Lubebenamawe
JF-Expert Member
- Oct 27, 2014
- 1,952
- 2,194
Huko kukodi ni kwa kila mwaka mbona kama ni hivyo ni upigaji mkubwa sana.Chini ya dr Menard Kalemani tuliambiwa tanesco tayari ilikua inajiendesha yenyewe na taarifa ya mwisho ya hesabu shirika lilianza kupata faida.
Asili ya tanesco kua mzigo ni kugeuzwa shamba la bibi na wapigaji. Mikataba ya uzalishaji ya kinyonyaji na makampuni binafsi na ubadhilifu wa vigogo ndio ilikua kawaida.
Baada ya Rais kumuondoa Kalemani na kumuweka Januari Makamba wa tu wameshituka. Huo ndio ukweli mtupu. Wananchi hawamuamini Januari kutokana na kauli zake na kundi lao kukejeli na kudharau juhudi za Magufuli alipokuwa Rais.
Makamba ameanza kuweka watu wake kwenye bodi wakiwepo wafanyabiashara wakubwa halafu mara shirika linaingia mkataba wa kukodi software eti ya managrment kwa dola za kimarekani milioni 30.
Kama Serikali imefanya uchunguzi wa nani anataka kupewa kandarasi za kujenga meli za shirika la meli 'due diligence' na kukuta madudu ya kutisha tungependa wafanye pia uchunguzi kama ilikua lazima kukodi software ya management na kwa bei hiyo kubwa ya kushangaza. Na pia kama utaratibu wa manunuzi wa serikali haujakiukwa.
Kuna watu nchini wanasifiwa tu wakati ujuzi wao ni kutoa kandarasi za kipigaji tu. Inavyofahamika nchini kuna wajuzi wazuri wa tehama na wameweza kutengeneza software nzuri zinatumika na serikali. Hawa kina Januati na timu yake ameweka tanesco ni sawa na wale walitaka kupeleka ndege ya air tanzania afrika ya kusini kuweka nembo na maandishi ya kampuni kwa dola millioni kadha.
Ikiwa tunataka kuendelea lazima tusimamishe upigaji.
Kwa hivyo tunataka uchunguzi wa ukodishaji hiyo software vinginevyo hayo ya bandari tutaona ni 'selective' action kufanya show tu. Ni mambo yale ya awamu ya nne yaani usanii tu.