Je, Serikali bado imelala usingizi mzito wakati ajali inamaliza wananchi wake na kuwaachua ukilema mamia?

ruhi

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
3,740
5,426
Inafikirisha sana kusikia kila leo kumetokea ajali na vifo vya abiria vikiwa vingi sana hadi unajiuliza, je serikali inashirikiana na madereza pamoja na wamiliki wa mabasi kutengeneza ajali?

Je, mabasi haya kabla ya kusafiri/kuanza safari zinakaguliwa na chombo gani na kuruhusu waendelee na safari?

Utakuta kwa mfano gari linatoka Dodoma linafika Dar es salaam then linashusha abiria na kupakia abiria kwa ajili ya kuanza safari ya kurudi...ni chombo gani inajiridhisha na uhimara wa gari ili ianze safari tena?

Wamiliki wa mabasi jaribuni kuwashauri madereva ambao mmewapatia jukumu la kuendesha magari yenu kuwa waache kujiona kuwa wao wenyewe ndiyo wenye haki ya kuendesha magari wanavyojisikia. Ukiwa unaendesha gari ndogo alafu basi la abiria anavyo Overtake gari yako au magari mengine inasikitisha sana.
Swali la msingi, kwanini mabasi ya abiri yanayofanya safari zao nje ya nchi yanaendeshwa kwa utaratibu bila kutokea ajali za mara kwa mara kama mabasi yanayofanya safari za ndani ya nchi?

Nitoe wito pia kwa abiria, msiwe kama kondoo wakati mnapokuwa safarini; mwambieni driva ukweli kama anakeuka taratibu za uendeshaji.
Utakuta pale mbele kwa dereva pako open kabisa na amejaza staff wake wanapiga stori na simu pia anatumia kitu ambacho kinampunguzia umakini lakini abiria wamekaa kimya kabisa bila kumkanya.

Traffic wanaokaa barabarani acheni tabia ya kufika mlango kwa mabasi then unahamasisha abiria kufunga mkanda bila kuwabana wenye gari kabla ya gari kuondoka stendi mmekagua gari kama mikanda yote ni salama kwa ajili ya matumizi. Utakuta mkanda wa Gari ni chafu alafu haifungi vizuri mpaka unajiuliza SUMATRA wao kazi yao ni nini?

Serikali iingilie kati na kuangalia namna bora ya kupunguza ajali hizi zinazoleta umasikini kwa wananchi wake na kuwaachia wengine kilema za kudumu kwa sababu ya uzembe ya watu wachache.
 
Utakuta kwa mfano gari linatoka Dodoma inafika Dar es salaam then unashusha abiria na kupakia abiria kwa ajili ya kuanza safari ya kurudi...ni chombo gani inajiridhisha na uhimara wa gari ili ianze safari?
 
Barabara si rafiki. Magari yamekuwa mengi na makubwa wakati "Highway" zetu ni kama barabara za mitaani. Barabara zinatakiwa kuwa pana kama ilivyofanyika maeneo ya Mafinga.
 
Inafikirisha sana kusikia kila leo kumetokea ajali na vifo vya abiria vikiwa vingi sana hadi unajiuliza, je serikali inashirikiana na madereza pamoja na wamiliki wa mabasi kutengeneza ajali?

Je, mabasi haya kabla ya kusafiri/kuanza safari zinakaguliwa na chombo gani na kuruhusu waendelee na safari?

Utakuta kwa mfano gari linatoka Dodoma linafika Dar es salaam then linashusha abiria na kupakia abiria kwa ajili ya kuanza safari ya kurudi...ni chombo gani inajiridhisha na uhimara wa gari ili ianze safari tena?

Wamiliki wa mabasi jaribuni kuwashauri madreva ambao mmewapatia jukumu la kuendesha magari yenu kuwa waache kujiona kuwa wao wenyewe ndiyo wenye haki ya kuendesha magari wanavyojisikia. Ukiwa unaendesha gari ndogo alafu basi la abiria anavyo Overtake gari yako au magari mengine inasikitisha sana.
Swali la msingi, kwanini mabasi ya abiri yanayofanya safari zao nje ya nchi yanaendeshwa kwa utaratibu bila kutokea ajali za mara kwa mara kama mabasi yanayofanya safari za ndani ya nchi?

Nitoe wito pia kwa abiria, msiwe kama kondoo wakati mnapokuwa safarini; mwambieni driva ukweli kama anakeuka taratibu za uendeshaji.
Utakuta pale mbele kwa driva pako open kabisa na amejaza staff wake wanapiga stori na simu pia anatumia kitu ambacho kinampunguzia umakini lakini abiria wamekaa kimya kabisa bila kumkanya.

