magode
JF-Expert Member
- Oct 2, 2014
- 2,204
- 3,336
Wanajamvi
Salaam,
Nchi yetu haina Dini na kila mtu ana uhuru wa kuabudu dini yoyote kama tu havunji sheria. Yaani Kwa Tanzania ukisajili taasisi ya dini, hata ukiwalisha waumini wako mijusi hakuna shida Kwa sababu ni uhuru wao.
Ukiangalia nchi yetu Kwa sasa ina utitiri wa Makanisa ya kiroho, ambayo yanashindana kufanya kile wanachoita miujiza ili kuvutia watu.
Ukifanya uchunguzi hata kidogo tu, utabaini kwamba ile inayoitwa miujiza ni utapeli wa wazi. Wale wanaotumika kutoa ushuhuda ni watu ambao wanapangwa Kwa ustadi na wanalipwa pesa na viongozi wa hayo Makanisa.
Karibu Makanisa yote Haya yanayojiita ya kiroho, yana lengo moja tu la kukusanya pesa kutoka Kwa watu masikini na wale wa daraja la kati. Watu wanafilisika Sana Kwa kutoa kila kitu kuwapelekea hao watumishi wa Mungu ambao kwangu mm ni matapeli.
Kule Japan kilichomkuta waziri mkuu wa zamani Shinzo abe ni matokeo ya dhuruma za watumishi wa Mungu. Shinzo abe Kwa kushirikiana na jamaa zake walikuwa na dhehebu kiroho, kijana aliyempiga risasi alimpiga risasi Kwa sababu, mama wa huyo kijana alikuwa muumini wa Kanisa lao ambaye alichukua pesa zote na kupeleka katika dhehebu la kina Shinzo Abe.
Baada ya kufilisika na familia kuanza Kupitia dhiki, Yule kijana akajawa na Hasira akaanza kujitengenezea bunduki yake ambayo Ndo alikuja kumwadhibu nayo Shinzo abe.
Nakushauri serikali ichukue hatua Kwa Haya Makanisa. Kwanza ifanye research kuthibitisha hiki ninachokiandika hapa. Serikali inaweza isiyafungie Lkn iweke ukomo wa waumini kutoa pesa kanisani.
Kama mchungaji anataka kujenga Kanisa apeleke mchoro serikalini na serikali ielekeze jinsi ya kuwachangisha waumini wake. Ni ujinga tena wa hatari kuendelea kuwaacha hawa matapeli wakiendelea kupora pesa za wanyonge.
Watu wana matatizo mengi sana ya kisaikolojia, na wachungaji wanatumia udhaifu huo kuwachukulia hata akiba zao za kujikimu. Magufuli alisema hakuna uhuru usio ni mipaka. Uchunguzi wa bbc umeonyesha hata marehemu Tb Joshua alikuwa mbakaji na tapeli.
Serikali imeweka sheria nyingi tu za kukusanya kodi, kodi ambayo kimsingi inawarudia wananchi Kwa kufanyia shughuli za maendeleo. Kwa nini serikali iache hizi pesa zichukuliwe tu na hawa wahuni Kwa kigezo cha dini!? Kama lengo lao ni kuwasaidia watu kuacha dhambi na wao ni watu wa Mungu hizo pesa wanazotumia kufanya anasa ni za nini!? Serikali chukueni hatua haraka.
Nawasilisha.
08/01/2024.