Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 3,721
- 11,717
1. Serikali isitishe kwa muda matumizi yasiyo ya lazima (anasa) yanayohitaji fedha za kigeni kama vile kununua magari ya kutembelea viongozi na safari za nje ya nchi (zote mpaka za SSH hazina tija).
2. Kampuni za ndani zitakazolipwa kwa shilingi zipewe kipaumbele kwenye miradi ya ujenzi na uwekezaji mwingine.
3. Serikali isitishe kukopa mikopo ya nje. Kwasasa mapato yetu ya fedha za kigeni mengi yanaishia kuhudumia madeni ya nje yaliyokopwa kwa pupa na serikali hii ya SSH kwa ushauri mbovu wa Mwigulu. Serikali isiongeze mzigo mwingine. Ikope ndani kwa kuuza bondi na njia nyinginezo.
4. Wizara ya fedha na wizara ya mipango ziwekwe chini ya ofisi ya makamu wa rais. Ni wazi kuwa hizo wizara mbili wameshindwa kujisimamia, na mamlaka kuu haina ujuzi wala uwezo wa kuzisimamia. Ni vema kazi hiyo apewe Dr. Mpango kwa wizara hizo kuwekwa chini yake rasmi.
5. Tunakaribia kutumbukia kwenye mgogoro mkubwa wa kiuchumi, majibu ya kisiasa na shortcuts haziwezi kusaidia. Siasa maji taka za kutoa "ufafanuzi" na matamko ya kijingajinga hayatatufikisha popote. Na wala kuvutia uwekezaji wa nje kwa njia za kihuni na rushwa hauwezi kutufikisha popote zaidi ya kutengeneza matatizo mengine.
Hauwezi kuuficha mdororo wa kiuchumi, sote tunaona kinachoendelea kwenye upatikanaji wa mafuta. Serikali ichukue hatua haraka.