Nyamesocho
JF-Expert Member
- May 5, 2023
- 476
- 1,244
Ingekuwa ni kikundi cha ugaidi kinaua Watanzania basi serikali ingetoa kila aina ya silaha kupambana nacho au angekuwa ni mtu anawapiga risasi raia wasio na hatia basi jeshi la polisi lingekuwa na operation za hatari.
Ajali zinazosababishwa na bodaboda ni zaidi ya ugaidi au mauaji ya kuwafyatulia risasi raia mtaani huku serikali ikiwa kimya kuhusu haya mauaji yanayoondoa watanzania kwa kila saa.
Binafsi ndani ya miaka 2 tu nimeshuhudia watu 6 tuliokuwa tunafahamiana wamekufa kwa sababu ya ajali za bodaboda kwa muda tofauti tofauti kwa nini huu usiwe ugaidi?
Serikali imekaa kimya huku jamii za kitanzania kila kukicha wanazika wenzao kwa sababu ya bodaboda na wengine wakiachiwa na ulemavu wa kudumu, kwa mfano kila familia ya Kitanzania imezika ndugu jamaa au rafiki kwa sababu ya bodaboda.
Hatukatai bodaboda imerahisisha usafiri na ajira kwa vijana lakini tunapoteza watu wengi sana kwa sababu ya bodaboda.
Serikali iandae utaratibu mpya wa bodaboda kudhibiti ajali, na waendesha bodaboda wapimwe akili, haiwezekani mwendesha bodaboda aondoke kwa speed 120 umbali wa mita 100.
Serikali ije na mpango mkakati kupunguza au kuondoa ajali za bodaboda, huu ni zaidi ya ugaidi tofauti yake ni ndogo tu, ugaidi watu wengi wanauawa kwa muda mfupi lakini huu watu wachache wanakufa kwa saa na serikali ipo tu.
Na serikali ianzishe kitengo cha kutoa takwimu za ajali za bodaboda kila mwezi ili jamii ichukue tahadhari.