Serikali iingilie kati Makanisa ya Miujiza? Watanzania masikini wa kutupwa wanakamuliwa mamilioni kwa utapeli huku wahubiri wakigeuka mamilionea

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,604
Wanabodi

Kama kawa kila nipatapo fursa huja na makala zangu elimishi za kwa maslahi ya taifa. Topic ya leo, ni kutoa wito kwa Serikali yetu kuingilia kati kitu kinachoendelea kwenye baadhi ya makanisa ya wakovu yanayojinasibu kufanya miujiza, kutoa mapepo, kutoa uchawi na kufanya miujiza ya uponyaji?.

Baadhi ya wahubiri hawa wanatumia nguvu za giza za kiini macho kwa kitu kinachoitwa auto suggestion kwa Watanzania Masikini wa Kutupwa, kuaminishwa umasikini wao ni kwasababu wamelogwa, hivyo ili kuuondoa uchawi wa umasikini, unatakiwa kufanya appointment kumuona Mtumishi, ambapo utapangiwa kiwango cha fedha kumuona mtumishi.

Kwenye matangazo yao kupitia redio na TV, unaambiwa njoo na sadaka yako bila kuambiwa kiwango. Ukifika kanisani,
utaandikishwa na kuambiwa kiwango cha kumuona mtumishi akueleze jinsi ulivyologwa na ni nani amekuloga. Kiwango kilianzia 10,000, baadae ikawa 20,000, ikapanda kuwa 50,000, 100,000 sasa ni 200,000.

Unatakiwa kuitafuta hiyo pesa popote ulipe ndipo umuone mtumishi. Hivyo ni waumini wenye pesa tuu ndio watamuona mtumishi!.

Baada ya kuingia kumuona, mtumishi atakuambia prophesy yako na ku conclude matatizo yako yote, ya kiuchumi, umasikini, maradhi, au majanga yoyote, ni umelongwa na watu wa jijijini kwako!.

Baada ya hapo sasa ndio utapewa bili ya sadaka. Mtumishi atajifanya anamuuliza Mungu, then unaambiwa Mungu amesema njoo na sadaka ya milioni 2, 5, 10, 20, kutegemea na ukubwa wa tatizo lako, ya kuleta hiyo sadaka ndipo Mungu atalimaliza tatizo lako!.

Kutokana na wewe kuwa ni tayari umesha pigwa ganzi, utakwenda kuzitafuta hizo pesa na kuzileta cash!.

Watanzania masikini wa kutupwa, wanakamuliwa mamilioni kwa utapeli, na baadhi ya hawa ma Pastor, huku hao ma Pastor na wahubiri wakineemeka na kuageuka mamilionea na mabilionea huku wakivuta mi ndinga ya nguvu!.

Kuna Mama mmoja alifiwa na mtoto wake, the only son, amedanganywa mtoto wake hajafa, amechukuliwa tuu kichawi, mama kaambiwa akatafute sadaka kiasi fulani, arejeshewe mwanae!, huyo mama ana haha kusaka hiyo pesa ili kumrejesha mwanae!.

Japo haya ni mambo ya imani, na waumini wanakwenda wenyewe kwa hiyari yao na wana toa fedha kwa ridhaa zao, na serikali yetu imetoa uhuru wa kuabudu, lakini ikifikia kiwango Watanzania wanatapeliwa, serikali ina wajibu wa kuingilia kati wananchi wake wasiendelee kutapeliwa!.

Namalizia kwa ile hoja ya msingi jee kuna haja ya serikali iingilie kati shughuli za haya makanisa ya wakovu ya miujiza ili Watanzania masikini wa kutupwa, wasiendelee kukamuliwa mamilioni kwa utapeli, huku wahubiri wakizidi kunona kwa kuwa mamilionea!.

Naomba kuwasilisha.

Paskali
Update
Kuhani Musa pale Kimara Temboni kaporomosha mjengo wa billion kadhaa! Alianzia kwenye banda la mabati!
Mkuu Mywangu, usimwingize Mtumishi kweli wa Mungu, Kuhani Mussa, kumuona Kuhani Musa ni bure ila unaweza kuleta sadaka yako yoyote.