Traffic wanaokaa barabarani acheni tabia ya kufika mlango kwa mabasi then unahamasisha abiria kufunga mkanda bila kuwabana wenye gari kabla ya gari kuondoka stendi mmekagua gari kama mikanda yote ni salama kwa ajili ya matumizi. Utakuta mkanda wa Gari ni chafu alafu haifungi vizuri mpaka unajiuliza SUMATRA wao kazi yao ni nini?

Serikali iingilie kati na kuangalia namna bora ya kupunguza ajali hizi zinazoleta umasikini kwa wananchi wake na kuwaachia wengine kilema za kudumu kwa sababu ya uzembe ya watu wachache.

Ajali zaidi ni makosa ya kibinadamu wala si ubovu wa vyombo husika:

Ajali: Tuambiane ukweli dhahama hili lituepuke
 
Kwa wiki moja mkoa wa Tabora wamefariki zaidi ya Raia 30 Kwa ajali.
Mkuu wa Mkoa kafunga kichwa na masikio Kwa kitambaa hasikii wala haoni.
 
Mtanikumbuka!
 
Attachments

  • A36F4D49-BFFA-4CF6-B923-D6FF21022B44.jpeg
    A36F4D49-BFFA-4CF6-B923-D6FF21022B44.jpeg
    42.4 KB · Views: 3
Ijumaa majira ya saa mbili usiku kuna bus aina ya Scania likitokea Dodoma kwenda Dar lilianguka katikati ya barabara umbali wa Kilomita moja kutoka Ferry Dumila, haikujulikana chanzo cha ajali kilikuwa ni nini ila kulikuwa na majeruhi wengi na Polisi walikuwa hapo wakiwatoa ndani ya bus wahanga wa ajali.

Hii ajali haikusikika ilifanywa siri
 
Kwa wiki moja mkoa wa Tabora wamefariki zaidi ya Raia 30 Kwa ajali.
Mkuu wa Mkoa kafunga kichwa na masikio Kwa kitambaa hasikii wala haoni.
Acha upumbavu sasa dereva anaovertake bila kuwa makini hapa serikali inaingia vipi?refer ajali ya jana dereva wa basi anaovertake bila kuwa makini na kuleta janga kubwa utailamu serikali ?
 
Acha upumbavu sasa dereva anaovertake bila kuwa makini hapa serikali inaingia vipi?refer ajali ya jana dereva wa basi anaovertake bila kuwa makini na kuleta janga kubwa utailamu serikali ?
Unajua faini ya mahakamani Kwa dereva aliyeua abiria 18 huko Tabora?
Serikali inahusika 100%.

Sheria Za makosa ya barabara ukiwa mtu ni Za kijinga.

Pia waliokufa Bima yao ni 0 hapo.
Ilitakiwa ukiwa abiria dereva anafungwa kifungo cha miaka 10 bila faini , ajali zingepungua.
Kwa sasa hiyo ajali faini itakuwa Tsh 30,000.
 
Udereva ni utaalamu tofauti usio na mahusiano hata kidogo na kusolve simultaneous equation, au Mfekane War
Uko nje ya mada.

Issue siyo ku solve ma question. Issue ni cognition. Hata kwenye kulima nyanya, kuugua, kuuguza, biashara, nk. minimum formal education ni muhimu.

Ajali, ustaarabu, ufahamu, common sense nk, na elimu haviwezi kutenganishwa.
 
Hivi unajua mtu alieishia form 4 anaweza kwenda aviation college na akarusha ndege? Kwahiyo wao kuishia form 4 na kwenda vyuo vya udereva na kuendesha magari ni sawa kabisa elim ya form 4 inatosha kabisa kwa madereva assumption uliyonayo kwamba ufaulu mzuri wa darasani ndo utendaji mzuri hiyo siyo kweli kwa ajali za barabarani hata umuweke mtu mwenye ufaulu gan wa darasan huo siyo utatuzi wa suala hilo.
 
Hivi unajua mtu alieishia form 4 anaweza kwenda aviation college na akarusha ndege? Kwahiyo wao kuishia form 4 na kwenda vyuo vya udereva na kuendesha magari ni sawa kabisa elim ya form 4 inatosha kabisa kwa madereva assumptions uliyonayo kwamba ufaulu mzuri wa darasani ndo utendaji mzuri hiyo siyo kweli.

Hata aliyeishia form IV anaweza kuwa lawyer, daktari nk baada ya kwenda college.

Kwanini minimum education ndugu?

Minimum education huondoa wasiofaa. Hata polisi minimum education ingepanda ustaarabu ungeingia.

Sijui wapo unasoma ufaulu mzuri darasani. Tofautisha minimum education na ufaulu darasani.
 
Tatizo kubwa la ajali ni traffic police. Ajali hazitaisha hadi traffic waondoke barabarani. Siku barabara za highway zikiwa hazina traffic police wanaovizia madereva kuwapiga fine..ajali zaitaisha au kupungua sana.
 
Back
Top Bottom