Trafiki Makao Makuu yawataka madereva kutokuwa chanzo cha huzuni Nchini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini limesema zipo Sheria zinazotoa miongozo na taratibu za matumizi sahihi ya Barabara hapa nchini huku likiwataka madereva kutokuwa chanzo cha huzuni kwa watanzania kwa kusababisha ulemavu wa kudumu na kupoteza Maisha ya Watanzania.

Hayo yamesemwa mapema DEsemba 23,2023 na Afisa Mnadhimu Namba Moja wa Kikosi cha Usalama Barabani Nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Pili Misungwi katika Kituo cha mabasi yaendayo Mikoani na nchi Jirani Jijini Arusha ambapo amebainisha kuwa kikosi hicho kinaendelea na operesheni zake za ukaguzi na kutoa Elimu nchi nzima lengo likiwa ni kutomeza ajali hapa nchini.
8746cddf-ad2d-4b93-9a1e-cedb733c9719.jpeg

24dca4e1-9f8e-48c5-b55b-35a3b11d5321.jpeg
ACP Misungwi ameeleza kuwa hivi karibuni kikosi hicho kilifanya uhakiki wa leseni nchi nzima ili kubaini madereva wenye sifa ambao wanapaswa kuendesha vyombo vya moto huku akibainisha kuwa kwa sasa wanahakiki madereva hao kama wanasifa za kuendesha vyombo husika hapa nchini.

Pia amewataka abiria kote nchini kupaza sauti kwa baadhi ya madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani na pale inapobidi kumwambia dereva asiendeshe kwa mwendo kasi ikiwa ni Pamoja nakutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili hatua stahiki zichukuliwe kwa dereva ambaye amekiuka sheria za usalama barabarani.

Afisa mnadhimu huyo ametumia fursa hiyo kuwatakia safari njema abiria wanaosafari maeneo tofauti tofauti hapa nchini na nje ya nchi heri ya krismasi na mwaka mpya 2024.

Nao baadhi ya abiria wanaokwenda maeneo tofauti tofauti hapa nchini wamesema operesheni hiyo imekuja wakati sahihi ambapo kipindi hiki wananchi wengi wanakwenda maeneo mbalimbali hapa nchini kusalimia ndugu na jamaa huku wakilipongeza Jeshi la Polisi husasani kikosi cha Usalama Barabarani kwa kuendelea kutoa elimu na kufanya operesheni hizo ambazo zimesaidia kupunguza ajali nchini.

Amini Khamis ambaye ni dereva wa basi la kampuni ya Hajs amesemma wao kama madereva wanaendelea kufuata sheria za usalama barabarani ambazo zinawaongoza huku akibainisha kuwa elimu waliyopewa na afisa mnadhimu namba moja wa kikosi cha usalama Barabarani nchini yote waliyoambiwa watayafanyia kazi.
 
Hawa jamaa wameshindwa kukimbizana na nyakati.
Siku hizi information nyingi ni mitandaoni.

Traditional approach sio wakati wake.

Wangetengeza mifumo imara ya kutoa Habari, kupokea ushauri na wafanye askari wawe more friendly.

Lazima waanze kubadilika
 
Kuna madereva ni wa$eng£ yani unaweza ukawa upo rod na umezingatia kila sheria na tahadhari zote alafu akatokea fala mmoja kichwa kimejaa kiwingu na cuca, akakubadilishia historia ya maisha yako bila wewe kutarajia.
 
Ujumbe mzuri kutoka kwa kamanda ambao ameutoa kisiasa, reality iliyopo kwenye barabara zetu kuna sheria za aina tatu, kwanza zinazowahusu madereva wote wa serikali, jeshi,police, dfa etc etc ,hawa wao wapo above law ni untouchables, pili kuna buses &trunks drivers, hawa wana take chances na mwisho ni walala hoi, hawa ndio wanawindwa na traffic cops, na kuhusu uhakiki wa driving licenses, hii ni kazi ya poĺice SIO driver, inamaana police hawana systems ya utunzaji wa licenses?,kweli tumo shimoni,utawala wangu driving licenses zitatolewa na traffic dept.ya kila municipalities ,na zote zitajumuishwa pamoja kwenye systems mama, nitaiita NATIS
 
Back
Top Bottom