Kazi ya ujenzi wa Ngome ya Yesu pale Kimara Temboni, inafanyika kupitia kadi zinaitwa Partnership, hupangiwi kiwango, unajifanyia personal assessment ndipo unajaza!.

Watumishi matapeli kumuona ni lazima utoe 200,000, kuna watu walikuwa na 100,000 walitoa na zikapokelewa, watu wa 200,000 walipoongezeka, wale wa 100,000 walirudishiwa fedha zao, wakaambiwa wakadundulize mpaka zitimie 200,000 ndipo warudi.

Ukimuona Kuhani Mussa anakuombea na kukupatia vifaa vya kiroho bure extra utalipia lakini kuwaona matapeli hawa, unatakiwa kwenda kuleta kwanza sadaka, with the amount, from 6 figures ndipo uombewe!.

P
 
Hizo ni biashara za watu. Labda kwa ushauri taasisi za ya kidini (wakristo) wakemee kwa kufanya usajili hayo makanisa ili kuwabana wahusika.

Matendo hayo yanaleta image mbaya kwa taasisi na wakristo wote, ni vizuri taasisi kubwa za kikristo kuwa na mamlaka ya kukemea hata kufungia hao manabii.
 
Uko sahihi mkuu,tatizo ukiwahoji sana wanasema wanakula kwa urefu wa kamba..binafsi sioni shida "wajinga" wakipigwa...as long as hawajalazimishwa! Mjini mipango unadhani wataishije..siku zote masikini ndio waathirika wakubwa..na kwakua hawatumii akili zao vizuri!

Biblia yenyewe imesema "watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa" waache wapigwe mkuu..tena wapigwe sana! Mijitu inajifanya imebobea kwenye dini huiambii kitu,iache ipigwe.
 
Wanabodi
Kama kawa kila nipatapo fursa huja na makala zangu elimishi za kwa maslahi ya taifa. Topic ya leo, ni kutoa wito kwa

Baada ya kuingia kumuona, mtumishi atakuambia prophesy yako na ku conclude matatizo yako yote, ya kiuchumi, umasikini, maradhi, au majanga yoyote, ni umelongwa na watu wa jijijini kwako!.


Naomba kuwasilisha.

Paskali
Wenzetu waliona mbali ndomaana leo hii China imekuwa nchi ya pili kwa uchumi duniani.

Sisi bado tunaambiwa taifa teule ni Israel tu, hivyo hata kama sisi ni masikini tunapaswa kuwachangia katika vita vinavyohusu masilahi yao binafsi ili tubarikiwe.

Wengine wanasema siku ya kiama Mungu ataongea kiarab tu, hivyo tupambane kukijua.
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    45.6 KB · Views: 8
Sasa kama Chama kinaenda kuwaomba hao watumishi waingie kwenye siasa sababu wana mtaji wa watu alafu afu at the same time utarajie serikali kuja na sheria za kuwabana hiyo ni kama ule msemo wa Tanzania bila ukimwi inawezekana.
 
Japo haya ni mambo ya imani, na waumini wanakwenda wenyewe kwa hiyari yao na wana toa fedha kwa ridhaa zao, na serikali yetu imetoa uhuru wa kuabud
Mkuu Pascal.
Hapa ndipo ilipo pointi ya msingi.
Ukishasema walikwenda kwa hiari yao na wanatoa fedha kwa ridhaa zao na serikali imetoa uhuru wa kuabudu.
Kuingilia kwa serikali ni kuvunja haki za watu hao wenye akili zao, hiari yao kutoa pesa.

Maswali ya msingi.
Mchungaji anataka pesa ya nini ili mtoto aweze kurudishwa? Je pasipo kupata hiyo pesa mtoto hawezi kurudi?

Kuna chaka hawa watu wamelipata roho mtakatifu kanionyesha maono.
Hili chaka linaumiza maskini wengi.
 
Back
Top Bottom