Serikali imeamua kabisa kula kuku kwa mrija kufurahia watanzania kupoteza maisha/kupata ulemavu wa kudumu

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,718
Nsikuchoshe na Usinchoshe, tusichoshane!.

Hivyo ndivyo navyo weza kusema kwasababu ni kama viongozi waliopewa dhamana ya kuwatumikia watanzania na kuhakikisha mali na usalama wa maisha yao unalindwa kwa wivu mkubwa.

Hizi ajali zinazoendelea kuwamaliza watanzania na kuwaacha wengi wakiwa na ulemavu wa kudumu bila viongozi wa serikali wenye mamlaka kuchukua hatua stahiki ni kana kwamba wanafurahia kinachoendelea huko mabarabarani. Ni ndani ya wiki iliyopita tu tumeona na kushuhudia kampuni ya magari ya New force ikipata ajali kadhaa ambazo zimetushangaza wengi.

Jambo la kuchekesha na kufurahisha(Kituko) ni viongozi wa LATRA kuyafungia hayo magari yasianze safari saa 9 usiku na badala yake yaanze safari kuanzia ule muda wa kawaida uliozoeleka wa saa 12 asubuhi, hivi ndugu viongozi mmeona kabisa hizo ajali chanzo ni kuanza kwa safari saa 9? Hiyo kampuni ya New force hapo kabla ya huo muda wa saa 9 usiku kupitishwa rasmi hazikuwa zikipata ajali?

Tuachane na hilo
Leo tarehe 4.7.2023 huko Tabora kuna gari la kampuni ya Happy Nation limepata ajali na kuna hati hati itakuwa imeua na kuwaacha wengine wakiwa na ulemavu wa kudumu.

Mimi kama mtanzania huwa naona uchungu sana na naumia sana namna ndugu zetu wanavyopoteza maisha kunakosababishwa eidha na ubovu wa chombo,uzembe wa dereva au kutokuwajibika sawasawa kwa serikali na idara zake.

Kwa bahati nzuri ni kwamba,hapa JF tuna viongozi ambao husoma nyuzi mbalimbali,sasa niwaombe ndugu zangu viongozi,mara kadhaa nimekuwa nikiandika namna Bora ya kukomesha au kupunguza kabisa hizi ajali za barabarani kama si kuziondoa kabisa.

Naomba viongozi mpate muda wa kusoma ushauri wangu na ikiwezekana wafikishieni viongozi wenzenu muweze kuchambua yanayowezekana ili yafanyiwe kazi ili kupunguza kabisa maafa yatokanayo na ajali za barabarani,nipo tayari kushirikiana na viongozi kama ukihitajika ufafanuzi ili kuweza kufanikisha kuokoa maisha ya watanzania.
 
Naomba viongozi mpate muda wa kusoma ushauri wangu na ikiwezekana wafikishieni viongozi wenzenu muweze kuchambua yanayowezekana ili yafanyiwe kazi ili kupunguza kabisa maafa
 
Dereva anaendesha Gari, kichwa kinamtuma aovertake Kwenye Kona na Gari inamshinda na kuingia vichakani Serekali itamfanyaje Huyu dereva!? Anyway huenda Kuna angalizo, napendekeza Serekali ianzishe mafunzo Maalumu Kwa madereva Ili waweze kuthamini Maisha Yao na ya abiria waliowabeba!! Otherwise sheria Kali zinaongeza tatizo Kwani akicheleweshwa ndio kunachochea Giza likiingia afanye mashindano
Dereva Hana staha barabarani, dereva anaendesha kukwepa tochi, Huku kwenye Kona, kitonga Nako Kuna tochi!?
 
Mkuu pitia hiyo link hapo nimependekeza na kutoa ushauri kwa hao madereva wazembe na namna ya kuwashughulikia
 
Ila swala la ajali huwaga aina kinda mara kaza wa kwaza serikali tunaonaa inaingilia kati ila kuhusu ajari iyo ni big shida
 
Mkuu pitia hiyo link hapo nimependekeza na kutoa ushauri kwa hao madereva wazembe na namna ya kuwashughulikia
Tunajenga nyumba Moja Mkuu, nimekuja na solution tayari, ni Hivi kama kampuni inamiliki vyombo vya usafiri liwekwe sharti ya kuwa ni lazima Kuwe na permanent staff WA occupation health and safety officer ambaye atakuwa ameajiriwa permanent, hivyo tool box meetings za madereva ziwe zinafanyika kila Wakati na viashiria vyote vya ajali wawe wanawafundisha madereva!!
Kwani Ajali hutokea Kwa kusababishwa na Mtu mmoja TU Kwa uamuzi usiofaa anaoufanya wakati Fulani ambaye ndio dereva, hivyo jitihada zote zifanyike kubadilisha minds za madereva,
Hii Sio vinginevyo Zaidi ya elimu na ukaribu wa usimamizi WA safety kazini
 
Safi kabisa mkuu
 
Back
Top Bottom