TANESCO yasaini mkataba wa kuzalisha Umeme Jua MW 150 Kwa Bilioni 275. Waziri Makamba apiga marufuku mauziano ya Umeme kwa Dola

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,785
Serikali Kupitia Tanesco imeandika Historia ya kusaini mkataba wa Kuzalisha Umeme wa Juna na kampuni ya China wenye thamani ya Shilingi Bilioni 275 ambao utazalisha megawatt 150 Kishapu ,Shinyanga na Kwa awamu ya kwanza Wataanza na megawatt 50.

Waziri wa Nishati January Makamba akishuhudia mkataba huo amepiga marufuku Tanesco kununua Umeme kutoka Kwa wazalishaji Kwa malipo ya dola badala yake Shilingi ndio ittumika..

Aidha amewataka Tanesco kuwawezesha wazawa Ili waweze kuzalisha umeme akisema hakuna maajabu Hadi wao washindwe..

My Take
Hongera sana Makamba,majungu achilia failures wewe endelea kuchapa kazi.

=======

Wizara ya Nishati kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imesaini mkataba wa kwanza wa uzalishaji wa umeme Jua wa kiasi cha megawati 50 utakaotekelezwa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Mkataba huo umesainiwa tarehe 29 Mei, 2023 jijini Dodoma na kushuhudiwa na Waziri wa Nishati, Mhe.January Makamba ambaye alikuwa mgeni rasmi.

Kwa ujumla mradi huo wa umeme wa Jua ni wa megawati 150 ambapo awamu kwanza itajengwa mitambo itakayozalisha megawati 50 na awamu ya pili itajengwa mitambo ya megawati 100 kwa jumla ya shilingi bilioni 275. Utekelezaji wa mradi wa Awamu ya kwanza hautazidi miezi 12.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Nishati amesema kuwa “kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi tunaingiza umeme wa Jua katika gridi ya Taifa, nimpomgeze Rais wetu kwa kwa muongozo na uongozi ambao umepelekea nchi kuaminiwa na washirika wa maendeleo ikiwemo Shirika la Maendeleo la Ufaransa ambalo limetoa mkopo ambao utatekeleza mradi huu.”

Ameeleza kuwa, utekelezaji wa mradi huo wa Jua ni jitihada za Serikali za kuhakikisha inatengeneza mchanganyiko wa umeme wenye afya katika gridi ya Taifa ambao utatokana na vyanzo mbalimbali kama vile maji, gesi, upepo na Jua ili hata pale chanzo moja kinapotetereka, vyanzo vingine vitaendelea kuzalisha umeme.

Waziri Makamba amesema kuwa, ili kuongeza zaidi uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati jadidifu, Serikali inakuja na Sera mpya ya Nishati Jadidifu (iko kwenye maandalizi) ambayo itasaidia nchi kuongeza uwekezaji kwenye eneo hilo kwani fedha nyingi duniani, masoko ya mitaji na teknolojia mpya zinajielekeza kwenye nishati jadidifu.

Ameongeza kuwa, kwa sasa kazi inayofanyika pia ni kuainisha maeneo yaliyo na rasilimali ya nishati jadidifu na kipaumbele kitakuwa kwa wazawa kuwekeza kwenye miradi kama ya Upepo na Jua na Serikali itawaunga mkono na kwamba Serikali itakuja na muongozo wa utekelezaji wa suala hilo.

Ameongeza kuwa, kwa maeneo yaliyo nje ya gridi kama vile visiwa, bado Serikali itaendelea kuwezesha jitihada za kupelewa umeme kwa kutumia miradi ya nishati jadidifu kama vile Jua na Upepo.
 
Serikali Kupitia Tanesco imeandika Historia ya kusaini mkataba wa Kuzalisha Umeme wa Juna na kampuni ya China wenye thamani ya Shilingi Bilioni 275 ambao utazalisha megawatt 150 Kishapu ,Shinyanga na Kwa awamu ya kwanza Wataanza na megawatt 50.
Issue sio kuzalisha hata Jangwani wanaweza kuzalisha kuzalisha ma_gigawatt let alone Megawatt issue ni tunazitunza vipi hizo megawatt ili wakati hakuna jua tuzitumie ? (Storage bado ni bottleneck kwenye solar)
Waziri wa Nishati January Makamba akishuhudia mkataba huo amepiga marufuku Tanesco kununua Umeme kutoka Kwa wazalishaji Kwa malipo ya dola badala yake Shilingi ndio ittumika..

Aidha amewataka Tanesco kuwawezesha wazawa Ili waweze kuzalisha umeme akisema hakuna maajabu Hadi wao washindwe..
Kwanini wanunue ili wauze ?, Kwanini wazimalize Bwawa la JKN haraka na lianze kazi ili badala ya kununua wao ndio wauze ?
 
Issue sio kuzalisha hata Jangwani wanaweza kuzalisha kuzalisha ma_gigawatt let alone Megawatt issue ni tunazitunza vipi hizo megawatt ili wakati hakuna jua tuzitumie ? (Storage bado ni bottleneck kwenye solar)

Kwanini wanunue ili wauze ?, Kwanini wazimalize Bwawa la JKN haraka na lianze kazi ili badala ya kununua wao ndio wauze ?
Wewe una shida mahala
 
Wewe una shida mahala
People, Issues, Events....... Wengi tunachochagua ku-invest muda wetu, no wonder vingi vinavyofanyika sio endelevu....

Badala ya ku-pinpoint wapi nimekosea unajaza server kwa kuniongelea mimi a non entity katika mjadala huu.....
 
Back
Top Bottom