Rais Samia akiwa ziara ya kitaifa nchini India, leo Oktoba 9, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ziara ya kitaifa nchini India tarehe 9 Oktoba, 2023.


Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania na India zimekubaliana kukuza uhusiano wao wa kihistoria baina ya mataifa hayo mawili kwa kiwango cha Ushirika wa Kimkakati.

Rais Samia ameyasema hayo wakati wa mutano na waandishi wa habari katika ziara yake ya kitaifa ya siku 3 nchini India.

Miongoni mwa masuala ambayo viongozi hao wameyawekea msisitizo katika ushirikiano ni pamoja na ulinzi, nishati, kujenga uwezo, usalama wa majini, biashara na uwekezaji.

Hadi kufika mwaka 2022, kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbili ulifikia dola za Kimarekani bilioni 3.1, hivyo kuifanya India kuwa mshirika wa tatu kwa ukubwa katika biashara na mwekezaji wa tano kwa ukubwa nchini Tanzania.

Wakati huo huo, nchi hizo mbili zimetia saini hati za makubaliano 14 na mkataba mmoja, ambapo hati 10 zimehusisha taasisi za serikali na mitano ni za sekta binafsi.

Mbali na kuwa tayari India inaisaidia Tanzania katika masuala ya ubobezi wa kupandikiza figo na uboho (bone marrow), pia viongozi hao wamejadili namna ya kuanzisha kituo cha dawa asilia.

Rais Samia ameshukuru pia kwa kuanzishwa kampasi ya kwanza ya chuo cha IIT nje ya India chenye hadhi ya juu katika masuala ya teknolojia visiwani Zanzibar kitakachowanufaisha wanafunzi mbalimbali, siyo tu wa Tanzania ila hata nje ya mipaka.

Masuala mengine yaliojadiliwa katika ziara ya Rais Samia ni pamoja na usalama wa mitandao, kushirikisha vijana hasa kupitia vuo vya VETA, kutoa mafunzo kwa wahandisi wa madini, kushirikiana kwenye kilimo na miradi ya maji.

IMG_8705.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa India Mhe. Droupadi Murmu pamoja na Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi mara baada ya kuwasili Ikulu ya India (Rashtrapati Bhawan) New Delhi nchini humo.
IMG_8706.jpeg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na ujumbe wake akiwa na Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi katika mazungumzo Rasmi katika Jengo Maalum la kupokelea wageni wa Kitaifa Hyderabad House New Delhi Nchini India.
IMG_8707.jpeg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi wakati wakizungumza na Waandishi wa Habari katika Jengo Maalum la kupokelea wageni wa Kitaifa Hyderabad House New Delhi Nchini India
 
Ziara zisizo na tija kwa nchi...kaambatana na lundo la mawaziri na maofisa wengine wa serikali.
Sa100 sio mchumi hata kdg, ziara zake ni hasara kuliko faida, achilia mbali mikataba ya hovyo anayoingia!.
 
T
Ziara zisizo na tija kwa nchi...kaambatana na lundo la mawaziri na maofisa wengine wa serikali.
Sa100 sio mchumi hata kdg, ziara zake ni hasara kuliko faida, achilia mbali mikataba ya hovyo anayoingia!.
That is the worst of you
 
Chonde mama kuwa makini sana.
Kumbuka yule waziri mpigaji alikutangulia huko!
Huenda aliwahi yeye na "rostitamu" kuipiga nchi tena!
 
Ziara zisizo na tija kwa nchi...kaambatana na lundo la mawaziri na maofisa wengine wa serikali.
Sa100 sio mchumi hata kdg, ziara zake ni hasara kuliko faida, achilia mbali mikataba ya hovyo anayoingia!.
Mbona bwana yule alichukua wauza mayai, manabii na mitume, yaani watu 200 huku wengi wakiwa manyangarakasha, waliporudi mpaka sasa hakuna mrejesho.
 
Tanzania na India zimetia saini hati za makubaliano 14 na mkataba mmoja, ambapo hati 10 zimehusisha taasisi za serikali na tano za sekta binafsi.Katika mkutano wa pamoja na waadhishi wa habari, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, na Waziri Mkuu wa India, Mhe. Narendra Modi wameshuhudia makabidhiano ya hati 6 kati ya zile zilizosainiwa ambazo zinajumuisha:

1. Hati ya makubaliano kati ya Wizara ya Elektroniki na Teknolojia ya Habari ya India na Wizara ya Habari, Mawasiliano, na Teknolojia ya Habari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu ushirikiano katika nyanja ya kupeana suluhu zenye mafanikio za kidijitali zinazotekelezwa kwa ujuzi wa idadi ya watu kwa ajili ya mabadiliko ya kidijitali.

2. Mabadilishano ya Hati ya makubaliano ya kiufundi kati ya Jeshi la Wanamaji la India na Shirika la Wakala wa Meli wa Tanzania kuhusu kupeana taarifa za meli za kibiashara.

3. Hati ya makubaliano ya mpango wa kubadilishana utamaduni kati ya India na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka ya 2023 - 2026.

4. Hati ya makubaliano kati ya Baraza la Michezo la Taifa la Tanzania na Mamlaka ya Michezo ya India kuhusu Ushirikiano katika Sekta ya Michezo.

5. Hati ya makubaliano kati ya Mamlaka ya Bandari ya Jawaharlal Nehru chini ya Wizara ya Usafirishaji wa Bandari na Njia za Majini ya India na Kituo cha Uwekezaji Tanzania kwa ajili ya kuanzisha Kongani ya Biashara nchini Tanzania.

6. Hati ya makubaliano kati ya Coaching Shipyard Limited na Marine Services Cooperation Limited kuhusu ushirikiano katika Sekta ya Usafiri wa Majini
 
Ziara zisizo na tija kwa nchi...kaambatana na lundo la mawaziri na maofisa wengine wa serikali.
Sa100 sio mchumi hata kdg, ziara zake ni hasara kuliko faida, achilia mbali mikataba ya hovyo anayoingia!.
Mapimbi wako wengi duniani
Unaambiwa mikataba 15 , imetiwa saini 10 ikiwa ya serikali na mitano ya wafanya bishara.
Hivi unaichukuliaje Ziara kama hii kama TZ imekubaliana na India kutumia Sarafu zao katika bashara badala ya US dolla?
Mmi nadhani wewe Pimbi usiyejua mambo ya Uchumi na Mahusiano ya Kimataifa na Uchumi.
India ni mnunuaji mkubwa wa Mbaazi na Nafaka ikiwemo Korosho.
India Ina idadi kubwa ya Watu zaidi ya 1.3 Bilion ambao ukiambiwa uuze Nafaka zetu zote Tz basi hatuwezi kulisha hata robo ya population.
Usidharau soko kubwa la taifa kubwa kama India.
Wewe Ni Pimbi uliye na msongo wa Akili
Pole sana
Unahitaji kufanyiwa Upasuaji wa Ubongo
 
Back
Top Bottom