nyumba za Watumishi wa Afya kwani wana fika 60ml?.
Wake up...elewa kitu kinachozungumziwa,
Nilichozungumzia kuna sehemu ni vijini saaana, Wananchi wa maeneo hayo wanajenga nyumba zao tu za kuishi na familia zao, hivyo despite ya Walimu hawa wa Shule za Msingi hasa kule kwenye shule shikizi kuwa na uwezo wa kupanga lakini nyumba za kupanga hazipo, ombi langu katika sehemu kama hizi Serikali ipeleke mradi wa ujenzi wa nyumba za Watumishi.
 
Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
13,626
25,929
Mheshimiwa Rais, Kwa Watanzania wengi wewe ni Mama yetu kipenzi, Kwa Watumishi wote wewe ndiyo mboni yao.

Mheshimiwa Rais, kwa muda mfupi uliokaa madarakani kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umefanya mengi makubwa na mazuri.

Katika sekta ya Afya umeboresha miundo mbinu yake ikiwa ni umaliziaji na ujenzi wa Zahanati, Vituo vya Afya, kuweka vifaa Tiba ikiwa ni pamoja ujenzi wa nyumba za Watumishi wa sekta za Afya.

Katika Sekta ya Elimu pia umeboresha miundo mbinu yake kwa kiwango kikubwa saana, madarasa yamejengwa kwa idadi ambayo haijawahi kutokea, kwa sasa hakuna Mwanafunzi anayesomea chini ya mti na kama yupo basi Mkurugenzi wa Halamashauri hiyo hakutendei haki Mheshimiwa Rais.
Ujenzi na umaliziaji wa mabweni, maabara za sayansi na mabwalo ya kulia chakula umefinyika karibia shule zote za Tanzania. Hakika Mwenyezi amungu aendelee kukupa nguvu za kuwatumikia Watanzania.

Kuna miradi mingi inaendelea ikiwa ni pamoja na miradi ya ujenzi wa barabara, SGR, miundo mbinu ya maji/mabwawa/Visima , mageuzi katika Kilimo pamoja na mambo mengi ambayo umeendelea kuyasimamia. Itoshe kusema Watanzania wengi wanakuombea Afya njema ili kuendelea kuwahudumia.

Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, nikiwa kama Mtanzania, mtoto wako wa Kitanzania, natambua mambo mengi uliyo nayo, natambua kila Mtanzania angetamanj ukamilishe jambo analopenda kwa kuwa binadamu ndivyo tulivyo hivyo jukumu la kuamua lipi utekeleze liko mikononi mwako pamoja na Serikali unayoiongoza.

Mhe Rais, Mama yetu, OMBI LANGU KWAKO, NAOMBA UIKUMBUKE SEKTA YA ELIMU KATIKA UPANDE WA NYUMBA ZA WALIMU HASA KWA SHULE ZA MSINGI ZILIZO VIJIJINI KABISA AMBAKO HAKUNA HATA NYUMBA ZA KUPANGA.

Mhe Rais, kuna Watumishi wako ambao ni Walimu wako vijijini ( hasa katika shule shikizi zilizoanzishwa miaka ya kuanzia 2000+ ) wanakosa hata nyumba za kupanga kutokana na ukweli kwamba Wakazi wa maneno yale wengi wanajenga nyumba za kuishi na familia zao tu.

Mhe Rais, nakuomba ikikupendeza wewe na Washauri wako azisha mradi ( program) Maalum wa ujenzi wa nyumba za Walimu wanaoishi maeneo ambayo hata nyumba za kupanga hazipo. Kama ambavyo Serikali imefanya vizuri katika program za umaliziaji maboma ya madarasa na maabara naamini kukiwa na program Maalum ya ujenzi wa nyumba za Walimu waliopo katika mazingira magumu ambako hata nyumba za kupanga ni shida itasaidia saana Watumishi hawa waweze kutekeleza majukumu yao vyema.

Imani yangu ni kuwa Mhe Rais utasikia kilio hiki cha Walimu hasa wa Shule za Msingi na kupunguza ukubwa wa tatizo.

#Mungu ibariki Tanzania
#Mungu mbariki mama yetu Samia Suluhu Hassan.
#Tanzania ndio nchi yetu.
Badala ujenge kwako, unaomba ujengewe na serikali??
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom